Vijana
Kupata Shangwe katika Kristo


“Kupata shangwe katika Kristo,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi (2022)

“Kupata shangwe katika Kristo,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana

Picha
Mchoro wa Yesu na mwanamke wakizungumza karibu na kisima.

Kupata Shangwe katika Kristo

Chaguzi ni muhimu. Chaguzi zenye msingi juu ya mafundisho ya injili ni hatua ambazo zinakuongoza karibu zaidi kwa Baba yako wa Mbinguni na Yesu Kristo. Yesu alisema, “Mambo haya nimewaambia, … ili furaha yenu itimizwe” (Yohana 15:11). Kwa kila hatua kumwelekea Yeye, utahisi kuwa karibu zaidi na Roho na uhusiano wako wa agano na Mungu utakuwa imara zaidi.

Lakini hiyo haimaanishi kwamba njia itakuwa haina matatizo. Na kwa kuwa hakuna anayetembea kiukamilifu kwenye mstari ulionyooka, mara kwa mara hakiki mwelekeo wako na heshimu amri za Mungu. Shika maagano yako na Mungu, na jiandae kufanya maagano zaidi. Maagano yanakuunganisha kwa Baba wa Mbinguni na Mwokozi. Yanaongeza nguvu ya Mungu katika maisha yako na yanakuandaa kupokea uzima wa milele.

Katika chaguzi zote zinazowezekana, mmoja ambao ni muhimu zaidi ni uchaguzi wa kumfuata Yesu Kristo. Yeye ni nguvu kwa vijana. Injili Yake ni njia yenye shangwe kurudi kwa Baba yako wa Mbinguni.

Chapisha