Njoo, Unifuate
Novemba 16–22. Etheri 6–11: “Kwamba Uovu Utupiliwe Mbali”


“Novemba 16–22. Etheri 6–11: ‘Kwamba Uovu Utupiliwe Mbali,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Novemba 16–22. Etheri 6–11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Mashua za Wayaredi ndani ya bahari

Nitawarudisha juu Tena kutoka kwenye Kilindi, na Jonathan Arthur Clarke

Novemba 16–22

Etheri 6–11

“Kwamba Uovu Utupiliwe Mbali”

Mawazo yaliyoko katika muhtasari huu siyo maelekezo unayolazimika kuyafuata. Yamekusudiwa kuchochea ubunifu wako na kualika uvuvio.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Tumia picha kutoka muhtasari wa wiki hii na muhtasari wa wiki iliyopita katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia kuwasaidia watoto kurejea kile walichojifunza kuhusu Wayaredi kuvuka bahari. Waache wafanye zamu kushiriki kile wanachojua.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Etheri 6:2–12

Baba wa Mbinguni anaweza kunifariji wakati ninapokuwa na woga.

Yawezekana ilikuwa ya kutia hofu kwa Wayaredi “kutupwa juu ya mawimbi ya bahari mbele ya upepo” (Etheri 6:5). Lakini Bwana aliwaweka salama na aliwasaidia. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kumgeukia Bwana wakati wanapohisi kuogopa?

Shughuli za Yakini

  • Kwa kutumia maneno na vifungu vya maneno kutoka Etheri 6:2–12, waelezee watoto safari ya Wayaredi kuvuka bahari. Waalike watoto wajifanye kwamba wanaingia ndani ya mashua na wajifanye kwamba mashua yao imesukumwa na kufunikwa na mawimbi. Ni kwa jinsi gani ungehisi kuwa ndani ya mashua halisi iliyo ndani ya dhoruba? Tunaweza kufanya nini tunapohisi hofu? Someni pamoja mstari wa 7 na 9 kuona kile Wayaredi walichofanya wakati walipokuwa na hofu.

  • Simulia kuhusu wakati ambapo ulikuwa na hofu na Baba wa Mbinguni akakufariji. Shiriki pamoja na watoto wimbo wa Kanisa au wimbo unaokusaidia “kumshukuru na kumsifu Bwana” (Etheri 6:9) kwa usaidizi Wake. Waache watoto washiriki nyimbo za msingi wanazozipenda, na imbeni baadhi ya nyimbo hizo pamoja.

  • Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kutengeneza mashua za karatasi. Elezea kwamba mashua ziliwasaidia Wayaredi kuwa salama hata wakati walipozungukwa na maji (ona Etheri 6:7, 10). Ni nini ambacho Baba wa Mbinguni ametupatia kutuweka salama katika safari yetu ya kurudi Kwake?

Etheri 6:9, 12, 30; 7:27; 10:2

Naweza kuwa mwenye shukrani.

Baada ya kufika salama katika nchi ya ahadi, Wayaredi walikuwa na shukrani kwamba “machozi ya shangwe yakatiririka” (Etheri 6:12). Ni kwa jinsi gani unaweza kuhimiza roho ya shukrani kwa watoto unaowafundisha?

Shughuli za Yakini

  • Wasomee watoto vifungu vya maneno kutoka Etheri 6:9 na 12 ili kuwafundisha jinsi Wayaredi walivyoonyesha shukrani yao kwa Bwana kwa kuwasaidia kufika nchi ya ahadi. Waombe watoto wataje baadhi ya mambo waliyo na shukrani kwayo. Imbeni pamoja, kama Wayaredi walivyofanya, wimbo unaoonyesha shukrani, kama vile “I Thank Thee, Dear Father” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,7).

  • Wasomee watoto Etheri 10:2 kuonyesha kwamba hata miaka mingi baadaye, Wayaredi walikumbuka jinsi Bwana alivyowasaidia babu zao kuvuka bahari. Wasaidie watoto kufikiri juu ya jinsi ambavyo Bwana amewabariki. Kisha waruhusu watoto wachore picha ya kuwakumbusha juu ya baraka hizi (au wasaidie kuchagua kutoka kwenye picha unazoleta, pengine kutoka kwenye magazeti ya Kanisa).

Etheri 7:24–27

Ninabarikiwa pale ninapomfuata nabii.

Kitabu cha Etheri kwa uwazi kinaonyesha kwamba wakati Wayaredi walipomfuata nabii, walibarikiwa, na wakati walipowakataa manabii, maisha yao yalikuwa magumu. Fikiria juu ya jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kuona kwamba hiyo ni kweli hata kwetu.

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha ya nabii aliye hai, na waulize watoto kile wanachokijua kuhusu yeye. Nabii ana kazi gani? Elezea kwamba Wayaredi pia walikuwa na manabii, na wakati wote walipomfuata nabii, walibarikiwa na walikuwa na furaha (ona Etheri 7:24–27). Ni kwa jinsi gani tunaweza kumfuata nabii?

