Njoo, Unifuate
Novemba 2–8. Mormon 7–9: “Ninawazungumzia Kama Vile Mko Hapa”


“Novemba 2–8. Mormon 7–9: ‘Ninawazungumzia Kama Vile Mko Hapa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Novemba 2–8. Mormoni 7–9,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Moroni akiandika kwenye mabamba ya dhahabu

Moroni Akiandika kwenye Mabaamba ya Dhahabu, na Dale Kilborn

Novemba 2–8

Mormoni 7–9

“Ninawazungumzia Kama vile Mko hapa ”

Mormoni na Moroni walikuwa na imani kwamba kumbukumbu yao ingewatia msukumo wale ambao wanaishi katika siku za mwisho. Unaposoma Mormoni 7–9, andika mawazo yanayokujia kuhusu jinsi unavyoweza kutumia kile unachojifunza.

Andika Misukumo Yako

Mormoni na Moroni walijua jinsi ilivyohisi kuwa peke yako katika ulimwengu wenye uovu. Kwa Moroni upweke ni lazima ulikuwa mkubwa hasa baada ya baba yake kuuawa vitani na Wanefii kuangamizwa. “Na hata nimebaki peke yangu,” aliandika. “Sina marafiki wala popote pa kwenda” (Mormoni 8:3, 5). Inaweza kuwa ilionekana kuwa hakuna tumaini, lakini Moroni alipata tumaini katika ushuhuda wake juu ya Mwokozi na ufahamu wake kwamba “kusudi la milele la Bwana litaendelea” (Mormoni 8:22). Na Moroni aljua ya kwamba wajibu muhimu katika kusudi hilo la milele ungetimizwa kupitia Kitabu cha Mormoni—kumbukumbu ambayo alikuwa sasa akiikamilisha kwa bidii, kumbukumbu ambayo siku moja “ingetoa nuru kutoka gizani” na kuwaleta watu wengi “kwenye ufahamu wa Kristo” (Mormoni 8:16; 9:36). Imani ya Moroni katika ahadi hizi ilimwezesha kutangaza kwa wasomaji wa siku zijazo wa kitabu hiki, “Ninazungumza Kwenu Kama vile Mpo hapa” na “Najua kwamba mtapokea maneno yangu” (Mormoni 8:35; 9:30). Na sasa tunayo maneno yake, na kazi ya Bwana ina endelea, kwa kiasi fulani kwa sababu Mormoni na Moroni walibaki wakweli kwenye misheni yao, hata wakati walipokuwa peke yao.

ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mormoni 7

Sina budi kumwamini Yesu Kristo na “kushikilia” injili Yake.

Maneno ya mwisho ya Mormoni, yaliyoandikwa katika Mormoni 7, yameandikwa kwa ajili ya uzao wa Walamani katika siku za mwisho, lakini ndani yake kuna kweli ambazo zinatufaa sisi sote. Je, ujumbe wa Mormoni unakufundisha nini kuhusu Kristo na injili Yake? Ni kwa nini Mormoni anaweza kuwa aliuchagua ujumbe huu kuhitimisha maandishi yake?

Mormoni 7:8–10; 8:12–22; 9:31–37

Kitabu cha Mormoni ni cha thamani kubwa.

Rais Russell M. Nelson aliuliza: “Ikiwa ungepewa almasi au rubi au Kitabu cha Mormoni, ungechagua nini? Kusema kweli, kipi ni muhimu zaidi kwako?” (“Kitabu cha Mormoni: Maisha Yako Yangekuwaje Bila hicho?Ensign au Liahona, Nov. 2017, 61.

Mormoni na Moroni walijua ya kwamba maandishi waliyokuwa wakiandika yangekuwa na umuhimu mkubwa katika siku zetu, kwa hivyo walifanya dhabihu kubwa kuyatayarisha na kuyalinda. Unaposoma Mormoni 7:8–10; 8:12–22; na 9:31–37, fikiria ni kwa nini kumbukumbu hiyo ni yenye thamani kubwa katika siku zetu. Unaweza kupata umaizi wa ziada katika 1 Nefi 13:38–41; 2 Nefi 3:11–12; na Mafundisho na Maagano 33:16; 42:12–13. Ni uzoefu gani umekusaidia kujua kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha thamani kubwa?

