“Desemba 7–13. Moroni 7–9: ‘Kristo Akuinue Juu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Desemba 7–13. Moroni 7–9,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020
Desemba 7–13
Moroni 7–9
“Kristo Akuinue Juu”
Jukumu lako ni kuwasaidia watu kuja karibu na Mungu, siyo tu kuwasilisha somo. Jiandae kwa Ajili ya Shule ya Jumapili kwa kusoma Moroni 7–9 ukiwa na washiriki wa darasa akilini, ukitafuta kanuni ambazo zitawasaidia.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Mualike kila mshiriki wa darasa kurejea Moroni sura ya 7, 8, au 9 na kutafuta ukweli ambao una maana kwake. Washiriki wa darasa kisha wangeweza kushiriki ukweli waliopata na jinsi ulivyowabariki.
Fundisha Mafundisho
“Kile kilicho cha Mungu hukaribisha na kushawishi kufanya mema daima.”
-
Ili kuwa wafuasi wa Yesu Kristo, lazima tuweze kuhukumu kati ya wema na uovu. Pengine kujadili kweli katika Moroni 7:3–19 kungewasaidia washiriki wa darasa kuepuka kuhukumu “kwa makosa” (Moroni 7:18). Ili kujiandaa kwa majadiliano, nusu ya darasa wangeweza kuchunguza mistari hii kutafuta ushauri ambao Mormoni anatoa kuhusu jinsi ya kutambua kile kinachotoka kwa Mungu, na nusu nyingine wangeweza kutafuta jinsi ya kutambua kile kinachotoka kwa shetani. Kisha wangeweza kujadili kile walichopata na kushiriki mifano ya vitu ambavyo huwaalika wao “kufanya mema, na kumpenda Mungu, na kumtumikia” (Moroni 7:13). Ni kwa jinsi gani tunatumia ushauri wa Mormoni katika maamuzi yetu ya kila siku? Ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya chaguzi za haki na bado tukaonesha upendo kwa walio karibu yetu ambao hawaishi injili?
-
Watu wengi hujiuliza, “Nitajuaje kama msukumo nilionao umetoka kwa Mungu au kwenye mawazo yangu mwenyewe?” Ungeweza kuandika swali hili ubaoni na kuwaalika washiriki wa darasa kuchunguza Moroni 7:13–16 kupata kanuni ambazo zingeweza kusaidia kujibu swali hili. Ni jinsi gani ujumbe katika mistari hii hutusaidia kutambua ushawishi mtakatifu? Inaweza kusaidia kufafanua kwamba “Roho wa Kristo,” pia akijulikana kama nuru ya Kristo, wakati mwingine hujulikana kama dhamiri. Maelezo ya Rais Gordon B. Hinckley katika “Nyenzo za Zaida” na video “Patterns of Light: Discerning Light” (ChurchofJesusChrist.org) vinaweza pia kusaidia.
Wafuasi wa Yesu Kristo hutafuta imani, tumaini, na hisani.
-
Ili kusaidia darasa lako kuelewa vizuri muungano kati ya imani, tumaini, na hisani, ungeweza kuonesha kiti cha miguu-mitatu (au picha ya kiti hicho) na kuwaomba washiriki wa darasa kufikiria jinsi imani, tumaini, na hisani ni kama miguu hii mitatu (ona maelezo ya Rais Dieter F. Uchtdorf katika “Nyenzo za Zaida”). Kisha ungeweza kuwaalika kuchagua moja ya sifa hizi na kutafuta kile Mormoni anachofundisha kuihusu katika Moroni 7:21–48. Jadili maswali kama yafuatayo: kwa nini tunahitaji imani na tumaini ili kupokea karama ya hisani? Ni kwa jinsi gani kila moja ya sifa hizi hutuunganisha kwa Yesu Kristo? Kwa nini sifa hizi ni muhimu kwa mfuasi wa Yesu Kristo? Nini kingeweza kutokea kwetu kama tungepoteza imani? Tumaini? hisani? Waalike washiriki wa darasa kuchukua muda mchache kuandika misukumo waliyopata.
Kuelewa mafundisho sahihi kunaweza kutusaidia kufanya chaguzi sahihi.
-
Darasa lako linaweza lisihitaji kujadili kwa nini si sahihi kubatiza watoto wadogo, lakini maneno ya Mormoni juu ya mada hii yanaweza kuwasaidia kuona hatari za mafundisho ya uongo kwa ujumla. Ili kuonyesha kwa mfano jinsi Kitabu cha Mormoni “[kinavyofadhaisha] mafundisho ya uwongo” (2 Nefi 3:12), ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma Moroni 8:4–21 katika makundi au kibinafsi. Nusu yao wangeweza kutafuta mafundisho ambayo Mormoni alihisi watu hawakuyaelewa, ikiwa ni pamoja na Upatanisho wa Yesu Kristo (ona mstari wa 20) na uwajibikaji (ona mstari wa 10). Nusu wengine wangeweza kutafuta athari za makosa ya watu. Kila kundi lingeweza kushiriki pamoja na darasa kile walichopata. Ni nini mistari hii hutufunza kuhusu umuhimu wa kujifunza na kuishi kwa mafundisho sahihi? Ni wapi tunaweza kupata ufafanuzi sahihi wa mafundisho ya Kristo? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuhakikisha uelewa wetu wa mafundisho ni sahihi?
