Njoo, Unifuate
Novemba 23–29. Etheri 12–15: “Kwa Imani Vitu Vyote Hutimizwa”


“Novemba 23–29. Etheri 12–15: ‘Kwa Imani Vitu Vyote Hutimizwa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Novemba 23–29. Etheri 12–15,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
Etheri akiingia pangoni

Etheri Akijificha kwenye Pango la Mwamba, na Gary Ernest Smith

Novemba 23–29

Etheri 12–15

“Kwa Imani Vitu Vyote Hutimizwa”

Kuandika mawazo kunaweza kualika ufunuo zaidi na kuimarisha ushuhuda wako. Pia inakusaidia kukumbuka misukumo yako na kuishiriki pamoja na wengine katika siku za baadaye.

Andika Misukumo Yako

Unabii wa Etheri kwa Wayaredi ulikuwa “mkubwa na wa ajabu” (Etheri 12:5). Aliwaambia juu ya vitu vyote, kutokea mwanzo wa binadamu” (Etheri 13:2). Aliona mbele “siku za Kristo” na Yerusalemu Mpya ya siku za mwisho (Etheri 13:4). Na alizungumzia juu ya “tumaini kwa ajili ya ulimwengu bora, ndio, hata mahali katika mkono wa kuume wa Mungu” (Etheri 12:4). Lakini Wayaredi waliyakataa maneno yake, kwa sababu sawa na zile watu mara nyingi hukataa unabii wa watumishi wa Mungu—“kwa sababu [hawauoni]” (Etheri 12:5). Inahitaji imani kuamini ahadi au maonyo kuhusu vitu ambavyo hatuwezi kuviona, kama vile ilivyochukuwa imani kwa Etheri kutabiri juu ya “vitu vikubwa na vya ajabu” kwa watu wasio amini. Ilihitaji imani kutoka kwa Moroni kuamini kwamba Mungu angeweza kuchukua “unyonge wake katika maandishi” na kuugeuza kuwa nguvu (ona Etheri 12:23–27). Ni aina hii ya imani ambayo inatufanya “kuwa na uhakika na thabiti, siku zote tukizidi sana katika kutenda kazi njema, tukiongozwa kumtukuza Mungu” (Etheri 12:4). Na ni aina hii ya imani ambayo kupitia kwayo “vitu vyote hutimizwa” (Etheri 12:3).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Etheri 12

Imani katika Yesu Kristo inaweza kusababisha miujiza mikuu.

Watu wengi leo, kama Wayaredi katika siku za Etheri, wanataka kuona ushahidi kabla hawajaamini katika Mungu na uwezo Wake. Hata hivyo, Moroni alifundisha kwamba “Imani ni vitu ambavyo vinatumainiwa na havionekani” na kwamba “hampati ushahidi wowote mpaka baada ya majaribu ya imani yenu” (Etheri 12:6).

Weka alama kila wakati unapopata neno “imani” katika Etheri 12, na uandike kile unachojifunza kuhusu imani. Tafuta majibu kwa maswali kama haya: Imani ni nini? Nini matunda ya maisha yaliyojazwa imani? Unaweza pia kuandika mawazo yako kuhusu ushahidi ulioupata “baada ya majaribu ya imani yako” (Etheri 12:6).

Ona Pia Waebrania 11; Alma 32.

Etheri 12:1–9, 28, 32

Yesu Kristo anatupa “tumaini lenye ubora zaidi .”

Pamoja na umaizi mkubwa kuhusu imani, Etheri 12 pia ina mengi ya kusema kuhusu tumaini—pengine unaweza kuweka alama kila wakati neno “tumaini” linapotokea. Tumaini inamaanisha nini kwako? Ni sababu zipi Etheri alikuwa nazo za “kutumaini ulimwengu bora”? (ona Etheri 12:2–5). Ni jinsi gani injili ya Yesu Kristo imetupa “tumaini lenye ubora zaidi.”? (Etheri 12:32).

Ona pia Moroni 7:40–41; Dieter F. Uchtdorf, “Nguvu ya Tumaini Bila Kikomo,” Ensign au Liahona, Nov. 2008, 21–24; Hubiri Injili Yangu, 117.

Etheri 12:23–29

Yesu Kristo anaweza kuvifanya vitu dhaifu kuwa na nguvu.

Wakati tunaposoma maandiko yenye nguvu ya Moroni , ni rahisi kusahau ya kwamba alikuwa na wasiwasi kuhusu “unyonge wake katika maandishi na aliogopa kwamba watu wangedhihaki maneno yake (ona Etheri 12:23–25). Lakini Mungu aliahidi kwamba “angefanya vitu dhaifu kuwa vyenye nguvu” kwa ajili ya wanyenyekevu (mstari wa 27), na nguvu ya kiroho katika maandishi ya Moroni ni ushahidi wa kuaminika kwamba Bwana alitimiza ahadi Yake.