Nakala za Kitabu cha Mormoni katika lugha tofauti

Maandishi ya manabii katika Kitabu cha Mormoni yanatumika kwetu.

Mormoni 8:26–41; 9:1–30

Kitabu cha Mormoni kiliandikwa kwa ajili yetu leo.

Yesu Kristo alimuonyesha Moroni kile ambacho kingekuwa kinatendeka wakati Kitabu cha Mormoni kingetokea (ona Mormoni 8:34–35), na kile ambacho Moroni aliona kilimsababisha kutoa maonyo makali kwa ajili ya siku zetu. Unaposoma Mormoni 8:26–41 na 9:1–30, tafakari kama kuna ishara zozote za mitazamo na vitendo hivi katika maisha yako. Ungefanya nini kitofauti?

Kwa mfano, Mormoni 9:1–30 ina ujumbe wa Moroni kwa kujibu kutokuwa na imani katika Yesu Kristo alikokuona katika siku zetu. Fikiria kuandika kile unachojifunza kutoka kwenye maneno yake kuhusu yafuatayo:

Je, ni nini unachojifunza kutoka kwa Moroni ambacho kinaweza kukusaidia kuwaleta wengine karibu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

Mormoni 7:5–7, 10; 9:11–14

Ni nini mistari hii inatufundisha kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni na kwa nini tunamhitaji Mwokozi?

Mormoni 7:8–10

Tumejifunza nini katika kujifunza kwetu Kitabu cha Mormoni mwaka huu ambacho kimesaidia kuimarisha imani yetu katika Biblia? Ili kuanza mjadala, mnaweza kusoma pamoja maandiko kidogo kutoka katika Kitabu cha Mormoni na Biblia ambayo yanafundisha kweli sawa na hizo, kama vile Alma 7:11–13 na Isaya 53:3–5 au 3 Nefi 15:16–24 na Yohana 10:16.

Mormoni 8:1–9

Je, ingeleta hisia gani kuwa peke yako jinsi Moroni alivyokuwa? Nini kinachotuvutia sisi kuhusu kazi aliyoitekeleza?

Mormoni 8:12, 17–21; 9:31

Fikirieni kusoma mistari hii kama familia na kisha kusoma kauli ifuatayo kutoka kwa Mzee Jeffrey R. Holland: “Isipokuwa kwa Mwanawe wa Pekee mkamilifu, watu wasio wakamilifu ndiyo tu Mungu amewahi kuwa nao katika kufanya kazi. … Unapoona upungufu, kumbuka kwamba kizuizi hakipo katika utakatifu wa kazi hii” (“Naamini,” Ensign au Liahona, Mei 2013, 94). Kwa nini ni hatari kufokasi kwenye mapungufu ya wengine, ikiwa ni pamoja na wale walioandika Kitabu cha Mormoni?

Mormoni 8:36–38

Inamaanisha nini kujichukulia jina la Yesu Kristo juu yetu? Kwa nini mtu anaweza kuona aibu kujichukulia juu yake jina la Kristo? Tunawezaje kuwa jasiri katika shuhuda zetu juu ya Mwokozi?

Mormoni 9:16–24

Viungo fulani vinahitajika kufanya jaribio la kisayansi au kiungo cha upishi kufaulu. Fikiria kufanya jaribio au kupika chakula mnachokipenda kama familia kabla ya kusoma Mormoni 9:16–24. Unaposoma mistari (hasa mistari 20–21), tafuta “viungo” muhimu vinavyosababisha miujiza kufanyika. Ni miujiza gani tunaweza kuiona duniani na katika familia yetu?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Kujifunza Kibinafsi

Rejea katika nyenzo rasmi za Kanisa. Kama una maswali ya injili, vyanzo bora zaidi vya majibu ni sala, maandiko, maneno ya manabii walio hai, na machapisho mengine rasmi ya Kanisa (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 17–18, 23–24).

Mormoni akifupisha bamba za dhahabu

Mormoni Akifupisha Bamba za Dhahabu, na Jon McNaughton