“Maelekezo kwa Ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni (2020) (2018)
“Maelekezo kwa Ajili ya Muda wa Kuimba,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020
Maelekezo kwa Ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti
Marais Wapendwa wa Msingi na Viongozi wa Muziki,
Nyimbo za watoto wa Msingi ni nyenzo zenye nguvu sana katika kuwasaidia watoto kujifunza kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni wa furaha na kweli za msingi za injili ya Yesu Kristo. Wakati watoto wakiimba kuhusu kanuni za injili, Roho Mtakatifu atashuhudia kweli za kanuni hizo. Maneno na muziki vitakaa katika akili na mioyo ya watoto maisha yao yote.
Tafuta msaada wa Roho unapojiandaa kufundisha injili kupitia muziki. Shiriki ushuhuda wako wa kweli mnazoziimba. Wasaidie watoto kuona jinsi muziki unavyoshabihiana na kile wanachopitia na kujifunza nyumbani na katika madarasa ya Msingi. Watoto na familia zao watabarikiwa kwa juhudi zako za dhati.
Tunawapenda na tunatoa shukrani zetu kwa huduma ya kujitolea ambayo mnatoa kuimarisha na kulinda watoto wetu wenye thamani.
Urais Mkuu wa Msingi
Maelekezo kwa ajili ya Mawasilisho Kwenye Mkutano wa Sakramenti
Chini ya uelekezi wa askofu, mawasilisho ya watoto kwenye mkutano wa sakramenti kwa kawaida hufanyika katika robo ya nne ya mwaka. Kama urais wa Msingi na kiongozi wa muziki, panga kukutana mapema katika mwaka na mshauri katika uaskofu ambaye anasimamia Msingi ili kuanza kujadili mipango ya mawasilisho. Wakati umeshamaliza mipango, pata ruhusa kutoka kwake.
Mawasilisho yanapaswa kuwaruhusu watoto kuwasilisha kile ambacho wao na familia zao wamejifunza kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni nyumbani na katika Msingi, ikijumuisha nyimbo za Msingi walizoimba katika mwaka. Kwa sala fikiria kanuni zipi za injili na nyimbo zinasaidia kile ambacho wamejifunza. Katika mwaka mzima, weka kumbukumbu ya hotuba za watoto na uzoefu binafsi kwa ajili ya matumizi wakati wa mawasilisho. Waalike watoto kushiriki maandiko, hadithi, na shuhuda zao katika mawasilisho. Wakati ukipanga mawasilisho, fikiria njia ambazo mawasilisho yanaweza kusaidia mkusanyiko kulenga kwa Mwokozi na mafundisho Yake.
Matawi yenye idadi ndogo ya watoto yanaweza kufikiria njia ambazo wanafamilia wanaweza kushiriki pamoja na watoto wao. Mshiriki wa uaskofu anaweza kuhitimisha mkutano kwa maneno mafupi.
Wakati ukiandaa mawasilisho, kumbuka mwongozo ufuatao:
-
Mazoezi yasichukue muda usio wa lazima kutoka kwenye madarasa ya Msingi au familia.
-
Vitu vya kuona, vinyago, na video za kuangalia havifai kwa ajili ya mkutano wa sakramenti
Ona Handbook 2: Administering the Church, 11.5. 4.
Maelekezo kwa Ajili ya Muda wa Kuimba
Dakika 5 (Urais wa Msingi): Sala ya kufungua, maandiko au makala ya imani, na hotuba moja
Dakika 20 (kiongozi wa muziki): Muda wa kuimba
Urais wa Msingi na kiongozi wa muziki huchagua nyimbo kwa ajili ya kila mwezi ili kuimarisha kanuni watoto wanazojifunza katika madarasa yao na nyumbani. Orodha ya nyimbo ambazo zinaimarisha kanuni hizi imejumuisha katika mwongozo huu. Nyimbo hizi pia zimependekezwa katika muhtasari kwenye Njoo, Unifuate—Kwa Ajili Ya Msingi.
Unapofundisha nyimbo kwa watoto, waalike kushiriki kile ambacho tayari wamejifunza kuhusu hadithi na kanuni za msingi zifundishwazo na nyimbo. Unaweza kutaka kurejea mihutasari ya Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi ambayo watoto wanajifunza katika madarasa yao. Hii itakusaidia kujua hadithi na kanuni ambazo wanajifunza ili kwamba uweze kufikiria jinsi ya kusaidia katika kujifunza kwao kupitia muziki.
