Njoo, Unifuate
Novemba 9–15. Etheri 1–5: “Kupasua Pazia la Kutoamini”


“Novemba 9–15. Etheri 1–5: ‘Kupasua Pazia la Kutoamini,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Novemba 9–15. Etheri 1–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Wayaredi wakisafiri kupitia nyikani

Wayaredi Wakiondoka Babeli, na Albin Veselka

Novemba 9–15

Etheri 1–5

“Kupasua Pazia la Kutoamini”

Unapofanya marejeo ya kile ulichojifunza wakati wa usomaji wako wa Etheri 1–5, ni kweli zipi unahisi kuvutiwa kuwasaidia watoto kugundua? Pengine kuna mawazo katika muhtasari huu ambayo yanaweza kusaidia.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha ya kaka wa Yaredi (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Waalike watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu kaka wa Yaredi.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Ether 1:33–43; 2:16–25; 3:1–6

Baba wa Mbinguni husikia na kujibu sala zangu.

Hadithi ya kaka wa Yaredi huonyesha kwa mfano njia kadhaa ambazo kwazo Mungu anaweza kutusaidia pale tunaposali.

Shughuli za Yakini

  • Waalike waumini kadhaa wa kata wanaofahamu lugha nyingine kusema sentensi kadhaa katika lugha ile kwa ajili ya darasa lako (au weka sauti iliyorekodiwa ya lugha nyingine). Waache watoto wajifanye kuzungumza lugha nyingine, na onyesha jinsi ilivyo vigumu kuelewana wakati hatuzungumzi lugha moja. Tumia hii kutambulisha tukio la Mnara wa Babeli katika Mwanzo 11:1–9 na Etheri 1:33. Soma Etheri 3:13 na 15, na elezea jinsi kaka wa Yaredi alivyoomba kwamba yeye na rafiki zake na familia wangeweza kuelewana (ona Etheri 1:34–37). Soma na wasaidie watoto kuelewa jibu la Bwana kwa ombi lake katika Etheri 1:35. Ungeweza pia kutumia “Mlango wa 50: Wayaredi Wanaondoka Babeli” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 143–44, au video inayohusiana katika ChurchofJesusChrist.org).

  • Waalike watoto wajifanye kujenga mashua, kama ilivyoelezewa katika Etheri 2:16–17. Elezea matatizo waliyokuwa nayo Wayaredi kwenye mashua zao (ona Etheri 2:19), na waulize watoto ni nini wangefanya kuhusu matatizo haya. Soma Etheri 2:18–19 kuwafundisha watoto jinsi kaka wa Yaredi alivyopeleka matatizo yake kwa Bwana katika sala. Shuhudia kwamba daima tunaweza kuomba wakati tunapokuwa na maswali au matatizo.

  • Fanyia ufupisho Etheri 2:19–3:6 kuelezea jinsi Bwana alivyojibu swali la kaka wa Yaredi kuhusu mashua. Weka mawe 16 kote darasani, na waalike watoto kuyahesabu pale wanapoyapata. Onyesha picha kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, na waache watoto warudie kusimulia hadithi (ona pia ukurasa wa shughuli ya wiki hii).

Etheri 3:13, 15

Niliumbwa kwa mfano wa Mungu.

Wakati kaka wa Yaredi alipomwona Bwana, alijifunza kwamba “watu wote waliumbwa katika mwanzo kwa jinsi ya kama maumbile [Yake]” (Etheri 3:15).

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha ya Mwokozi, na waalike watoto kuonyesha sehemu tofauti za mwili Wake. Elezea kwamba wakati kaka wa Yaredi alipomwona Yesu Kristo, alijifunza kwamba sote tunafanana na Yesu. Unapoonyesha kila sehemu ya mwili katika picha, waalike waonyeshe sehemu inayofanana kwenye miili yao wenyewe. Shuhudia kwamba tuliumbwa kufanana na Baba yetu wa Mbinguni na Yesu Kristo.

  • Imbeni pamoja wimbo unaohusiana na miili yetu, kama vile “Head, Shoulders, Knees, and Toes” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 275). Wasaidie watoto kuzungumzia kuhusu kwa nini wana shukrani kwa ajili ya sehemu tofauti za miili yao.

watoto wakikimbia uwanjani

Tumeumbwa kwa mfano wa Mungu.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Etheri 1:33–43; 2; 3:1–17

Ninaweza kupokea ufunuo ili kunisaidia.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujifunza kuhusu ufunuo kutokana na mfano wa kaka wa Yaredi? Ni uzoefu gani unaoweza kushiriki wakati Bwana alipokusaidia kupata suluhisho la matatizo au maswali yako?

