Vijana
Fanya chaguzi zenye uvuvio


“Fanya chaguzi zenye uvuvio,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi (2022)

“Fanya chaguzi zenye uvuvio,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana

Picha
Msichana akisali kwenye kitanda chake.

Fanya chaguzi zenye uvuvio

Ndani ya Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana, utapata mafundisho ya Yesu Kristo na ya manabii Wake. Ukiwa na kweli hizi kama mwongozo wako, unaweza kufanya chaguzi zenye uvuvio ambazo zitakubariki sasa na milele yote.

Yesu Kristo ndiye njia ya kwenda kwenye shangwe ya milele. Kadiri unavyotumia haki yako ya kujiamulia kumfuata Yesu Kristo, unakuwa kwenye njia ambayo inaongoza kwenye furaha ya milele. Mfanye Yesu Kristo awe kiwango chako, msingi wako imara wa mwamba. Jenga maisha yako juu ya mafundisho Yake na pima chaguzi zako kwa mafundisho hayo. Maagano unayofanya unapobatizwa, wakati wa sakramenti na hekaluni ni matofali ya kujengea msingi wako imara katika Kristo. Bado utakabiliana na mapambano na majaribu, lakini Baba wa Mbinguni na Mwokozi watakusaidia kuyapita yote.

Wewe ni mtoto mpendwa wa kiroho wa Mungu. Mpango Wake mkuu wa furaha unafanya iwezekane kwa wewe kukua kiroho na kukuza uwezekano wako wa kiungu. Hii ndiyo sababu alimtuma Yesu Kristo kuwa Mwokozi wako.

Baba yako wa Mbinguni ana tumaini juu yako. Amekupa baraka kuu, ikijumuisha utimilifu wa injili na ibada takatifu na maagano ambayo yanakuunganisha wewe Kwake na kuleta nguvu Yake ndani ya maisha yako. Pamoja na baraka hizo huja ongezeko la majukumu. Anajua unaweza kuleta utofauti katika ulimwengu na hiyo inahitaji, katika hali nyingi, kuwa tofauti na ulimwengu. Tafuta mwongozo wa Baba yako wa Mbinguni pale unapofanya chaguzi. Yeye atakubariki kwa mwongozo wa kiungu kupitia Roho Mtakatifu.

Azma ya Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana si kukupa jibu la “ndiyo” au “hapana” kuhusu kila uwezekano wa uchaguzi unaoweza kukabiliana nao. Badala yake, Bwana anakupa mwaliko wa kuishi katika njia iliyo ya juu zaidi na takatifu zaidi—njia Yake. Mwongozo huu utakufundisha kuhusu njia Yake. Unaelezea kweli ambazo Yeye amezifunua. Fanya kweli hizi ziwe mwongozo wako wa kufanya chaguzi—chaguzi kubwa, kama vile kufanya maagano hekaluni na kuhudumu misheni, vile vile chaguzi za kila siku, kama vile jinsi ya kuwatendea watu au jinsi ya kutumia muda wako.

Wakati wengine wanaweza kukusaidia, ukuaji wako wa kiroho ni wako binafsi. Ni kati yako wewe na Bwana. Yeye anaujua moyo wako na ni Yeye pekee anaweza kuwa Hakimu wa mwisho. Fanya kwa uwezo wako wote ili kujiboresha kila siku, shika amri za Mungu na heshimu maagano yako na wasaidie wengine kuja karibu zaidi na Mwokozi.

Ona Mosia 4:29–30 (Njia za kutenda dhambi hazihesabiki, kwa hiyo hatuna budi kujichunga wenyewe); Helemani 5:12 (jenga msingi wako juu ya Kristo); Mafundisho na Maagano 45:57 (mfanye Roho Mtakatifu awe mwongozo wako); 82:15 (jiunganishe kwa Bwana kupitia maagano).

Picha
Watu wakitumia ikoni ya ramani

Jinsi mwongozo huu ulivyopangiliwa

Kila mada ina sehemu tatu:

  1. Kweli za milele, au mafundisho ya injili ya urejesho ya Yesu Kristo

  2. Mialiko kutenda juu ya kweli hizo

  3. Baraka zilizoahidiwa ambazo Bwana anatoa kwa wale wanaoyaishi mafundisho Yake

Chapisha