Njoo, Unifuate
Kiambatisho A: Ni Jinsi Gani Roho Ananishuhudia Kwamba Kitabu cha Mormoni Ni cha Kweli?


Kiambatisho A: Ni Jinsi Gani Roho Ananishuhudia Kwamba Kitabu cha Mormoni Ni cha Kweli? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020 (2020)

“Kiambatisho A,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Kiambatisho A

Ni Jinsi Gani Roho Ananishuhudia Kwamba Kitabu cha Mormoni Ni cha Kweli?

Unaweza kuwa umesikia kuhusu ahadi ya Moroni kwa wale wote watakaosoma Kitabu cha Mormoni: “Ikiwa mtauliza na moyo wa kweli, na kusudi halisi, mkiwa na imani katika Kristo, atawaonyesha ukweli wa [Kitabu cha Mormoni] kwenu, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu” (Moroni 10:4). Lakini ina maana gani “kujua ukweli kwa uwezo wa Roho Mtakatifu”? Unawezaje kujua wakati Roho Mtakatifu anapozungumza nawe?

Inaweza kuwa na manufaa kukumbuka kwamba Roho Mtakatifu huwasiliana nasi kupitia njia ambazo zinatofautiana na njia ambazo tumezoea kutumia kuwasiliana sisi kwa sisi. Lakini Baba yako wa Mbinguni anataka kukusaidia kujifunza kutambua Roho. Amekupatia Kitabu cha Mormoni, ambamo watumishi kadhaa waaminifu wanaelezea uzoefu wao wa sauti ya Bwana.

Kwa mfano, Nefi aliwaambia kaka zake kwamba Bwana alikuwa amezungumza nao “kwa sauti ndogo tulivu,” ingawaje si lazima kwamba ilikuwa sauti ambayo wangeweza kusikia kwa masikio yao. Kwa kweli, Nefi alisema kaka zake walikuwa “wamekufa ganzi” na hawangeweza “kuhisi maneno yake” (1 Nefi 17:45, herufi za italiki zimeongezwa). Enoshi alielezea majibu kwa sala yake kama “sauti ya Bwana” ikimjia “kwenye mawazo [yake]” (Enoshi 1:10). Fikiria maneno haya yanayoelezea sauti iliyotoka mbinguni wakati Mwokozi aliyefufuka alipotokea katika nchi ya Neema: “Na haikuwa sauti kali, wala ya makelele; walakini, … iliwatoboa mpaka kwenye roho , na ikasababisha mioyo yao kuchomeka” (3 Nefi 11:3).

Pengine umekuwa na uzoefu sawa na huu, au pengine uzoefu wako umekuwa tofauti. Roho mtakatifu huwasiliana kwa njia mbalimbali, na ufunuo unaweza kuja kwa kila mmoja wetu kwa njia tofauti. Na wakati Roho yuko katika maisha yetu, tutaona ushawishi Wake juu yetu katika njia mbalimbali. Mtume Paulo alizungumzia, “Tunda la Roho ni upendo”—hisia za “furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, na upole kiasi” miongoni mwa mengine mengi (Wagalatia 5:22–23).

Haya ni baadhi ya mafunzo mengine na mifano kutoka katika Kitabu cha Mormoni kuhusu Roho Mtakatifu. Unaposoma, unaweza ukaona kwamba Roho Mtakatifu amekuwa akizungumza nawe zaidi ya vile unavyotambua, akikushuhudia ya kwamba Kitabu cha Mormoni kwa kweli ni neno la Mungu.

Shukrani na Shangwe

Kitabu cha Mormoni kinaanza na nabii Lehi akiona ono la ajabu. Katika ono hili, alipewa kitabu na akaalikwa kukisoma. “Na ikawa alipokuwa akisoma,” maandiko yanasema, “alijazwa na Roho wa Bwana.” Uzoefu huu ulimwongoza Lehi kumsifu Mungu kwa ajili ya “nguvu, na wema, na rehema,” Zake na “nafsi yake [Lehi] ilishangilia, na moyo wake wote ulijaa furaha” (1 Nefi 1:12, 14–15).

Je, umewahi kuwa na uzoefu sawa na huo? Je, kusoma Kitabu cha Mormoni kumewahi kuujaza moyo wako na shukrani kwa ajili ya wema na rehema za Mungu? Virai katika Kitabu cha Mormoni vimewahi kusababisha nafsi yako kusherehekea? Hisia hizi ni usawishi wa Roho, akikushuhudia wewe kwamba maneno unayosoma yanatoka kwa Mungu na yanafundisha ukweli Wake.

