Njoo, Unifuate
Desemba 14–20. Moroni 10: “Mje kwa Kristo, na Mkamilishwe Ndani Yake”


“Desemba 14–20. Moroni 10: ‘Mje kwa Kristo, na Mkamilishwe ndani Yake,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Desemba 14–20. Moroni 10,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Yesu anawatokea Wanefi

Kwamba Muweze Kufahamu, na Gary L. Kapp

Desemba 14–20

Moroni 10

“Mje kwa Kristo, na Mkamilishwe Ndani Yake”

Washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa wamepata uzoefu wenye maana kwa kusoma Kitabu cha Mormoni mwaka huu. Ongeza kwenye uzoefu huu kumuhamasisha kila mmoja darasani kusoma maandiko.

Andika Misukumo Yako

ikoni kushiriki

Alika Kushiriki

Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kufikiria kuwa Moroni anatembelea darasa. Je, ni nini wangekisema kwake kuhusu kile alichoandika katika Moroni 10? Je, kuna mistari yoyote ambayo ina maana maalumu kwao? Pengine wangeweza kushiriki uzoefu ambao wamekuwa nao kwenye mistari hii.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Moroni 10:3–7

Ninaweza kujua ukweli kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

  • Washiriki wa darasa wanaweza kupata umaizi mpya ikiwa watasoma Moroni 10:3–5 kwa makini. Ili kuwasaidia, ungeweza kuandika vifungu muhimu vya maneno kutoka kwenye mistari hii kwenye vipande tofauti vya karatasi na kumpa kila mshiriki wa darasa au kila kundi la washiriki wa darasa. Waalike kutafakari au kujadili ni nini kifungu chao cha maneno humaanisha, ikijumuisha kile wanachoweza kufanya kukifanyia kazi katika maisha yao. Kisha mngeweza kusoma Moroni 10:3–5 pamoja, mkipumzika pale mnapofikia kifungu cha maneno ambacho mtu alikisoma ili kwamba mshiriki wa darasa aweze kushiriki mawazo yake.

  • Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki uzoefu ambao wamekuwa nao kwa kufanyia kazi mwaliko wa Moroni katika mistari hii, ungeweza kuwaalika kufikiria wanajaribu kumuhimiza rafiki au mwana familia kupata ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni. Ni kwa jinsi gani wangeweza kutumia Moroni 10:3–7? Ni uzoefu gani wangeweza kuushiriki? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia wengine kuelewa kile kinachomaanishwa kujua jambo “kwa uwezo wa Roho Mtakatifu”? (Moroni 10:5).

Moroni 10:8–25

“Msikatae karama za Mungu.”

  • Kwa nini maonyo: “Usikatae karama za Mungu” ni muhimu hasa katika siku hizi za mwisho? (Moroni 10:8). Wahimize washiriki wa darasa kutafakari swali hili wakati wakisoma Moroni 10:8–18. Ili kusaidia kuimarisha uaminifu wa washiriki wa darasa wa karama za roho, ungeweza kuwaalika kushiriki mifano ya watu kwa kutumia kila karama ambayo imeorodheshwa katika Moroni 10:9–16. Mifano ingeweza kuja kutoka kwenye maandiko, kutoka kwenye historia ya Kanisa, au kutoka kwenye maisha yao wenyewe. (Mifano kutoka katika Kitabu cha Mormoni imependekezwa katika “Nyenzo za Ziada.”) Mngeweza pia kujadili jinsi baadhi ya karama zilizoelezewa katika mistari hii zilidhihirika wakati wa ujio wa Kitabu cha Mormoni. Kwa nini ni muhimu kwa mtu ambaye anatafuta ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni kuamini katika karama za roho? Je, ni nini wakati mwingine tunafanya “kukataa” karama hizi katika maisha yetu? Ni kwa jinsi gani karama hizi hutusaidia sisi “kuja kwa Kristo, na kukamilishwa ndani yake”? (ona Moroni 10:30–33).

  • Njia nyingine ya kutafuta karama za roho iliyoelezewa katika mistari hii ni kuandika ubaoni swali kama Karama za roho ni nini? Zinatolewa kwa akina nani? Kwa nini zinatolewa? Na Ni kwa jinsi gani tunazipokea? Kisha waalike washiriki wa darasa kupekua Moroni 10:8–25 ili kupata majibu. (Maelezo ya Rais Brigham Young na Rais Dallin H. Oaks katika “Nyenzo za Ziada” yanaweza pia kusaidia.) Kwa kuongezea kwenye karama za roho zilizoorodheshwa katika mstari 9–16, ni “karama zipi nyingine za Mungu” tumepokea au kubarikiwa nazo? (Moroni 10:8). Unaweza kutaka kushiriki kile Mzee Bruce R. McComkie alichofundisha: “Karama za roho hazina mwisho kwa idadi na hazina kikomo kwenye aina. Zile zilizoorodheshwa katika maandiko ni mifano tu ya mmiminiko usio na kifani wa neema takatifu ambayo Mungu mwenye neema huwapa wale wanaompenda na kumtumikia” (Ushahidi Mpya katika Makala ya Imani [1985], 371).

