Njoo, Unifuate
Novemba 30–Desemba 6. Moroni 1–6: “Kuwaweka kwa Njia Nzuri”


“Novemba 30–Desemba 6. Moroni 1–6: ‘Kuwaweka kwa Njia Nzuri,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Novemba 30–Desemba 6. Moroni 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
Alma Anabatiza watu Katika Maji ya Mormoni

Minerva Teichert (1888–1976), Alma Anabatiza katika Maji ya Mormoni, 1949–1951, mafuta kwenye masonite, inchi 35⅞ x 48. Sanaa ya Jumba la Makumbusho la Chuo kikuu cha Brigham Young, 1969

Novemba 30–Desemba 6

Moroni 1–6

“Kuwaweka kwa Njia Nzuri”

Kabla hujaanza kupanga shughuli za kujifunza kwa ajili ya watoto, kwa sala soma Moroni 1–6, ukitafuta kanuni na mistari ambayo unahisi wanahitaji kuelewa.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kushiriki kile ambacho wamekuwa wakijifunza kuhusu Moroni. Ungeweza kutumia “Mlango wa 53: Moroni na Mafundisho yake” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 154–55, au video zinazohusiana katika ChurchofJesusChrist.org) ili kuwasaidia kukumbuka.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Moroni 4–5

Ninapokea sakramenti kuonyesha kwamba daima nitamkumbuka Yesu Kristo.

Sakramenti inaweza kuwa uzoefu mtakatifu wa kiroho—hata kwa watoto wadogo. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kutumia muda wakati wa sakramenti kumfikiria Yesu?

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha ya watu wakipokea sakramenti (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.108). Waombe watoto wakuambie nini kinatendeka wakati wa sakramenti. Nini tunapaswa kuwa tunafanya wakati wa sakramenti?

  • Waalike waumini wawili wa kata kuja darasani ili kusoma Moroni 4:3 na 5:2 kwa watoto na shiriki kwa nini wanapokea sakramenti kila wiki. Waombe wapendekeze mambo watoto wanayoweza kufanya ili kuwasaidia kumfikiria Yesu wakati wa sakramenti na daima kumkumbuka Yeye.

  • Imba wimbo unaowasaidia watoto kumfikiria Yesu, kama vile “Reverently, Quietly” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 26). Waombe watoto kufanya mazoezi kukaa kwa unyenyekevu kama ambavyo wangefanya wakati wa sakramenti.

Moroni 6:1–3

Ninaweza kujiandaa kwa ajili ya kubatizwa.

Maelezo ya Moroni ya watu waliobatizwa katika siku yake yanaweza kuwasaidia watoto kujiandaa kupokea ibada hii muhimu leo.

Shughuli za Yakini

  • Soma vifungu vya maneno kutoka Moroni 6:1–3 ambavyo vinafundisha nani anaweza kubatizwa. Fafanua maneno ambayo watoto wanaweza wasiyaelewe. Kwa mfano, maana moja ya “moyo uliopondeka na roho iliyovunjika” ni kujutia dhambi zetu (Moroni 6:2). Simulia kuhusu jinsi ulivyojiandaa kubatizwa, au muulize mtu aliyebatizwa karibuni kuelezea jinsi alivyojiandaa. Wasaidie watoto kufikiria jinsi wanavyoweza kujiandaa kubatizwa siku moja.

  • Onyesha picha za watu wakibatizwa (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 103, 104), na waruhusu watoto kuzungumza kuhusu kile wanachokiona kwenye picha. Wasaidie kugundua kila kitu, kama vile maji na nguo nyeupe. Waulize watoto kwa nini tunabatizwa, na elezea kwa nini ulichagua kubatizwa.

Moroni 6:4–6, 9

Ninabarikiwa pale ninapokwenda kanisani.

Je, watoto unaowafundisha wanaelewa kwa nini tunaenda kanisani kila wiki? Moroni 6 inatoa baadhi ya sababu muhimu.

Shughuli za Yakini

  • Waulize watoto kwa nini wanapenda kwenda kanisani, na wasaidie kutaja baadhi ya mambo tunayofanya kanisani. Wasomee baadhi ya mambo haya kutoka Moroni 6:4–6, 9, na waalike kuigiza au kuchora picha zao wenyewe wakifanya baadhi ya mambo haya (kama vile kusali, kuhubiri, kuimba, na kupokea sakramenti).

  • Wasaidie watoto kuimba wimbo kuhusu kuhudhuria kanisani, kama vile “When I Go to Church” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,157). Waambie watoto kwa nini unapenda kwenda kanisani na jinsi kufanya hivyo kulivyokubariki.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Moroni 2–6

Roho Mtakatifu ni kipawa kitakatifu.

Roho Mtakatifu ametajwa mara kadhaa katika Moroni 2–6. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia milango hii kuwasaidia watoto kuelewa jinsi Roho Mtakatifu anavyoweza kuwasaidia?

