Vijana
Ujumbe kutoka kwa Urais wa Kwanza


“Ujumbe kutoka kwa Urais wa Kwanza,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi (2022)

“Ujumbe Kutoka kwa Urais wa Kwanza,” Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana

Picha
Mchoro wa mwanamke akikagua mkono wa Yesu miongoni mwa watazamaji.

Ujumbe kutoka kwa Urais wa Kwanza

Wapendwa akina kaka na akina dada vijana,

Tunawapenda ninyi na tuna imani kubwa kwenu. Ninyi kwa hakika ni miongoni mwa roho wateule wa Baba wa Mbinguni, walioletwa duniani wakati huu kufanya mambo muhimu.

Yawezekana kukawa na nyakati ambapo hauhisi kuwa na nguvu na mwenye kuweza. Hiyo ni kawaida. Hususani katika nyakati hizo, mgeukie Mwokozi. Yeye ni “nguvu kwa vijana.”

Mwongozo huu utakusaidia kujenga msingi thabiti kwa ajili ya kufanya chaguzi ili kubaki kwenye njia ya agano. Utakusaidia kujiandaa kufanya maagano matakatifu hekaluni, kujiandaa kuhudumu misheni na kupata furaha katika kumfuata Yesu Kristo katika maisha yako yote. Tunatumaini unajihisi kwamba wewe ni wa Kanisa la Mwokozi na una nguvu kutoka Kwake ya kukamilisha azma Zake kwa ajili yako.

Tunajua Mungu yu hai. Ni sala yetu kwamba utabaki imara kwenye njia ya agano ambayo inaongoza kurudi kwa Baba yako wa Mbinguni. Unapofanya hivi, utakuwa ushawishi kwa mema, kushiriki injili kwa furaha na kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi.

Urais wa Kwanza

Chapisha