“Somo la 19: Fedha,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 19,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 19
Money
Shabaha: Nitajifunza kuuliza na kujibu maswali kuhusu kununua vitu.
Personal Study
Jiandae kwa ajili kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: Exercise Faith in Jesus Christ
Tumia imani katika Yesu Kristo.
Jesus Christ can help me do all things as I exercise faith in Him.
Yesu Kristo anaweza kunisaidia kufanya vitu vyote ninapoonyesha imani Kwake.
Siku moja, Yesu Kristo alikuwa akifundisha maefu ya watu jangwani. Yesu na wanafunzi Wake walikuwa na wasi wasi kwa sababu watu hawakuleta chakula chochote. Mvulana mmoja katika kundi alitoa mikate mitano na samaki wawili. Watu wengi walishangaa jinsi mikate mitano na samaki wawili vingeweza kuwalisha wale watu wote. Lakini Yesu alimshukuru Mungu kwa ajili ya chakula kile, alikibariki, akakigawa katika vikapu na kuwatuma wanafunzi wakagawe. Biblia inasema:
“Wakala wote wakashiba; na … [kukawa kumebakia] vikapu kumi na viwili, vimejaa” (Mathayo 14:20).
Kila mtu alikula, na kukawa na chakula zaidi. ulikuwa ni muujiza. Vivyo hivyo, wewe unaweza kuhisi huna muda wa kutosha kujifunza Kiingereza. Fuata mfano wa Yesu katika hadithi hii. Mshukuru Mungu kwa ajili ya muda na nguvu ulizo nazo na muombe Yeye azibariki. Kama utatoa kile ulichonacho kwa imani, Mungu anaweza kuongeza uwezo wako. Hata kama una wakati mdogo tu, pengine unaweza kujifunza mipangilio michache au kujaribu kutumia maneno machache mapya kila siku. Mungu anaweza kuzifanya juhudi zako ziwe na mafanikio zaidi. Kuwa na imani katika Yesu Kristo na kufuata mfano Wake kunaweza kukusaidia wewe kufanya mengi zaidi kuliko unavyofikiria inawezakana.
Ponder
-
Ni kwa jinsi gani Mungu anaweza kukusaidia wewe kujifunza Kiingereza?
-
Fikiria wakati ambapo Mungu alikusaidia wewe kufanya zaidi kuliko vile ulivyofikiri ilikuwa inawezekana. Je, ulifanya nini? Je, Yeye alifanya nini?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kutumia maneno hayo katika maisha yako. Fikiria kuhusu lini na wapi ungeweza kutumia maneno haya.
buy |
nunua |
cost/costs |
gharama/gharama |
want |
kutaka |
How much does this cost? |
Je, hiki ni bei gani? |
Nouns
coat/coats |
koti/makoti |
dress/dresses |
gauni/magauni |
pants |
suruali |
shirt/shirts |
shati/mashati |
shoe/shoes |
kiatu/viatu |
tie/ties |
tai/tai |
car/cars |
gari/magari |
phone/phones |
simu/simu |
Price
$50/fifty dollars |
$50/dola hamsini |
Adjectives
cheap |
rahisi |
expensive |
ghali |
good |
nzuri |
bad |
mbaya |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
Q: How much does this (noun) cost?A: It costs (price).
Examples
Q: How much does this phone cost?A: It costs five hundred dollars.
Q: How much do these pants cost?A: They cost twenty dollars.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kujifunza zaidi kuhusu mipangilio katika somo hili. Fikiria kutumia vitabu vya sarufi au tovuti.
Q: Do you want to buy this (noun)?A: Yes, this (noun) is (adjective).
Examples
Q: Do you want to buy that car?A: Yes, that car is cheap.
Q: Does she want to buy these shoes?A: No, those shoes are expensive.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali.
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Tazama picha. Chagua bei ya kila kitu Usimwambie mwenzako ni bei gani umechagua. Uliza na ujibu maswali kuhusu kiasi gani kila kitu kinagharimu. Chukueni zamu.
New Vocabulary
apple/apples |
tufaa/matufaa |
motorcycle/motorcycles |
pikipiki/pikipiki |
table/tables |
meza/meza |
Example
-
A: How much do your apples cost?
-
B: They cost three dollars. Do you want to buy these apples?
-
A: Yes, those apples are cheap.
-
B: How much do your apples cost?
-
A: My apples cost five dollars. Do you want to buy these apples?
-
B: No, those apples are expensive.
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Fanya Igizo. Mwenza B anafanya ununuzi wa mavazi na ana dola 50 za kutumia. Mwenza A hufanya kazi katika duka la mavazi. Uliza na ujibu maswali kuhusu vitu katika kila picha. Mwenza A anaamua kununua na hawezi kutumia zaidi ya dola 50. Badilishaneni nafasi.
New Vocabulary
pretty |
nzuri |
ugly |
mbaya |
Why not? |
Kwa nini? |
Yes, I want to buy it. |
Ndiyo, ninataka kuinunua. |
No, I don’t want to buy it. |
Hapana, sitaki kuinunua. |
Example
-
A: How much does this shirt cost?
-
B: It costs 15 dollars. Do you want to buy it?
-
A: No, I don’t want to buy it.
-
B: Why not?
-
A: That shirt is expensive and ugly.