“Somo la 7: Familia,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 7,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 7
Family
Shabaha: Nitajifunza kuuliza na kujibu maswali kuhusu wanafamilia.
Personal Study
Jiandae kwa ajili kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: Exercise Faith in Jesus Christ
Tumia imani katika Yesu Kristo.
Jesus Christ can help me do all things when I exercise faith in Him.
Yesu Kristo anaweza kunisaidia kufanya vitu vyote ninapoonyesha imani Kwake.
Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu. Yeye ana uweza wote. Katika maandiko, tunasoma kuhusu mtu ambaye alitumia imani yake katika Yesu Kristo. Mtoto wa mtu huyu alikuwa mgonjwa sana na hakuna mtu angeweza kumsaidia. Baba alimwomba Yesu amponye mtoto wake. Yesu alimwambia.
“Ukiweza, yote yawezekana kwake aaminiye. … “Mara babaye yule kijana akapaza sauti akasema akilia, Bwana, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu. … Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama” (Marko 9:23–24, 27).
Kama mtu huyu, unaweza kuanza na tumaini na imani ambayo tayari unayo. Kisha unaweza kukuza imani yako kupitia sala na kujifunza maandiko. Unaweza pia kukuza imani yako unapojaribu kujifunza Kiingereza. Unaweza kuanza na kile unachojua sasa. Fokasi juu ya kile unachoweza kufanya kwa Kiingereza, na ukitumie mara nyingi uwezavyo. Jaribu kusikiliza, kusoma, kusema na kuandika kwa Kiingereza kila siku. Kadiri unavyotenda kwa imani ya kuipa bidii yako yote, Yeye anaweza kusaidia imani yako kukua.
Ponder
-
Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia imani katika Yesu Kristo?
-
Ni kwa jinsi gani unaweza kukuza imani yako unapojifunza Kiingereza?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo.
Tell me about … |
Nielezee kuhusu … |
yourself |
wewe mwenyewe |
Nouns
cousin/cousins |
binamu/binamu |
eyes |
macho |
glasses |
miwani |
hair |
nywele |
mustache |
masharubu |
Adjectives
blue |
bluu |
brown |
kahawia |
green |
kijani |
hazel |
ukungu |
blonde |
nywele zenye rangi ya shaba |
black |
nyeusi |
gray |
kijivu |
red |
nyekundu |
white |
nyeupe |
long |
ndefu |
short** |
fupi |
tall |
ndefu |
short* |
fupi |
married |
kuoa/kuolewa |
single |
mseja |
**Katika Kiingereza, neno fupi linaweza kurejelea kimo au urefu.
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
A: Tell me about your (noun).B: They have (adjective) (noun).
Examples
A: Tell me about your brother.B: He has a mustache.
A: Tell me about your sisters.B: They have black hair.
A: Tell me about your aunt.B: She has blue eyes.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kutambua mipangilio hii wakati wa mazoezi yako ya kila siku. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
Q: Is your (noun) (adjective)?A: Yes, he is (adjective).
Examples
Q: Is your sister married?A: Yes, she is married.
Q: Are you married?A: No, I am single.
Q: Are your sisters tall?A: No, they are short.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanyia mazoezi mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Chagua mtu kutoka kwenye mojawapo ya makundi hapo chini. Usimwambie mwenzako ni mtu gani unamchagua. Sema sentensi tatu kuhusu mtu huyu. Mwenzako akisie ni nani huyu. Chukueni zamu.
New Vocabulary
bald |
upara |
beard |
ndevu |
curly |
enye kupinda |
straight |
iliyonyooka |
old |
mzee |
young |
kijana |
Example: Maria
-
A: She has blue eyes. She has gray hair. She has glasses.
-
B: Is it Maria?
-
A: Yes!
Image Group 1
Image Group 2
Image Group 3
Image Group 4
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Chagua wanafamilia watatu. Uliza na ujibu maswali kuhusu kila mtu. Sema mengi kadiri uwezavyo. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
Example
-
A: Tell me about your cousin.
-
B: My cousin has curly hair. She has blue eyes.
-
A: Is your cousin tall?
-
B: Yes, she is tall.
-
A: Is your cousin married?
-
B: No, she is single.