Moroni 10:30–33

Ninaweza kukamilishwa kupitia neema ya Yesu Kristo.

  • Je, ni nini unahisi kingewasaidia washiriki wa darasa lako kukubali mwaliko wa Moroni wa “kuja kwa Kristo, na kukamilishwa ndani Yake”? (Moroni 10:32). Pengine kuanza na wimbo wa kanisa kwenye mada hii, kama vile “Njoo, Unifuate” (Nyimbo za Kanisa, namba. 116), kungeweza kumwalika Roho kwenye mjadala wenu, na washiriki wa darasa wangeweza kushiriki miunganiko yoyote wanayoona kati ya wimbo na kweli zinazopatikana katika Moroni 10:30–33. Je,, tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii na wimbo huu kuhusu kile humaanishwa kwa kuja kwa Kristo? Je, inamaanisha nini “kukamilika ndani ya Kristo”? (Ona pia Mafundisho na Maagano 76:50–53, 69). Shiriki hisia zako kuhusu kile hummanishwa kwa “kufanywa mkamilifu kupitia Yesu” (Mafundisho na Maagano 76:69), na wahimize washiriki wa darasa kushiriki hisia zao.

  • Kwa sababu haya ni majadiliano ya mwisho ya darasa lako juu ya Kitabu cha Mormoni mwaka huu, unaweza kutaka kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki baadhi ya mambo waliyohisi na kujifunza wakati waliposoma kitabu hiki. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kufanya hili, mngeweza kusoma Moroni 10:32–33 pamoja na kuwaomba washiriki wa darasa kutumia muda mchache kutafakari jinsi Kitabu cha Mormoni kilivyowasaidia kuja kwa Kristo. Ungeweza kuuliza: Je, ni kwa jinsi gani Kitabu cha Mormoni kimetusaidia kuwa na upendo mkubwa kwa Mungu? Je, ni kwa jinsi gani kimetusaidia kutegemea kikamilifu rehema za Kristo? Je, ni kwa jinsi gani kimetusaidia “kutokataa” nguvu ya Mwokozi? Waalike washiriki wa darasa kutoa shuhuda zao za Kitabu cha Mormoni na ushahidi wake wa Yesu Kristo.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutazamia kusoma Mafundisho na Maagano mwaka ujao, ungeweza kurejelea Moroni 10:9–16 na kuelezea kwamba karama hizi zote ni dhahiri katika Kanisa leo. Tunaposoma Mafundisho na Maagano, tutaona jinsi karama na nguvu za Mungu zilivyotumika kuifanya kazi Yake katika siku za mwisho.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Udhihirisho wa karama za roho katika Kitabu cha Mormoni.

Ushuhuda wa Rais Brigham Young wa karama za roho.

Imani. Wakati unapoamini kanuni za Injili na kupata kwa imani, ambayo ni karama ya Mungu, anaongeza imani zaidi, akiongeza imani kwenye imani. …

Karama ya Uponyaji. Niko hapa kushuhudia katika mamia ya matukio ya wanaume, wanawake, na watoto wakiponywa kwa nguvu za Mungu, kupitia kuwekewa mikono, na wengi nimeona wakiinuliwa kutoka kwenye milango ya kifo, na kurejeshwa karibu na umilele; na baadhi ambao roho zao kwa kweli ziliacha miili yao, zikirejea tena. Ninashuhudia kwamba nimeona wagonjwa wakiponywa kwa kuwekewa mikono, kulingana na ahadi ya Mwokozi. …

Unabii, Ufunuo, na Ufahamu. Kila mwanaume na mwanamke anaweza kuwa mfunuzi, na kuwa na ushuhuda wa Yesu, ambao ni roho ya unabii, na kuona kabla akili na mapenzi ya Mungu kuwahusu, epukana na uovu, na chagua kile kilicho chema” (Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Brigham Young [1997], 252–53).

“Shikilia kila karama nzuri.”

Rais Dallin H. Oaks alielezea jinsi kutafuta karama za roho kulivyombariki mama yake: “Baada ya kuwa amempoteza mume wake, mama yangu mjane alikuwa hajakamilika. Jinsi alivyoomba kwa kile alichohitaji kukamilisha jukumu lake la kulea watoto wadogo watatu! Alikuwa akitafuta, alistahili, na alibarikiwa! Maombi yake yalijibiwa kwa njia nyingi, ikiwa ni pamoja na kupokea karama za roho. Alikuwa nazo nyingi, lakini zile ambazo zinajitokeza wazi katika kumbukumbu zangu ni karama ya imani, ushuhuda, na hekima” (“Karama za Roho,” Ensign, Sept. 1986, 72).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tenga muda kwa wanaojifunza kushiriki. “Wakati wanafunzi wanaposhiriki kile wanachojifunza, si tu kwamba wanahisi Roho na kuimarisha shuhuda zao, bali pia wanawahimiza washiriki wengine wa darasa kugundua kweli kwa ajili yao wenyewe” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 30).