Kujifunza Kiingereza
Somo la 9: Mavazi na Rangi


“Somo la 9: Mavazi na Rangi,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Somo la 9,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi

wasichana wakitembea

Lesson 9

Clothing and Colors

Shabaha: Nitajfunza kuelezea ni kitu gani mtu amevaa.

Personal Study

Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.

ikoni a
Study the Principle of Learning: Counsel with the Lord

Shauriana na Bwana

I improve my learning by counseling with God daily about my efforts.

Ninaweza kuboresha kujifunza kwangu kwa kushauriana na Mungu kila siku kuhusu juhudi zangu.

Uongofu ni mchakato ambao unatokea baada ya muda kupita. Mungu anataka kukusaidia ujifunze na ukue. Yeye anataka kukusaidia ujifunze jinsi ya kuchukua hatua ndogo ndogo ili kutimiza mambo makubwa. Kitabu cha Mormoni husimulia juu ya mtu mwenye nguvu ya imani aliyeitwa Alma. Yeye alikuwa nabii wa Mungu na kiongozi wa nchi yake. Alma alifundisha:

“Kupitia vitu vilivyo vidogo na rahisi vitu vikubwa hutendeka. … Shauriana na Bwana kwenye matendo yako yote, na atakuongoza kwa yale mema” (Alma 37:6, 37).

Bwana hufanya kazi kupitia vitu vidogo na rahisi. Vitendo vidogo vinaweza kuleta matokeo makubwa baada ya muda Sisi tunasali kwa Baba yetu wa Mbinguni katika jina la Mwanawe, Yesu Kristo. Kupitia sala na kujifunza maandiko, unaweza kushauriana na Bwana. Yeye anaweza kukusaidia kuchagua njia ndogo ndogo na rahisi ili kuwa bora. Je, unahitaji kuboresha uelewa wako wa kusikiliza? Unaposhauriana na Mungu katika sala, unaweza kuamua kutumia dakika 10 katika siku kufanya mazoezi ya Kiingereza na rafiki. Je, unasumbuka kukumbuka maneno mapya? Unaposhauriana na Mungu, unaweza kuamua kupitia tena maneno unapokuwa unasafiri katika basi. Juhudi zako thabiti zitaleta “mambo makubwa” unapojifunza Kiingereza.

mvulana na msichana wakisali kitandani

Ponder

  • Je, utamaduni wako una msemo sawa na huu “vitu vidogo na rahisi”?

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kushauriana na Mungu kuhusu juhudi zako?

  • Je, ni vitu gani vidogo vidogo unavyoweza kufanya kila siku ili kujifunza Kiingereza?

ikoni b
Memorize Vocabulary

Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kutumia maneno katika maisha yako. Fikiria kuhusu lini na wapi ungeweza kutumia maneno haya.

I’m

Mimi ni

he’s

yake

she’s

yake

they’re

wao ni

wearing

wamevaa

looking for

wanatafuta

this/these

hiki/hivi

that/those

kile/vile

clothing

mavazi

color/colors

rangi/rangi

Nouns

coat/coats

koti/makoti

dress/dresses

gauni/magauni

pants

suruali

shirt/shirts

shati/mashati

shoe/shoes

kiatu/viatu

skirt/skirts

sketi/sketi

sweater/sweaters

sweta/masweta

Adjectives

orange

chungwa

purple

zambarau

yellow

njano

Ona somo la 7 kwa ajili ya colorszaidi.

ikoni c
Practice Pattern 1

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”

Q: What are you wearing?A: I’m wearing a (adjective) (noun).

Questions

maswali ya mpangilio wa 1 wewe umevaa nini

Answers

majibu ya mpangilio wa 1 Nimevaa kivumishi nomino

Examples

shati jekundu la polo

Q: What is he wearing?A: He’s wearing a red shirt.

Q: What is she wearing?A: She’s wearing an orange skirt.

Q: What are they looking for?A: They’re looking for black shoes.

ikoni d
Practice Pattern 2

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali.

Q: Do you like this (adjective) (noun)?A: Yes, I like that (adjective) (noun).