Wakati wa kuimba, unaweza pia kurejea nyimbo ambazo watoto tayari walishajifunza hapo awali na nyimbo wanazofurahia kuziimba. Wakati ukifanya marejeo, waalike watoto kushiriki mawazo yao na hisia kuhusu kweli zipatikanazo katika nyimbo.
Kitabu cha Nyimbo za Watoto ni nyenzo ya msingi ya muziki katika Msingi. Nyimbo kutoka kitabu cha nyimbo za Kanisa na nyimbo kutoka kwenye jarida la Rafiki na Liahona pia zinafaa. Mara chache watoto wanaweza kuimba nyimbo za kizalendo au za siku kuu ambazo zinafaa kwa ajili ya Jumapili na umri wa watoto. Matumizi ya muziki wowote tofauti kwenye Msingi lazima yaidhinishwe na uaskofu (ona Handbook 2: Administering the Church, 11.2.4).
Muhtasari wa Msingi
Kila wiki, Msingi hujumuisha:
-
Muda wa kuimbaDakika 25
-
MapumzikoDakika 5
-
MadarasaDakika 20
Viongozi wa Darasa kubwa la Msingi wanaweza kuwagawa watoto katika makundi mawili na kuwa na kundi moja katika madarasa ya Msingi wakati kundi jingine likiwa katika muda wa kuimba. Kisha makundi mawili yangeweza kubadilishana nafasi. Katika hali kama hiyo, viongozi wa darasa la Msingi wanaweza kuhitaji kubadilisha muda ulioonyeshwa hapo juu ili kukidhi hali yao.
Muziki kwa ajili ya Muda wa Kuimba
Januari
-
“Book of Mormon Stories,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 118–19
-
“Keep the Commandments,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47
-
“The Iron Rod,” Nyimbo za Kanisa, na. 274
Februari
-
“Nephi’s Courage,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 120–21
-
“I Feel My Savior’s Love Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75
-
I Love to See the Temple,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95
Machi
-
“When I Am Baptized,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 103
-
“Dare to Do Right,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 158
-
“A Child’s Prayer,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13
Aprili
-
“Easter Hosanna,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 68–69
-
“When We’re Helping,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 198
-
“Love One Another,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 136–37
Mei
-
“I Will Be Valiant,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 162
-
“Help Me, Dear Father,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 99
-
“Testimony,” Nyimbo za Kanisa, na. 137
Juni
-
“We’ll Bring the World His Truth,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 172–73
-
“Follow the Prophet,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11
-
“I Want to Be a Missionary Now,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 168
Julai
-
“My Heavenly Father Loves Me,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29
-
“Faith,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96–97
-
“As I Search the Holy Scriptures,” Nyimbo za Kanisa, na. 277
Agosti
-
“Repentance,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 98
-
“The Still Small Voice,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto 106–7
-
“Follow the Prophet,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11
Septemba
-
“Samuel Tells of the Baby Jesus,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 36
-
“I’m Trying to Be Like Jesus,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79
-
“The Wise Man and the Foolish Man,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 281
Oktoba
-
“Reverently, Quietly,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 26
-
“Families Can Be Together Forever,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 188
-
“The Church of Jesus Christ,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77
Novemba
-
“Jesus Said Love Everyone,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 61
-
“Stand for the Right,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 159
-
“I Thank Thee, Dear Father,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 7
Desemba
-
“Search, Ponder, and Pray,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 109
-
“Away in a Manger,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 42–43
-
“He Sent His Son,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35
Kutumia Muziki Kufundisha Mafundisho
Muda wa kuimba umekusudiwa kuwasaidia watoto kujifunza kweli za injili. Mawazo yafuatayo yanaweza kusaidia wakati ukipanga njia za kufundisha kanuni za injili zipatikanazo katika nyimbo za kanisa na nyimbo za Msingi.
