Njoo, Unifuate
Desemba 7–13. Moroni 7–9: “Kristo Akuinue Juu”


“Desemba 7–13. Moroni 7–9: ‘Kristo Akuinue Juu”,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Desemba 7–13. Moroni 7–9,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
Moroni akiandika kwenye bamba za dhahabu

Minerva Teichert (1888–1976), Moroni: Mnefi wa Mwisho, 1949–1951, mafuta kwenye bamba la nyuzi, inchi 34¾ x 47. Jumba la Makumbusho la Chuo Kikuu cha sanaa cha Brigham Young, 1969

Desemba 7–13

Moroni 7–9

“Kristo Akuinue Juu”

Unapojifunza Moroni 7–9, sikiliza ushawishi wa Roho Mtakatifu, na uandike jumbe Zake kwako. Anaweza akakufundisha vyote viwili unachohitaji kujua na unachohitaji kufanya.

Andika Misukumo Yako

Kabla ya Moroni kuhitimisha kumbukumbu tunayoijua leo kama Kitabu cha Mormoni kwa maneno yake mwenyewe, alishiriki jumbe tatu kutoka kwa baba yake, Mormoni: waraka kwa “wafuasi wa imani ya Kristo” (Moroni 7:3) na nyaraka mbili ambazo Mormoni alikuwa amemuadikia Moroni. Pengine Moroni alizijumuisha jumbe hizi katika Kitabu cha Mormoni kwa sababu aliona kabla mifanano baina ya hatari za siku zake na zetu. Wakati maneno haya yalipoandikwa, Wanefi kwa ujumla walikuwa wakianguka ghafla na kwa haraka katika ukengeufu. Wengi wao walikuwa “wamepoteza mapenzi yao, mmoja kwa mwingine” na walifurahia “kila kitu isipokuwa kile ambacho ni kizuri” (Moroni 9:5, 19). Na ilhali Mormoni bado alipata sababu ya kuwa na tumaini—kutufundisha kwamba tumaini haimaanishi kupuuza au kuwa mshamba kuhusu shida za dunia; ina maana kuwa na imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, ambao uwezo wao ni mkubwa na wa milele kuliko shida hizo. Inamaana “[ku]shikilia kila kitu kizuri” (Moroni 7:19). Ina maanisha kuruhusu Upatanisho wa Yesu Kristo “na matumaini ya utukufu wake na uzima wa milele, yawe katika akili yako” (Moroni 9:25). Na hadi siku tukufu ya Ujio wa Pili wa Kristo, inamaanisha kutoacha “kazi [tuliyo nayo] ya kufanya … tuweze kumshinda adui wa haki” (Moroni 9:6).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Moroni 7:12–20

Nuru ya Kristo inanisaidia kuamua kati ya wema na mabaya.

Dunia ya sasa imejaa jumbe nyingi zenye kushawishi; ni jinsi gani tunaweza kujua kilicho sahihi na kilicho kibaya? Maneno ya Mormoni katika Moroni 7 yanatupatia kanuni kadhaa tunazoweza kutumia kuepuka “[ku]hukumu kwa makosa” (Moroni 7:18). Unapojifunza Moroni 7:12–20, tafuta kweli ambazo zinaweza kukusaidia kujua kile ambacho kitakuleta karibu na Mungu na kile ambacho hakitakusaidia. Unaweza kutumia kweli hizi kukusaidia kutathmini jumbe unazopata na uzoefu unaopata wiki hii, na kuamua kama vinakualika au kukushawishi kufanya mema au la. (ona Moroni 7:13).

Ona pia “Kuwahukumu Wengine,” Mada za Injili, topics.ChurchofJesusChrist.org; Kamusi ya Biblia, “Nuru ya Kristo.”

Moroni 7:20–48

Kupitia imani katika Kristo, naweza “kushikilia kila kitu kizuri.”

Baada ya kufundisha kuhusu jinsi ya kutofautisha baina ya wema na uovu, Mormoni aliuliza swali ambalo linaonekana kuwa linahusika leo hii: “Inawezekanaje [kushikilia] kila kitu kizuri?”—hasa wakati majaribu ya adui ni yenye ushawishi mkubwa (Moroni 7:20). Jibu la Mormoni laweza kupatikana kote katika sehemu iliyosalia katika sura ya 7. Unaposoma mistari ya 20–48, tafuta kweli ambazo zinakusaidia kutambua “kila kitu kizuri” ulichonacho kwa sababu ya Yesu Kristo. Je, ni kwa jinsi gani kuwa na imani kwake kunakusaidia kutafuta vitu vilivyo vizuri? Ni jinsi gani unaweza “kushikilia” vitu vizuri zaidi?

Ona pia Makala ya Imani 1:13.