Shughuli za Yakini

  • Kabla ya darasa, andika kifungu cha maneno “Simama, geuka, na kaa chini” katika lugha tofauti kwenye vipande kadhaa vya karatasi (ungeweza kutumia mtafsiri wa mtandaoni au usaidizi wa mtu mwingine anayefahamu lugha nyingine). Toa kipande kimoja kwa kila mtoto, na waalike kujaribu kufuata maelekezo. Tumia hiki kuelezea kile kilichochochea sala ya kaka wa Yaredi katika Etheri 1:33–37. Someni mistari hii pamoja, na waombe watoto kusikiliza kwa makini jinsi Bwana alivyohisi kwa Yaredi na rafiki zake na familia. Ni nini tunajifunza kutokana na tukio hili kuhusu sala?

  • Mpangie kila mtoto asome moja ya vifungu vya maneno vifuatavyo, na wasaidie kutafuta swali au tatizo kaka wa Yaredi alilokuwa nalo: Etheri 1:33–35; Etheri 1:36–37; na Etheri 2:18–20. Kaka wa Yaredi alifanya nini kuhusu matatizo au maswali haya? Ni kwa jinsi gani Bwana alimsaidia katika kila moja? Waalike watoto kufikiria kuhusu matatizo ambayo kwayo wanahitaji usaidizi. Ni kwa jinsi gani wanaweza kufuata mfano wa kaka wa Yaredi kupata suluhisho la matatizo yao? Shiriki uzoefu ambapo uliomba kwa ajili ya usaidizi na Bwana akakusaidia.

Etheri 3:4-17

Niliumbwa kwa mfano wa Mungu.

Watoto unaowafundisha watakutana na jumbe nyingi za uongo kuhusu Mungu, wao wenyewe, na miili yao. Mistari hii ni fursa ya kufundisha kweli za milele kuhusu mada hizi.

Shughuli za Yakini

  • Soma pamoja na watoto Etheri 3: 6–16, na wasaidie kutengeneza orodha ya mambo kaka wa Yaredi aliyojifunza kuhusu Bwana kutokana na uzoefu wake. Kwa nini ni muhimu kujua kuhusu mambo haya? Kwa mfano, ni kwa jinsi gani inaathiri jinsi tunavyoichukulia miili yetu kwa kujua kwamba tumeumbwa kwa mfano wa Bwana?

  • Andika mwili wa nyama na mwili wa kiroho ubaoni. Waalike watoto kushiriki sifa za mwili wa nyama (tuna ngozi, damu, na kadhalika), na andika majibu yao ubaoni. Someni Etheri 3:4–17 kwa pamoja, na waalike watoto kutafuta kile wanachojifunza kuhusu miili yetu ya nyama. Shuhudia kwamba miili yetu na roho zetu “viliumbwa kwa jinsi ya kama maumbile ya [Yesu]” (Ether 3:15)

Etheri 5:2–4

Mashahidi watatu wanashuhudia juu ya Kitabu cha Mormoni.

Moroni alitoa unabii kwamba Mashahidi Watatu wangesaidia kudhihirisha ukweli wa Kitabu cha Mormoni. Unaweza kutumia unabii huu kuimarisha shuhuda za watoto na kuwapa msukumo kuwa mashahidi wa Kitabu cha Mormoni katika njia zao wenyewe.

Shughuli za Yakini

  • Andika ubaoni baadhi ya maneno muhimu kutoka Etheri 5:2–4, kama vile bamba, nguvu, kweli, mashahidi,, na ushuhuda. Soma mistari hii pamoja na watoto, na waalike kusimama unapofikia moja ya maneno yaliyoko ubaoni na zungumza kuhusu kwa nini maneno haya ni muhimu. Ili kuwafundisha watoto kuhusu Mashahidi Watatu, ungeweza kurejea kwenye “Mlango wa 7: Mashahidi Wanaziona Bamba za Dhahabu” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 31–33) na “Ushuhuda wa Mashahidi Watatu” katika Kitabu cha Mormoni. Kwa nini Mungu alitaka watu watatu kuziona bamba za dhahabu?

  • Waambie watoto jinsi unavyojua Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Waalike watoto kushiriki kwa nini wanajua ni cha kweli. Wasaidie kufikiria njia ambazo wanaweza kuwa mashahidi wa Kitabu cha Mormoni, na wahimize kushiriki ushahidi wao na mtu fulani wiki hii.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kufikiria jambo wanaloweza kuliombea usaidizi wa Baba wa Mbinguni, kama kaka wa Yaredi alivyofanya. Wahimize kutafuta usaidizi Wake kupitia sala.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fundisha wakati wa shughuli. Wakati watoto wanapofanya shughuli kama vile kuchora au kufanyia kazi ukurasa wa shughuli, unaweza kutumia muda kusisitiza kweli zilizofundishwa kote kwenye shughuli hizo.