“Novemba 23–29. Etheri 12–15: ‘Kwa Imani Mambo Yote Yanatimizwa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Novemba 23–29. Alma 12–15,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020
Novemba 23–29
Etheri 12–15
“Kwa Imani Mambo Yote Yanatimizwa”
Unaposoma Etheri 12–15, fikiria kuhusu watoto unaowafundisha. Mawazo ya shughuli katika muhtasari huu yanaweza kukupa msukumo kwenye mawazo mengine ambayo yatakusaidia kukidhi mahitaji ya watoto katika darasa lako.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Wasaidie watoto kufikiria andiko au hadithi kuhusu watu walioonyesha imani kubwa. Baadhi ya mifano inapatikana katika Etheri 12:11–22.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Imani ni kusadiki katika mambo ambayo hatuwezi kuyaona.
Moroni anashiriki mifano kadhaa ya watu waliofanikisha mambo makubwa kwa sababu ya imani yao. Fikiria jinsi unavyoweza kutumia mifano hii kuwafundisha watoto imani ni nini.
Shughuli za Yakini
-
Wasomee watoto “imani ni vitu ambavyo vinatumainiwa na havionekani” kutoka Etheri 12:6, na waombe kurudia kifungu hiki cha maneno pamoja nawe. Waambie watoto kuhusu vitu unavyoviamini japokuwa huwezi kuviona, na wasaidie watoto kufikiria mifano zaidi. Wimbo “Faith” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96–97), au wimbo mwingine kuhusu imani, unaweza kusaidia.
-
Onyesha picha zinazoelezea mifano ya imani katika Etheri 12:13–15, 20–21 (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 78, 85, na ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Waache watoto wakuambie kile wanachoona katika picha na kile wanachojua kuhusu hadithi hizi. Zungumza na watoto kuhusu jinsi watu hawa walivyoonyesha imani na kile kilichotokea kwa sababu ya imani yao.
-
Cheza mchezo wa kubahatisha pamoja na watoto. Wape dokezo kuhusu watu waaminifu walioelezewa katika Etheri 12:13–15, 19–20 mpaka watoto waweze kubahatisha watu hao ni akina nani. Kisha waache watoto wacheze mchezo tena kwa kufanya zamu kutoa dokezo kuhusu watu hao hao (au watu wengine waaminifu) wakati watoto wengine darasani wakibahatisha. Shiriki kile unachovutiwa nacho kuhusu imani ya watu hawa.
Yesu Kristo anaweza kunisaidia kuwa imara.
Watoto wakati mwingine wanakumbana na hali ambazo kwazo wanahisi wadhaifu, kama vile Moroni alivyohisi. Wasaidie kujifunza kile Moroni alichojifunza—kwamba Mwokozi anaweza “kufanya vitu dhaifu kuwa vya nguvu” (Etheri 12:27).
Shughuli za Yakini
-
Waelezee watoto jukumu ambalo lingehitaji nguvu kubwa ya kimwili kulikamilisha. Waalike washiriki mifano ya mambo ambayo hawako imara vya kutosha kuyafanya sasa. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa imara vya kutosha kukamilisha majukumu haya? Elezea kwamba sisi pia tuna kazi ya kiroho ya kufanya, lakini wakati mwingine tunahisi wadhaifu kiroho. Moroni alihisi hivi kuhusu maandishi yake kwenye bamba. Soma Etheri 12:27 kwa watoto. Ni nini Bwana aliwaahidi wale wanaohisi wadhaifu?
-
Shiriki uzoefu ambapo Mwokozi alikusaidia au alimsaidia mtu mwingine unayemjua kufanya jambo gumu. Shuhudia kwa watoto kwamba kama watatafuta msaada Wake, Yesu anaweza kuwasaidia kuwa imara, hata wakati wanapohisi wadhaifu.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Imani ni kusadiki katika mambo ambayo hatuwezi kuyaona.
Watoto unaowafundisha wanajenga msingi wa shuhuda zao. Ushauri wa Moroni kuhusu imani, unaopatikana katika Etheri 12:6, unaweza kuwasaidia.
Shughuli za Yakini
-
Elezea kwamba nabii Etheri alijaribu kuwafundisha Wayaredi “vitu vikubwa vya ajabu,” lakini hawakuamini kile alichosema. Waalike watoto wasome Etheri 12:5 ili kujua ni kwa nini hawakuamini. Nini baadhi ya vitu Baba wa Mbinguni anataka tuamini hata kama hatuvioni? Someni pamoja Waebrania 12:6. Ni nini Moroni aliwafundisha watu ambao hawangeamini kweli za kiroho kwa sababu hawakuziona?
