Njoo, Unifuate
Novemba 9–15. Etheri 1–5: “Pasua Lile Pazia la Kutoamini”


“Novemba 9–15. Etheri 1–5: ‘Pasua Lile Pazia la Kutoamini,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Novemba 9–15. Etheri 1–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
Wayaredi wakisafiri nyikani

Wayaredi Wakiondoka Kutoka Babeli, na Albin Veselka

Novemba 9–15

Etheri 1–5

“Pasua Lile Pazia la Kutoamini”

Kitabu cha Etheri ni kumbukumbu ya Wayaredi, waliowasili katika nchi ya ahadi karne nyingi kabla ya Wanefi. Mungu alimtia msukumo Moroni aweze kuweka pamoja kumbukumbu ya Etheri na Kitabu cha Mormoni kwa sababu ya uhusiano wake na siku yetu. Jinsi gani unahisi ni muhimu katika maisha yako?

Andika Misukumo Yako

Wakati ni kweli kwamba njia za Mungu ni za juu kuliko zetu, na daima tunapashwa tukubali mapenzi Yake, pia Anatutia moyo tuweze kufikiria na kutenda kwa ajili yetu wenyewe. Hilo ni somo moja ambalo Yaredi na kaka yake walijifunza. Kwa mfano, dhana ya kusafiri kwenda katika nchi mpya iliyokuwa “chaguo juu ya zote duniani ” ilionekana kuanzia akilini mwa Yaredi, na Bwana “akawa na huruma” na akaahidi kukubali ombi lake, akisema “Na hii nitakufanyia kwa sababu ya muda huu mrefu ambao umeomba kwangu” (ona Etheri 1:38–43). Na wakati kaka wa Yaredi aligundua jinsi kulivyokuwa na giza ndani ya mashua ambazo zingewabeba hadi nchi yao ya ahadi, Bwana alimualika apendekeze suluhu, akiuliza swali ambalo sisi kwa kawaida humuuliza Yeye: “Ungetaka nifanye nini?” (Etheri 2:23). Ujumbe unaonekana kuwa kwamba hatufai kutarajia kwamba Mungu atatuamuru katika mambo yote. Tunaweza kushiriki naye mawazo yetu na dhana zetu, na Atasikiliza na kutupatia idhinisho au kutushauri vinginevyo. Wakati mwingine kitu ambacho kinatutenganisha na baraka tunazotafuta ni “pazia letu la kutoamini,” na kama tunaweza “kupasua lile pazia” (Etheri 4:15), tunaweza kushangazwa na kile ambacho Bwana yuko tayari kutufanyia.

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Etheri 1:33–43

Ninapomlilia Bwana, atakuwa na huruma kwangu.

Etheri 1:33–43 inasimulia sala tatu za kaka yake Yaredi. Je, unajifunza nini kutoka kwenye majibu ya Bwana kwa kila moja ya sala hizi? Fikiria kuhusu wakati ambapo ulihisi huruma ya Bwana wakati ulipomlilia kwa sala. Unawaweza kutaka kuandika zoezi hili na kulishiriki na mtu ambaye anaweza kuhitaji kusikia ushuhuda wako.

Etheri 2; 3:1–6; 4:7–15

Naweza kupokea ufunuo kwa ajili ya maisha yangu.

Rais Russell M. Nelson alisema: “Ninawasihi muongeze uwezo wenu wa kiroho wa kupokea ufunuo. … Chagua kufanya kazi ya kiroho inayotakiwa ili kufurahia karama ya Roho Mtakatifu na kuisikia sauti ya Roho mara kwa mara zaidi na kwa uwazi zaidi” (“Ufunuo kwa ajili ya Knisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 96).

Unapojifunza Etheri 2; 3:1–6; na 4:7–15, ni kweli zipi unazopata zinakusaidia kuelewa jinsi ya kutafuta ufunuo binafsi? Unaweza kuweka alama kwa rangi moja maswali au wasiwasi kaka ya Yaredi aliokuwa nao na kile alichofanya kuvihusu, na ukitumia rangi nyingine unaweza kuweka alama jinsi Bwana alivyomsaidia na kusababisha mapenzi Yake yajulikane. Ni nini kinakuvutia kuhusu jinsi kaka ya Yaredi alivyozungumza na Bwana, na unajifunza nini kutokana na hili kuhusu jinsi ya kuongeza mtiririko wa ufunuo katika maisha yako?