Questions

maswali ya mpangilio wa 2 unapenda kivumishi nomino

Answers

majibu ya mpangilio wa 2 ndiyo, ninapenda hiyo kivumishi nomino

Examples

jozi ya viatu vyekundu

Q: Do you like this green sweater?A: No, I don’t like that green sweater.

Q: Do you like these red shoes?A: Yes, I like those shoes.

ikoni e
Use the Patterns

Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.

Additional Activities

Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources au katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 1.

Act in Faith to Practice English Daily

Endelea kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi”. Pitia tena lengo lako la kujifunza na utathmini juhudi zako.

Conversation Group

Discuss the Principle of Learning: Counsel with the Lord

(20–30 minutes)

mvulana na msichana wakisali kitandani

ikoni ya 1
Activity 1: Practice the Patterns

(10–15 minutes)

Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.

Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:

  • Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.

  • Fanya mazoezi ya kujibu maswali.

  • Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.

Rudia mpangilio wa 2

ikoni ya 2
Activity 2: Create Your Own Sentences

(10–15 minutes)

New Vocabulary

belt/belts

kanda/mikanda

sock/socks

soksi/soksi

suit/suits

suti/suti

tie/ties

tai/tai

Part 1

Uliza na ujibu maswali kuhusu mavazi yako. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.

Example
  • A: What are you wearing?

  • B: I’m wearing blue pants, a white shirt, yellow socks, and red shoes.

Part 2

Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu mavazi ya kila mtu. Sema mengi kadiri uwezavyo. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.

Example: Eliana
mwanamke amenyanyua kombe, akiwa amevaa shati la kijivu na suruali nyeusi
  • A: What is Eliana wearing?

  • B: She’s wearing a gray shirt and black pants.

Image 1: Nadia

mwanamke akicheza dansi nyumbani

Image 2: Obasi

mwanaume anatabasamu akiwa katika suti

Image 3: Mateo

mvulana akiwa na kaptula ya bluu na shati ya njano akicheza mpira wa miguu (soka)

Image 4: Hina

msichana akiwa na shati jeusi, kaptula nyeusi, soksi nyeusi na viatu vya njano anacheza mpira wa miguu (soka)

ikoni ya 3
Activity 3: Create Your Own Conversations

(15–20 minutes)

Fanya igizo. Mwenza A hufanya kazi katika duka la mavazi. Mwenza B anafanya ununuzi wa nguo na viatu. Uliza na ujibu maswali kuhusu vitu katika kila picha. Badilishaneni nafasi. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.

Example

jozi ya viatu vya kahawia na viatu vya bluu
  • A: What are you looking for?

  • B: I’m looking for shoes.

  • A: Do you like these brown shoes?

  • B: No, I don’t like those brown shoes.

Image 1

jozi ya viatu vya kijani na viatu vyekundu

Image 2

mavazi ya wanawake yamening’inizwa dukani

Image 3

mavazi ya wanaume yamening’inizwa dukani

Image 4

soksi za aina mbali mbali za rangi

Image 5

tai za aina mbali mbali za rangi

Evaluate

(5–10 minutes)

Tathmini maendeleo yako juu ya shabaha na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Evaluate Your Progress

I can:

  • Talk about clothing and colors.

    Zungumza kuhusu mavazi na rangi.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Say what I and others are wearing.

    Sema mimi na wengine tumevaa nini.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha

Evaluate Your Efforts

Tathmini juhudi zako za:

  1. Kusoma kanuni ya kujifunza.

  2. Kukariri msamiati.

  3. Kfuanyia mazoezi mpangilio.

  4. Kufanya mazoezi kila siku.

Weka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.”

Shiriki lengo lako na mwenzako.

Act in Faith to Practice English Daily

“Tunaweza kuomba kwa Baba wa Mbinguni na kupokea mwongozo na maelekezo, na kuwezeshwa kukamilisha vitu kiurahisi ambavyo hatungeweza kufanya sisi wenyewe. …

“Sali … na kisha sikiliza! Andika mawazo ambayo yanakuja kwenye akili yako. Andika hisia zako na fuatilia matendo yako ambayo unasukumwa kuyatenda” (Russell M. Nelson,“Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu,” Liahona, Mei 2018, 94–95).