Moroni 7:44–48

“Hisani ni upendo msafi wa Kristo.”

Rais Dallin H. Oaks alieleza: Sababu ya hisani kutokushindwa kamwe na sababu ya hisani kuwa kuu zaidi ya hata vitendo vya maana kabisa vya wema … ni kwamba hisani, ‘upendo msafi wa Kristo’ (Moro. 7:47), si kitendo lakini ni hali au hali ya kuwa. … Hisani ni kitu ambacho mtu huwa” (“Mwito wa Kuwa,” Ensign, Nov. 2000, 34). Unaposoma Moroni 7:44–48, Zingatia maelezo ya Mormoni kuhusu hisani, na usikilize mawazo kutoka kwa Roho Mtakatifu; Anaweza kukusaidia kupata njia za kufanya vizuri zaidi. Ni kwa nini tunahitaji imani na tumaini ili tupokee karama ya hisani?

Moroni 9:9

Je, usafi wa kimwili na wema wangu vinaweza kuchukuliwa kutoka kwangu?

Maelezo ya Mormoni kuhusu dhambi za kuogofya miongoni mwa Wanefi yamesababisha baadhi kuhitimisha kimakosa kwamba waathiriwa wa unajisi na dhuluma wamevunja sheria ya usafi wa kimwili. Hata hivyo, Mzee RichardG. Scott aliweka bayana kuwa si hivyo. Alifundisha, “Ninashuhudia kwa dhati kwamba wakati vitendo vya mtu mingine vya kimabavu, upotovu, au kujamiiana kwa maharimu vinakuumiza vibaya, kinyume na nia yako, haulaumiwi na hufai kuhisi kuwa na hatia” (“Kuponya Makovu ya Kusikitisha ya Dhuluma,” Ensign, Mei 1992, 32).

Moroni 9:25–26

Ninaweza kuwa na tumaini kwa Kristo bila kujali hali yangu.

Baada ya kuelezea uovu ambao alikuwa ameona, Mormoni alimwambia mwanawe asihuzunike. Ni nini kinachokuvutia kuhusu ujumbe wa Mormoni wa matumani? Inamaanisha nini kwako Kristo “[kukuinua] juu? Ni mitazamo ipi ya Kristo na kanuni za injili yake “viko katika akili yako” na hukupa tumaini? (Moroni 9:25).

Ona pia Dieter F. Uchtdorf, “Tumaini la Nuru ya Mungu,” Ensign au Liahona, Mei 2013, 70, 75–77.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

Moroni 7:5–11

Kulingana na Moroni 7:5–11, kwa nini ni muhimu kufanya mambo sahihi kwa ajili ya sababu sahihi? Tunawezaje kujua ikiwa tunasali na kutii amri za Mungu kwa “kusudi jema”? (Ayaaya ya 6).

Moroni 7:12–19

Ni jinsi gani ushauri wa Mormoni unaweza kutusaidia kufanya maamuzi mazuri kuhusu jinsi tunavyotumia wakati wetu na ni nani tunaye tumia naye wakati huo ? Unaweza kuwaalika wanafamilia kutafuta nyumbani kwako na “kushikilia kila kitu kizuri” (Moroni 7:19), au kuvishikilia, vitu vinavyowakaribisha “kufanya mema, na kumpenda Mungu, na kumtumikia” (Moroni 7:13). Wasifie kwa yale mazuri wanayotenda.

Moroni 7:29

Baada ya kusoma aya hii, washiriki wa familia wanaweza kuzungumza kuhusu miujiza ambayo wameishuhudia au jinsi ambavyo wameuona mkono wa Mungu maishani mwao.

Moroni 8:5–26

Ni nini Wanefi waliokuwa wanawabatiza watoto wadogo walikosa kuelewa kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo? Tunajifunza nini kuhusu Upatanisho kutokana na mafunzo ya Mormoni?

Moroni 8:16–17

Inamaanisha nini kuwa na “upendo kamili”? Unatusaidiaje kushinda hofu? Unatusaidiaje kufundisha ukweli kwa ujasiri? Ni kwa namna gani tunaukuza?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia muziki kumwalika Roho Mtakatifu na kufundisha mafundisho. “Muziki unazo nguvu zisizo na kipimo kwa ajili ya kutusogeza [sisi] kuelekea kuwa watu wa kiroho zaidi” (“Dibaji ya Urais wa Kwanza,” Nyimbo za Kanisa x). Wimbo kuhusu upendo, kama vile “Love One Another” (Nyimbo za Kanisa, na. 308), unaweza kuboresha mjadala wa familia kuhusu hisani katika Moroni 7:44–48.

Picha
Yesu Kristo

Picha ya Kristo Mwokozi, na Heinrich Hofmann

Chapisha