Baada ya kusoma Etheri 12:23–29, tafakari nyakati ambazo Mungu amekusaidia kutambua udhaifu wako na kukufanya uwe na nguvu licha ya udhaifu huo. Huu unaweza pia kuwa muda mzuri wa kufikiria kuhusu udhaifu ambao unapambana nao kwa sasa. Unahisi unahitaji kufanya nini ili kujinyenyekeza mbele za Bwana na kuonyesha imani Kwake ili uweze kupokea ahadi Yake ya “kufanya vitu dhaifu kuwa vya nguvu”? (Etheri 12:27).

Unapotafakari mistari hii, umaizi ufuatao kutoka kwa Mzee Neal A. Maxwell unaweza kuwa wenye msaada: “Wakati tunaposoma katika maandiko juu ya ‘udhaifu’ wa mtu, hili neno linajumuisha … udhaifu wa asili katika hali ya kawaida ya mwandamu ambayo mwili una matokeo ya mfululizo juu ya roho (ona Etheri 12:28–29). Udhaifu pia unajumuisha, hata hivyo, udhaifu wa kibinafsi, ambao tunatarajiwa kuushinda (ona Mafundisho na Maagano 66:3; Yakobo 4:7)” (Bwana, Tuongezee Imani [1994], 84).

Ona Pia “Neema,” Mada za Injili, topics.ChurchofJesusChrist.org.

Etheri 13:13–22; 14–15

Kuwakataa manabii huleta hatari za kiroho.

Kuwa mfalme wa Wayaredi ilikuwa, kihistoria, wadhifa hatari. Hii ilikuwa kweli hasa kwa Koriantumuri, kwa maana, “watu wenye nguvu … walitafuta kumwangamiza” (Etheri 13:15–16). Katika Etheri 13:15–22, tambua kile ambacho Koriantumuri alifanya ili kujilinda na kile ambacho nabii Etheri alimshauri afanye badala Yake. Unaposoma sehemu iliyosalia ya kitabu cha Etheri, tafakari matokeo ya kutowaamini manabii. Nini hutokea kwa watu wakati “Roho ya Bwana [anapokoma] kushindana nao”? (Etheri 15:19).

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

Etheri 12:7–22

Mnaposoma mistari hii pamoja, mnaweza kufanya mapitio ya mifano ya kutia msukumo kuhusu imani ambayo mmesoma juu yake katika Kitabu cha Mormoni. Hii inaweza kupeleka kwenye mjadala kuhusu mifano ya imani katika historia ya familia yako au maisha yenu wenyewe—fikiria kuandika uzoefu huu ikiwa bado hujafanya hivyo.

Etheri 12:27

Kwa nini Bwana anatupatia udhaifu? Nini wajibu wetu katika “kuvifanya vitu dhaifu kuwa vyenye nguvu? Nini wajibu wa Mwokozi?

Etheri 12:41

Je, kuna njia ya kufurahisha unayoweza kutumia kuwafundisha watoto “kumtafuta … Yesu”? Njia moja inaweza kuwa kuficha picha ya Yesu na kuwaalika wanafamilia ‘kuitafuta” na kuipata picha hiyo. Ni kwa jinsi gani tunamtafuta Yesu, na jinsi gani tunabarikiwa tunapompata?

Etheri 13:13–14; 15:19, 33–34

Inaweza kuwa ya kupendeza wanafamilia wako kulinganisha uzoefu wa Etheri na uzoefu wa Mormoni na Moroni (ona Mormoni 6; 8:1–10). Zinafanana vipi? Ni kwa namna gani njia ya kuelekea maangamizo ya Wanefi ilifanana na ile ya Wayaredi? (linganisha Etheri 15:19 na Moroni 8:28). Ni kweli zipi tunaweza kujifunza ambazo zitatusaidia kuepuka kile kilichowatokea?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza maswali. Watoto kawaida ni wenye kutaka kujua. Wakati mwingine unaweza kuona maswali yao kama kikwazo kutokana na kile unachojaribu kufundisha. Badala yake, ona maswali kama fursa. Yanaashiria kwamba watoto wako tayari kujifunza—yanakupatia umaizi juu ya wasiwasi wa na jinsi wanavyohisi kuhusu kile wanachojifunza (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25–26).

Picha
Etheri akiwa amepiga magoti katika mlango wa pango

Wa ajabu Ulikuwa Unabii wa Etheri, na Walter Rane

Chapisha