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu manabii, kama vile “Follow the Prophet” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11; ona pia Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 4–27, 67–87). Zungumza na watoto kuhusu vitu ambavyo manabii wametufundisha kufanya (kwa mfano, kusoma maandiko yetu kila siku, kuitakasa Sabato, au kuwatumikia wengine), na waalike kuigiza kutii ushauri huo wakati unaposema “Mfuate nabii!”

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Etheri 6:2–12

Ninaweza kumwamini Baba wa Mbinguni kuniongoza kwenye uzima wa milele.

Tukio la safari ya Wayaredi kuvuka bahari linaweza kufananishwa na safari yetu kupitia maisha ya duniani. Safari zote mara kadhaa zina hatari na zinahitaji imani kwamba Bwana atatuongoza na kutulinda.

Shughuli za Yakini

  • Someni pamoja Etheri 6: 2–2, ukipumzika mara kwa mara ili watoto waweze kuchora picha za kile wanachokisoma. Ni kwa jinsi gani safari ya Wayaredi inafanana na maisha yetu? Wasaidie watoto kutambua na kujaza maelezo ya kile sehemu tofauti za michoro yao ingeweza kuwakilisha katika maisha yetu. Kwa mfano, Wayaredi wangeweza kutuwakilisha sisi. Mashua zingeweza kuwakilisha nyumba zetu, Kanisa, au injili. Ni nini upepo, maji, mawe yenye mwanga, na nchi ya ahadi vingeweza kuwakilisha?

  • Wasaidie watoto kutafuta maneno na vifungu vya maneno katika Etheri 6:2–12 ambavyo vinaonyesha jinsi Wayaredi walivyomtumaini Mungu. Shiriki mifano ya jinsi kumtegemea Mungu kumekusaidia wakati wa nyakati ngumu katika maisha yako. Wahimize watoto kushiriki uzoefu sawa na huo ambao wamekuwa nao.

    Wayaredi wakisafiri na wanyama

    Safari ya Wayaredi kuvuka Asia, na Minerva Teichert

Etheri 6:30; 7:27; 10:2

Kukumbuka kile Bwana alichonifanyia hunipa amani.

Kitu kimoja kinachotofautisha wafalme wa Kiyaredi wenye haki na waovu ni kwamba wafalme wenye haki “walikumbuka vitu vikubwa ambavyo Bwana alikuwa amefanya” kwa ajili yao (Etheri 7:27). Unawezaje kuwapa msukumo watoto kukumbuka kile Bwana alichowafanyia?

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto wasome Etheri 6:30; 7:27; na 10:2 kibinafsi au katika makundi madogo na kutafuta jambo la kufanana ambalo liko katika mistari hii. Shiriki hisia zako kuhusu kile ambacho Bwana amekufanyia, na waalike watoto kufanya vivyo hivyo.

  • Shiriki pamoja na watoto kuhusu njia unazojaribu kukumbuka jinsi Bwana alivyokubariki wewe na familia yako. Wasaidie watoto kufikiria njia ambazo wanaweza kujikumbusha kile Bwana alichowafanyia. Mpatie kila mtoto kipande cha karatasi, na waalike kutafakari na kuandika jambo ambalo Bwana amewafanyia hivi karibuni. Pendekeza kwamba wajenge tabia ya kuandika mara kwa mara baraka wanazogundua kutoka kwa Bwana (ona “O Remember, Remember” [video, ChurchofJesusChrist.org]).)

Etheri 9:28–35; 11:5–8

Bwana ana huruma wakati ninapotubu.

Japokuwa Wayaredi mara nyingi waliwakataa manabii na kuwa waovu, Bwana daima aliwasamehe pale walipojinyenyekeza na kutubu.

Shughuli za Yakini

  • Someni pamoja Etheri 9:28–35, na wasaidie watoto kufikiria sentensi tatu au nne fupi ambazo zinatoa ufupisho wa kile kilichotokea katika mistari hii. Kisha soma Etheri 11: 5–8, na wasaidie watoto kutambua mfanano kati ya matukio haya mawili. Tunajifunza nini kutoka kwenye hadithi hizi?

  • Waombe watoto wafikirie kuhusu watu wengine katika Kitabu cha Mormoni ambao walijinyenyekeza na wakasamehewa. Tumia picha kutoka Kitabu cha Sanaa ya Injili, au Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia ili kuwasaidia kukumbuka. Toa ushuhuda wako kwamba Bwana hutusamehe wakati tunapotubu kwa dhati.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki pamoja na familia zao jambo ambalo Baba wa Mbinguni amewatendea ambalo kwalo wana shukrani.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto wawe wabunifu. “Unapowafundisha watoto, waruhusu kujenga, kuchora, kupaka rangi, kuandika, na kubuni. Vitu hivi ni zaidi ya shughuli za kufurahisha—ni muhimu katika kujifunza” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).