Soma maandiko yanayohusiana. Kwa nyimbo nyingi katika Kitabu cha Nyimbo za Watoto na kitabu cha nyimbo za kanisa, marejeleo kwa ajili ya maandiko yameorodheshwa. Wasaidie watoto kusoma baadhi ya sehemu hizi, na zungumza kuhusu jinsi maandiko yanavyohusiana na wimbo. Ungeweza pia kuorodhesha marejeleo ya maandiko machache ubaoni na kuwaalika watoto kuoanisha kila rejeleo kwa wimbo au mstari kutoka kwenye wimbo.
Jaza nafasi zilizo wazi. Andika mstari wa wimbo ubaoni kwa kuacha baadhi ya maneno muhimu. Kisha waombe watoto kuimba wimbo, na kusikiliza maneno ambayo yatajaza nafasi zilizoachwa wazi. Wakati wakijaza kila nafasi iliyo wazi, jadili kanuni ipi ya injili mnajifunza kutokana na maneno yanayokosekana.
Dondoo kutoka kwa Viongozi wa Kanisa. Waalike watoto kusikiliza dondoo kutoka kwa kiongozi wa Kanisa ambayo hufundisha kanuni sawa ya injili kama ile iliyoko kwenye wimbo wa Msingi. Waombe kunyanyua mikono yao wakati wanaposikia kitu ambacho huwasaidia wao kuelewa kweli ambazo wanaziimba. Waalike kushiriki kile walichosikia.
Shuhudia. Toa ushuhuda mfupi kwa watoto kuhusu kweli za injili zipatikanazo kwenye wimbo wa Msingi. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kuimba ni njia mojawapo wanayoweza kutoa ushuhuda na kumhisi Roho.
Simama kama shahidi. Waalike watoto kufanya zamu kusimama na kushiriki kile walichojifunza kutoka kwenye wimbo wanaoimba au jinsi wanavyohisi kuhusu kweli zinazofundishwa katika wimbo. Waulize wanahisi nini wakati wanapoimba wimbo, na wasidie kutambua ushawishi wa Roho Mtakatifu.
Tumia picha. Waombe watoto wakusaidie kupata au kutengeneza picha ambazo zinaendana na maneno muhimu au vifungu vya maneno katika wimbo. Waalike kushiriki ni jinsi gani picha zinahusiana na wimbo na nini wimbo unafundisha. Kwa mfano, kama unafundisha wimbo “The Iron Rod” (Nyimbo za Kanisa, na. 274), ungeweza kuweka picha kuzunguka chumba zikionyesha maneno muhimu kutoka kwenye wimbo (kama vile fimbo ya chuma, neno la Mungu, kielekezi, majaribu, na mbingu). Waombe watoto kukusanya picha na kuzinyanyua juu katika utaratibu sahihi wakati mkiimba wimbo kwa pamoja.
Shiriki somo la vitendo. Ungeweza kutumia vitendo kutia msukumo majadiliano kuhusu wimbo. Kwa mfano, wimbo “Imani” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96–97) unaongelea kuhusu mbegu ndogo. Ungeweza kuwaonyesha watoto mbegu na kuzungumza kuhusu jinsi tunavyoonyesha imani pale tunapopanda mbegu; hii ingeweza kupelekea majadiliano kuhusu njia tunazoonyesha imani katika Yesu Kristo, kama ilivyoelezewa kwenye wimbo.
Alika ushiriki wa uzoefu binafsi. Wasaidie watoto kuunganisha kanuni zilizofundishwa kwenye wimbo na uzoefu ambao wamekuwa nao wa kanuni hizo. Kwa mfano, kabla ya kuimba “I love to See the Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95), ungeweza kuwaomba watoto kunyanyua mikono yao kama wamewahi kuona hekalu. Waalike kufikiria wakati wakiimba kuhusu jinsi wanavyoweza kuhisi wanapoliona hekalu.
Uliza maswali. Kuna maswali mengi ambayo unaweza kuuliza wakati mnaimba nyimbo. Kwa mfano, unaweza kuwauliza watoto nini wanajifunza kutoka kwenye kila mstari wa wimbo. Pia unaweza kuwaomba kufikiria maswali ambayo yanajibiwa na wimbo. Hii inaweza kupelekea majadiliano kuhusu kweli zinazofundishwa katika wimbo.