-
Muonyeshe mmoja wa watoto picha bila wengine kuiona, na muombe mtoto kuelezea picha kwa watoto wengine darasani. Kadiri muda unavyoruhusu, waruhusu watoto kwa zamu wafanye tendo sawa na hilo kwa kutumia picha tofauti. Kisha waalike kusoma Etheri 12:6 na kutafuta kifungu hiki cha maneno: “Imani ni vitu ambavyo vinatumainiwa na havionekani.” Ni kwa jinsi gani tunaonyesha imani katika Yesu Kristo wakati hatumwoni?
-
Waombe watoto wasome kifungu hiki cha maneno katika Etheri 12:6: “Hamtapata ushahidi wowote mpaka baada ya majaribu ya imani yenu.” Wasaidie watoto kuelewa kwamba tunapotii amri, tunaweza kujua kwamba ni ya kweli. Waombe wafikirie kanuni za injili ambazo Mungu anataka tuwe na ushuhuda nazo, kama vile kulipa zaka, kuitakasa Sabato, au kuishi Neno la Hekima. Kisha andika ubaoni Ili kupata ushuhuda wa , Ninapaswa . Shiriki jinsi ulivyoonyesha imani ili kupata ushuhuda wako wa kweli hizi na zingine za injili.
Tumaini ni kama ngao ya nafsi yangu.
Wasaidie watoto unaowafundisha kuelewa kwamba tunaweza “kutumaini ulimwengu bora” kwa sababu ya imani yetu katika Kristo (Etheri 12:4).
Shughuli za Yakini
-
Shiriki pamoja na watoto maana ya tumaini inayopatikana katika “Tumaini( Mwongozo kwenye Maandiko, scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Kulingana na maana hii na Etheri 12:4, 32, ni nini tunapaswa kukitumainia? (ona pia Moroni 7:40–42). Wasaidie watoto kufikiria maneno mengine kwa ajili ya tumaini, pamoja na maneno ambayo yanamaanisha kinyume cha tumaini. Shiriki pamoja nao baadhi ya kweli za injili ambazo hukupa tumaini, na waalike kufanya vivyo hivyo.
-
Onyesha (au chora ubaoni) picha ya meli na nanga. Kwa nini meli zinahitaji nanga? Nini kingeweza kutokea kwenye meli ambayo haina nanga? Someni pamoja Etheri 12:4, na waulize watoto ni kwa jinsi gani tumaini ni kama nanga. Waalike watoto kuchora picha zao wenyewe za meli na nanga ili waweze kuzifundisha familia zao kuhusu tumaini.
Yesu Kristo anaweza kunisaidia kuwa imara.
Watoto wanapokua, wanakuwa na uelewa zaidi wa udhaifu wao. Tumia mistari hii kuwafundisha jinsi Mwokozi anavyoweza kufanya “vitu dhaifu kuwa vya nguvu” (Ether 12:27).
Shughuli za Yakini
-
Waombe watoto wasome Etheri 12:23–25 ili kupata ni kwa nini Moroni alikuwa na wasiwasi. Waulize kama wamewahi kupata hisia sawa na hizo. Kisha waalike wasome mstari wa 26–27 ili kupata ni jinsi gani Bwana alimtia moyo Moroni. Tunahitaji kufanya nini ili Bwana aweze kutusaidia kuwa imara tunapohisi wadhaifu? Shiriki uzoefu ambapo Mwokozi alikusaidia kuwa imara vya kutosha kufanya jambo ambalo lilikuwa gumu.
-
Waalike watoto kuchora picha ya kitu dhaifu na kitu imara. Kisha waalike waongezee kwenye michoro yao baadhi ya maneno na vifungu vya maneno kutoka Etheri 12:23–29 ambavyo vinawafundisha kuhusu jinsi Mwokozi anavyoweza kutusaidia kugeuza udhaifu wetu kuwa nguvu. Wahimize watoto kufikiria kuhusu udhaifu wanaoweza kuwa nao na kisha kutafuta msaada wa Mwokozi ili wawe imara.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto waandike ukweli ambao wangependa kuupatia ushuhuda. Wasaidie kuweka lengo la kutumia imani ili waweze kupata ushahidi wa ukweli huo.