“Kiambatisho B: ‘Ukweli ulio Wazi na Wenye Thamani’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Kiambatisho B,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020
Kiambatisho B
“Ukweli ulio Wazi na Wenye Thamani”
Kitabu cha Mormoni kiliandaliwa ili kije katika siku za mwisho, wakati wa kuchanganyikiwa sana kuhusu mafundisho, au ukweli wa milele wa Mungu. Sehemu ya dhamira takatifu ya kitabu hicho ni, kama alivyotabiri Nefi, ni “kuthibitisha ukweli wa [Biblia],” “kufahamisha vitu vilivyo wazi na vyenye thamani” vilivyopotea kwa kipindi cha karne nyingi, na “kufahamisha makabila yote, lugha zote, na watu wote, kwamba Mwanakondoo wa Mungu ndiye Mwana wa Baba wa Milele, na Mwokozi wa ulimwengu”(1 Nefi 13:40).
Kitabu cha Mormoni kinafunua kweli za milele ambazo zilikuwa zimepotea wakati wa Ukengeufu na kuongeza ushahidi wa pili, unaoelezea wazi kweli nyingi zinazofundishwa katika Biblia. Hizi ni baadhi tu ya kweli hizo. Zitafute hizi na kweli zingine zilizo wazi na zenye thamani unaposoma Kitabu cha Mormoni.
Uungu
-
Baba wa Mbinguni, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu wote ni viumbe tofauti lakini wameungana kwa lengo moja (ona 3 Nefi 11:32, 36).
-
Mwokozi aliyefufuka ana mwili wa kushikika (ona 3 Nefi 11:10–17).
Maandiko ya ziada kuhusu Uungu: 2 Nefi 31:6–8; Etheri 12:41
Upatanisho wa Yesu Kristo.
-
Yesu Kristo aliteseka kwa ajili ya dhambi na huzuni zetu ili aweze kujua jinsi ya kutusaidia (ona Alma 7:11–13).
-
Tunaweza kukamilishwa kupitia neema ya Yesu Kristo (ona Moroni 10:32–33).
Maandiko ya ziada kuhusu Upatanisho wa Mwokozi: 1 Nefi 10:6; 2 Nefi 2:6–9; Yakobo 4:11–12; Mosia 3:1–19; Alma 34:8–16
Mpango wa Wokovu
-
Kuanguka kwa Adamu na Hawa kulikuwa sehemu muhimu katika mpango wa Baba wa Mbinguni (ona 2 Nefi 2:22–27).
-
Upinzani ulihitajika kwetu sisi ili tuweze kuwa na haki ya kujiamulia (ona 2 Nefi 2:11–16).
-
Sisi tutahukumiwa kulingana na kazi zetu na nia za mioyo yetu (ona Alma 41:3–7).
-
“Ziwa la moto na kiberiti” ni ishara ya mateso ya wasiotubu (ona 2 Nefi 9:16–19; Mosia 3:24–27).
Maandiko ya ziada kuhusu mpango wa wokovu: 2 Nefi 9:11–26; Alma 22:12–14; 34:31–35; 42:1–26
Ukengeufu na Urejesho
-
Ukengeufu Mkuu ulitokea kwa sababu ya uovu na kutoamini (ona Mormoni 8:28, 31–41).
-
Kitabu cha Mormoni kinaimarisha kweli zinazofundishwa katika Biblia (ona 1 Nefi 13:19–41; 2 Nefi 3:12).
-
Kanisa la Kristo linastahili kuitwa kwa Jina Lake (ona 3 Nefi 27:3–9).
Maandiko ya ziada kuhusu Ukengeufu: 1 Nefi 13:1–9, 24–29; 2 Nefi 27–28
Maandiko ya ziada kuhusu Urejesho: 1 Nefi 14:7–12; 22:7–11; 2 Nefi 3:7–24; 25:17–18
Manabii na Ufunuo
-
Manabii wote hushuhudia kuhusu Yesu Kristo (ona Mosia 13:33–35).
-
Ufahamu wa ukweli wa kiroho unakuja kupitia kwa Roho Mtakatifu (ona Alma 5:45–47).
-
Biblia haijumuishi maneno yote ya Mungu (ona 2 Nefi 29:10–13).
-
Ufunuo kutoka kwa Mungu haujakoma katika wakati wetu (ona Mormoni9:7–9).
Maandiko ya ziada kuhusu manabii: 1 Nefi 22:1–2; Mosia 8:16–18; Helamani 13:24–33
Maandiko ya ziada kuhusu ufunuo: Yakobo 4:8; Alma 12:9–11; 17:2–3; Moroni 10:5
Ukuhani
-
Wenye Ukuhani waliitwa na kutayarishwa tangu msingi wa dunia (ona Alma 13:1–3).
-
Ni lazima mtu apokee mamlaka kutoka kwa Mungu ili aweze kuhubiri injili (ona Mosia 23:17).
Maandiko ya ziada kuhusu ukuhani: Mosia 18:17–20; Alma 13; Helamani 10:7
Ibada na Maagano
-
Ubatizo ni muhimu katika kupokea uzima wa milele (ona 2 Nefi 31:4–13, 17–18).
-
Ubatizo lazima ufanyike kwa kuzamishwa ndani ya maji (ona 3 Nefi 11:23–27).
-
Watoto wadogo hawahitaji kubatizwa (ona Moroni 8:8–12).
-
Ibada lazima zifanyike kulingana na amri za Kristo kupitia mtu mwenye mamlaka halali (ona Mosia 18:17–18; 3 Nefi 11:21–27; Moroni 4:1).
Maandiko ya ziada kuhusu ibada: Mosia 18:8–17; 21:33–35; Alma 13:16; 3 Nefi 18:1–11; Moroni 2–6; 8:4–26
Maandiko ya ziada kuhusu maagano: 2 Nefi 11:5; Mosia 5:1–9; Alma 24:17–18
Ndoa na Familia
-
Waume na wake wanapaswa kupendana na kuwa waaminifu kwa kila mmoja (ona Yakobo 3:5–7).
-
Wazazi wanapaswa kuwalea watoto wao katika Bwana (ona 1 Nefi 7:1).
Maandiko ya ziada kuhusu ndoa na familia: 1 Nefi 1:1; 2 Nefi 25:26; Yakobo 2:23–28; Enoshi 1:1; Mosia 4:14–15; 3 Nefi 18:21
Amri
-
Bwana atatutayarishia njia tuweze kutimiza amri Zake (ona 1 Nefi 3:7).
-
Mungu anaahidi kutubariki kama tutatii amri Zake (ona Mosia 2:22–24).
Maandiko ya ziada kuhusu amri: 1 Nefi 17:3; 22:30–31; Alma 37:13, 35; 50:20