Etheri 2:16–25

Bwana atanitayarisha niweze kuvuka “bahari yangu kuu”.

Ili kufikia nchi ya ahadi, Wayaredi walikumbana na vizuizi vikubwa: kuvuka “bahari kuu” (Etheri 2:25). Kirai “bahari kuu” chaweza kuwa njia bora ya kuelezea kile majaribu na changamoto zetu wakati mwingine zinavyo hisiwa . Na wakati mwingine, kama ilivyokuwa hali ya Wayaredi, kuvuka “bahari [yetu] kuu” ni njia pekee ya kutimiza mapenzi ya Mungu kwa ajili yetu. Unaona mifanano kwenye maisha yako katika Etheri 2:16–25? Je, ni jinsi gani Bwana amekutayarisha kwa ajili ya changamoto zako? Anaweza kuwa anakutaka ufanye hivi sasa kujitayarisha kwa kile anachokuhitahi kufanya hapo baadae?

Etheri 3

Nimeumbwa kwa mfano wa Mungu.

Juu ya Mlima Shelemu, kaka wa Yaredi alijifunza mengi kuhusu Mungu na kuhusu yeye mwenyewe? Unajifunza nini kutoka Etheri 3 kuhusu asili ya kimwili na kiroho ya Mungu? Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinakusaidia kuelewa utambulisho na uwezo wako wa kiungu?

Picha
mwanamke na watoto wawili wakicheza ufukweni

Sisi sote tu watoto wa Mungu.

Etheri 3:6–16

Je, kaka wa Yaredi alikuwa mtu wa kwanza kumuona Bwana?

Mungu alikuwa Amejionyesha kwa manabii wengine kabla ya kaka wa Yaredi (kwa mfano, ona Musa 7:4, 59), kwa hivyo ni kwa nini Bwana alimwambia, “Kamwe sijajionyesha kwa binadamu”? (Etheri 3:15). Mzee Jeffrey R. Holland alijaribu kutoa uwezekano huu wa maelezo : “Kristo alikuwa akisema kwa kaka wa Yaredi, ‘Kamwe sijajionyesha kwa binadamu katika njia hii, bila ya hiari yangu, iliyosababishwa pekee na imani ya anayeona’” (Kristo Agano Jipya [1997], 23).

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

Etheri 1:34–37

Tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu kusali kwa ajili ya wengine? Ni kweli gani zingine kuhusu sala mistari hii inaonesha?

Etheri 2:16–3:6

Je, mfano wa kaka wa Yaredi unatufundisha nini kuhusu jinsi ya kutafuta majibu kwa shida na maswali yetu? Pengine wanafamilia wanawesa kushiriki uzoefu wakati walipotafuta na kupokea majibu kutoka kwa Bwana.

Etheri 4:11–12

Baada ya kusoma mistari hii, wanafamilia wanaweza kuandika vitu vya kila siku ambavyo vinaathiri familia yako (kama vile sinema, nyimbo, michezo, au watu) kwenye vipande vya karatasi na uviweke ndani ya bakuli. Kisha wanaweza kuchukua kwa zamu na kujadiliana ikiwa “huwashawishi [wao] kutenda mema” (Etheri 4:12). Ni mabadiliko gani familia yako inahisi kutiwa msukumo kufanya?

Etheri 5

Unaweza kuficha kitu au chakula kitamu ndani ya sanduku na umwalike mwanafamilia aangalie ndani na awapatie wanafamilia wengine vidokezo ili kuwasaidia kukisia kilicho ndani. Mnaposoma Etheri 5 pamoja, jadilianeni kwa nini ni muhimu kwamba Bwana huwatumia mashahidi katika kazi Yake. Je, tunawezaje kushiriki ushuhuda wetu juu ya Kitabu cha Mormoni na wengine?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa tayari daima. “Nafasi za kufundisha zisizo rasmi hupita haraka, kwa hiyo ni muhimu kuzitumia vyema wakati zinapotokea. … Kwa mfano, kijana anayekabiliwa na uamuzi mgumu wa kufanya anaweza kuwa tayari kujifunza jinsi ya kupokea ufunuo binafsi” (Kufundisha Katika Njia ya Mwokozi, 16).

Picha
Yesu akigusa mawe kumi na sita katika uwepo wa kaka wa Yaredi.

Je, Uliona Zaidi ya Hii? na Marcus Alan Vincent

Chapisha