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto watafute kila mstari katika Moroni 2–6 ambao unamtaja Roho Mtakatifu au Roho. Someni kila moja ya mistari hii pamoja, na waombe watoto waorodheshe ubaoni mambo wanayojifunza kuhusu Roho Mtakatifu. Ni kwa namna gani Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia?

  • Waambie watoto kuhusu wakati ambapo ulihisi ushawishi wa Roho Mtakatifu, kanisani au pengine popote. Elezea jinsi ulivyojua alikuwa ni Roho Mtakatifu na jinsi Alivyokusaidia. Waalike watoto kushiriki uzoefu wowote waliowahi kuwa nao na Roho Mtakatifu, na wahimize kutafuta ushawishi Wake.

    Picha
    msichana akipokea baraka

    Kipawa cha Roho Mtakatifu hutolewa kwa kuwekewa mikono.

Moroni 4–5

Ninapokea sakramenti kuonyesha kwamba daima nitamkumbuka Yesu Kristo.

Wakati watoto wanapoelewa utakatifu wa sakramenti, wanaweza zaidi kuichukulia kwa unyenyekevu na kuhisi karibu na Mungu wakati wa ibada hii.

Shughuli za Yakini

  • Andika vifungu vya maneno kutoka Moroni 4:3 na 5:2 kwenye vipande tofauti vya karatasi, na waombe watoto kuweka vifungu vya maneno katika mpangilio sahihi. Kulingana na mistari hii, kwa nini sakramenti ni muhimu?

  • Waalike watoto kufikiria kwamba rafiki anakuja kwenye mkutano wa sakramenti kwa mara ya kwanza. Ni kwa jinsi gani wanaweza kumuelezea rafiki sakramenti ni nini na kwa nini tunaipokea? Wahimize kutumia Moroni 4:3 na 5:2 katika maelezo yao.

  • Waalike watoto washiriki mambo ambayo familia zao hufanya wakati wa sakramenti ili kuwa wanyenyekevu na kumfikiria Yesu Kristo. Ni mawazo gani mengine wanayo? Waalike kuchukua moja ya mawazo haya na kuweka lengo la kutumia muda zaidi kumfikiria Mwokozi wakati wa sakramenti.

Moroni 6:4–6, 9

Tunakwenda kanisani kupokea sakramenti na kusaidiana sisi kwa sisi.

Maneno ya Moroni yangeweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kupata lengo katika kuja kanisani kila wiki.

Shughuli za Yakini

  • Andika Kwa nini tunakuja kanisani? Ubaoni, na waombe watoto kuandika majibu yanayowezekana. Waalike watafute majibu ya ziada katika Moroni 6:4–6, 9 na yaongeze kwenye orodha ubaoni. Waalike watoto kushiriki jinsi ambavyo wamebarikiwa kwa kuhudhuria kanisani. Waache waigize kumuelezea rafiki au mtu wa imani nyingine kwa nini wana shukrani kuwa Kanisani.

  • Onyesha picha au mifano ya vyakula vyenye lishe. Kwa nini ni muhimu kulisha miili yetu? Someni pamoja Moroni 6:4, na waulize watoto kile wanachofikiria kifungu cha maneno “kulishwa na neno nzuri la Mungu” humaanisha. Ni jinsi gani neno la Mungu linatupa lishe?

  • Mualike mmoja wa watoto asome nukuu ifuatayo kutoka kwa Mzee Jeffrey R. Holland, na kujadili kile inachofundisha kuhusu jinsi tunavyoweza kulishana sisi kwa sisi: “Watu wengi huwa hawaji Kanisani kutafuta tu kweli chache za injili ama kuonana na marafiki wa zamani, ingawa hayo yote ni muhimu. Huwa wanakuja kutafuta uzoefu wa kiroho. Wanataka amani. Wanataka imani yao iimarishwe na tumaini lao kufanywa upya. Wanataka, kwa ufupi, kulishwa na neno jema la Mungu, kuimarishwa na nguvu za mbinguni” (“Mwalimu Anatoka kwa Mungu,” Ensign, Mei 1998, 26). Tunawezaje kusaidia kulishana kiroho kanisani?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kuzungumza na familia zao kuhusu sababu zinazowafanya wanapenda kuhudhuria kanisani kila wiki.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Saidia Wazazi. Kwa sala tafuta njia za kuwasaidia wazazi wa watoto unaowafundisha. Ni kwa jinsi gani unaweza kuunga mkono juhudi zao za kufundisha injili kwa watoto wao? Kwa mfano, unaweza kuzungumza na wazazi kuhusu mahitaji na mambo wanayopendelea watoto wao au unaweza kushiriki nao juu ya yale watoto wao wanajifunza darasani (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).

Chapisha