-
Pengine darasa lako lingenufaika kwa kufuata mfano wa Mormoni wa kumsaidia mtu kufanya chaguzi sahihi kwa kuwafundisha mafundisho sahihi. Ungeweza kufanya hili kwa kuwaalika washiriki wa darasa kumfikiria mtu kutoka kwenye maandiko ambaye alifanya uchaguzi mbaya. Ni ukweli upi wa kimafundisho ungeweza kumsaidia mtu huyo kuepuka kufanya uchaguzi huo mbaya tena? Wape washiriki wa darasa dakika chache kutafuta maandiko au maelezo kutoka kwenye mkutano mkuu wa karibuni ambayo yangemsaidia mtu kuelewa ukweli wa mafundisho. Kisha ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki kile walichopata.
Tunaweza kuwa na tumaini katika Kristo, bila kujali hali zetu.
-
Ujumbe wa mwisho wa Mormoni ulioandikwa kwa mwana wake katika Moroni 9:25–26 unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kupata tumaini katika Kristo, hata katika hali zinazoonekana zisizo na tumaini. Pengine ungeweza kuanza kwa kuuliza washiriki wa darasa kushiriki sababu za Mormoni kuweza kuhisi kufa moyo. Kisha wangeweza kusoma mistari hii na kuorodhesha ubaoni kweli ambazo Mormoni alimhimiza Moroni kufokasi juu yake. Ni kwa jinsi gani kweli sawa na hizi “hutuinua [sisi] juu” katika siku yetu? Washiriki wa darasa wangeweza pia kushiriki mifano ya “rehema na uvumilivu” wa Mungu ambao wameshuhudia. Au wangeweza kushiriki mawazo kusaidiana kila mmoja kumweka Mwokozi na injili Yake “katika akili [yetu] milele,” hata pale tunapokabiliana na kufa moyo (mstari wa 25).
Himiza Kujifunza Nyumbani
Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma Moroni 10, ungeweza kupendekeza kwamba utakuwa ni muda muafaka wa kutafakari juu ya jinsi walivyopata ushahidi mpya wa ukweli wa Kitabu cha Mormoni walipokisoma mwaka huu.
Nyenzo za Ziada
Je, unatoka kwa Roho?
Ili kujibu swali “Ni kwa jinsi gani tunatambua ushawishi wa Roho?” Rais Gordon B. Hinckley alimnukuu Moroni 7:13 na kusema: “Sidhani [ni] vigumu sana, hasa. … Je, unamshawishi mtu kufanya mema, kuinuka, kusimama wima, kufanya jambo sahihi, kuwa mkarimu, kuwa mpaji? Basi ni wa Roho wa Mungu” (Mafundisho ya Gordon B. Hinckley [1997], 260–61).
Imani, tumanini na hisani.
Rais Dieter F. Uchtdorf alilinganisha imani, tumaini, na hisani na kiti chenye miguu mitatu, akielezea kwamba sifa hizi tatu “huweka sawa maisha yetu licha ya umbo la nje la kuparuza au ambalo haliko sawa tunaloweza kukabiliana nalo. …
“Imani, tumaini, na hisani hukamilishana , na wakati moja inapoongezeka, nyingine hukua vilevile. Tumaini huja kwa imani, kwani pasipo imani, hakuna tumaini. Kwa njia hiyo hiyo imani huja kwa tumaini, kwani imani ni ‘kiini cha mambo yatumainiwayo.’
“Tumaini ni kipeo kwa vyote imani na hisani. Wakati kutokutii, kufa moyo, na kuahirisha kunapomomonyoa imani, tumaini lipo pale kushikilia imani. Wakati kukata tamaa na kukosa uvumilivu kunapoipa changamoto hisani, tumaini hukaza kusudio letu na hutusihi kuwajali wanadamu wenzetu hata bila kutarajia malipo. Kadiri tumaini letu linavyokuwa angavu, ndivyo imani yetu inavyokua. Tumaini letu linavyokuwa imara, ndivyo hisani yetu inavyokuwa safi” (“Nguvu isiyo na Mwisho ya Tumaini,” Ensign au Liahona, Nov. 2008, 21, 23–24).
“Upendo msafi wa Kristo.”
Mzee Jeffrey R. Holland alipendekeza maana mbili zinazowezekana za kifungu cha maneno “upendo msafi wa Kristo”:
“Moja … ni aina ya rehema, ya upendo wa kusamehe ambao wafuasi wa Kristo wanapaswa kuwa nao kwa kila mmoja. …
“[Maana nyingine ni] upendo wa Kristo usioshindwa, wa mwisho na wa upatanisho kwa ajili yetu. … Ni hisani hiyo—upendo wake msafi kwetu—ambao bila ya huo tusingekuwa kitu chochote” (Kristo na Agano Jipya: Ujumbe wa Kimasiya wa Kitabu cha Mormoni [1997], 336).