Moyo Uliobadilika

Baada ya kuhubiri mahubiri ya kusifika kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo (ona Mosia 2–4), Mfalme Benyamini alitaka kujua kama watu wake “wameyaamini maneno ambayo alikuwa amewazungumzia.” Walijibu kwamba waliamini ujumbe wake. Kwa nini? “Kwa sababu ya Roho wa Bwana Mwenyezi, ambaye ameleta mabadiliko makuu ndani yetu, au mioyoni mwetu, kwamba hatuna tamaa ya kutenda maovu tena, lakini kutenda mema daima” (Mosia 5:1–2).

Labda umegundua kitu sawa na hicho ndani ya moyo wako wakati umekuwa ukisoma Kitabu cha Mormoni. Kwa mfano, unaweza kuwa umehisi kutiwa msukumo kuwa mtu mwema zaidi, kuepuka dhambi, au kufanya jambo jema kwa ajili ya mtu fulani. Huu ndio ushuhuda wa kiroho unaotafuta kwamba kitabu kimetoka kwa Mungu. Kama vile Mormoni alifundisha, “Kila kitu kinachokaribisha na kushawishi kufanya mema, na kumpenda Mungu, na kumtumikia, kinaongozwa na Mungu” (Moroni 7:13; ona pia 2 Nefi 33:4, 10; Alma 19:33; Etheri 4:11–12).

Akili Iliyoangazwa

Wakati Alma alitaka kuwasaidia Wazoramu “kujaribu juu ya maneno [yake]” na kujua wao wenyewe kama ushuhuda wake ulikuwa wa kweli, alilinganisha neno la Mungu na mbegu: “Sasa ikiwa mtatoa nafasi, ili mbegu ipandwe ndani ya moyo wako, tazama, ikiwa itakuwa mbegu ya kweli, au mbegu nzuri, ikiwa hamtaitupa nje kwa kutoamini kwenu, kwamba mtashindana na Roho ya Bwana, tazama, itaanza kuvimba ndani ya vifua vyenu; na wakati mtakaposikia huu mwendo wa kuvimba, mtaanza kusema ndani yenu—inawezekana kwamba hii ni mbegu mzuri, au kwamba neno ni zuri, kwani linaanza kukua ndani ya nafsi yangu; ndio, linaanza kuangaza kuelewa kwangu, ndio, linaanza kunipendeza mimi” (Alma 32:27–28).

“Unatoa nafasi” moyoni mwako kwa ajili ya maneno ya Kitabu cha Mormoni wakati unapoyapa nafasi ya ushawishi juu ya maisha yako na kuongoza chaguzi zako. Na ni kwa jinsi gani maneno haya “yanaanza kukua ndani ya nafsi [yako]” na “yanaanza kuangaza uelewa [wako]”? Unaweza kuhisi kwamba unazidi kuwa imara kiroho. Unaweza kuhisi mwenye upendo zaidi na muwazi kwa wengine. Unaweza kugundua kwamba unaelewa mambo vyema zaidi, hasa mambo ya kiroho—kama kwamba nuru inang’aa akilini mwako. Na unaweza kukubali kwamba mafundisho yanayofundishwa katika Kitabu cha Mormoni “ni ya kupendeza.” Hisia kama hizi zinaweza kukusaidia kuelewa ya kwamba kwa kweli umepokea ushuhuda wa kiroho wa ukweli, jinsi Alma alivyotangaza: “Ee basi, si hii ni kweli? Nawaambia, Ndio, kwa sababu ni nuru; na chochote ambacho ni nuru, ni kizuri, kwa sababu kinaonekana, kwa hivyo lazima mjue kwamba ni nzuri” (Alma 32:35).

Hauna Haja ya Kustaajabu

Hizi ni baadhi tu ya njia ambazo kupitia kwazo, Roho huwasiliana. Kuna zingine nyingi. Endelea kutafuta fursa za kusikiliza sauti ya Roho, na utapata ushuhuda Wake unaoendelea unaothibitisha ukweli wa Kitabu cha Mormoni.

Rais Russell M. Nelson ameahidi: “Hupaswi kushangaa kuhusu nini ni kweli. Hupaswi kujiuliza nani unaweza kumwamini kiusalama. Kupitia ufunuo binafsi, unaweza kupokea ushahidi wako mwenyewe kwamba Kitabu cha Mormoni ni neno la Mungu, kwamba Joseph Smith ni nabii, na kwamba hili ni Kanisa la Bwana. Bila kujali nini wengine wanaweza kusema au kufanya, hakuna hata mmoja anayeweza kamwe kuutoa ushahidi iliobebwa kwenye moyo na akili yako kuhusu nini ni kweli.” (“Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 95).

Chapisha