Sikiliza majibu. Waombe watoto kusikiliza majibu ya maswali kama vile “nani?” “kipi?” “wapi?” “muda gani?” au “kwa nini?” Kwa mfano, katika wimbo “Nephi’s Courage” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 120–21), Wangeweza kusikiliza nani alitakiwa kuchukua bamba na wapi, wakati gani, kwa jinsi gani, na kwa nini alimtii Bwana. Pia ungeweza kuwaomba watoto kusikiliza maneno muhimu au kuhesabu katika vidole vyao ni mara ngapi wanaimba neno fulani.
Kuwasaidia Watoto Kujifunza na Kukumbuka Nyimbo za Msingi
Watoto hujifunza wimbo kwa kusikia na kuuimba tena na tena. Mara zote yaimbe maneno ya wimbo mpya kwa watoto—usiyasome tu au kuyakariri. Hii huwasaidia watoto kuunganisha sauti ya muziki na maneno. Baada ya wimbo kufundishwa, urejee katika njia tofauti za kufurahisha kwa mwaka mzima. Yafuatayo ni baadhi ya mawazo ya kuwasaidia watoto kujifunza na kurejea nyimbo.
Tengeneza mabango. Onyesha mabango yakiwa na maneno kutoka kwenye kila mstari au picha ambayo huwakilisha maneno. Wakati watoto wakiimba, funika baadhi ya maneno au picha mpaka waweze kuimba mstari mzima bila bango. Pia unaweza kuwaalika watoto kukusaidia kutengeneza mabango.
Onyesha kwa mfano mpangilio wa sauti. Ili kuwasidia watoto kujifunza sauti ya muziki wa wimbo, weka mkono wako kwa upana, na wakati ukiimba maneno, peleka mkono wako juu kuonyesha sauti ya juu na chini kuonyesha sauti ya chini.
mwangwi. Waalike watoto kuwa mwangwi wa sauti yako kwa kurudia kile unachokiimba. Imba kwa watoto kirai kifupi au mstari, kisha waache waimbe kwa kurudia.
Tumia njia tofauti tofauti. Imba nyimbo katika njia tofauti tofauti, kama vile kwa kunong’ona, kwa kutotoa maneno, kwa kupiga makofi mapigo ya muziki, kwa kubadilisha kasi ya muziki, au kuimba ukiwa umekaa au kusimama. Pia ungeweza kutengeneza mchemraba kwa karatasi na, kwenye kila upande wa mchemraba, andika njia tofauti ya kuimba. Mwalike mtoto kuzungusha mchemraba kuchagua njia gani watoto wataimba wimbo.
Imba katika makundi. Mpe kila mtu darasani kirai cha kuimba wakati amesimama, na kisha waache wabadilishane virai mpaka kila darasa au kila mtu awe amepata kuimba kila kirai.
Tumia matendo ya mikono. Waalike watoto kufikiria kuhusu matendo rahisi ya mikono kuwasaidia kukumbuka maneno na jumbe za wimbo. Kwa mfano, wakati unapoimba ubeti wa pili wa “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29), ungeweza kuwaalika watoto kuonyesha macho yao, kuigiza kama vipepeo, na kuweka katika umbo la mwimuko mikono yao nyuma ya masikio yao. Waombe kuweka mikono yao kwenye mioyo yao wakati wakiimba “Yes, I know Heavenly Father loves me.”
Wasichana wanaimba, wavulana wanaimba. Chora picha ya mvulana na picha ya msichana, na zibandike katika fimbo tofauti. Wakati ukirejea wimbo, inua mojawapo ya picha kuonyesha nani anatakiwa kuimba sehemu hiyo ya wimbo.
Kikapu cha kurushia vitu. Weka vikapu au vyombo vingine vyenye namba mbele ya darasa—vyombo vingi kulingana na idadi ya beti za wimbo fulani. Mwalike mmoja wa watoto kurusha kifuko chenye mbegu au karatasi iliyokunjwa ndani ya au karibu na chombo chenye namba. Waache watoto waziimbe beti sawa na idadi ya namba kwenye chombo.
Oanisha picha na kirai. Andika kila mstari wa wimbo kwenye kipande tofauti cha karatasi, na kisha tafuta picha ambayo inawakilisha kila mstari. Weka picha kwenye upande mmoja wa chumba na karatasi upande mwingine. Imba wimbo, na waombe watoto kuoanisha picha na maneno.
Maelezo: Marejeleo kwa ajili ya kata na uaskofu pia yanatumika kwenye matawi na urais wa matawi.