“Kiambatisho,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi (2022)
“Kiambatisho,” Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana
Kiambatisho
Njia moja ya kutathmini maendeleo yako kwenye njia ya agano ni kutafakari maswali ya hapo chini. Ni maswali unayoulizwa unaposailiwa kupokea kibali cha hekaluni, lakini usingoje kwa ajili ya usaili. Fanya mapitio yako mwenyewe ya kiroho. Dhima ya Wasichana, Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni na Amri Kumi vinaweza pia kuwa nyenzo zenye msaada katika kujitathmini kwako binafsi.
Maswali ya kibali cha hekaluni kwa ajili ya vijana
Je, una imani katika na ushuhuda juu ya Mungu, Baba wa Milele; Mwanaye, Yesu Kristo; na Roho Mtakatifu?
Je, una ushuhuda juu ya Upatanisho wa Yesu Kristo na wa jukumu Lake kama Mwokozi na Mkombozi wako?
Je, unao ushuhuda juu ya Urejesho wa injili ya Yesu Kristo?
Je, unamkubali Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kama nabii, mwonaji na mfunuzi na kama mtu pekee duniani aliyepewa mamlaka ya kutumia funguo zote za ukuhani? Je, unawakubali washiriki wa Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji na wafunuzi? Je, unawakubali Viongozi Wakuu wengine wenye Mamlaka na viongozi wa Kanisa wa eneo lako?
Bwana amesema kwamba mambo yote lazima “yafanyike katika usafi” mbele Yake (Mafundisho na Maagano 42:41). Je, unajitahidi kuwa msafi wa maadili katika mawazo na tabia yako? Je, unatii sheria ya usafi wa kimwili?
Je, unafuata mafundisho ya Kanisa la Yesu Kristo katika tabia yako ya siri na ya hadharani kwa wanafamilia yako na watu wengine?
Je, unaunga mkono au kudhamini mafundisho yoyote, matendo au injili yaliyo kinyume na yale ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za Mwisho?
Je, unajitahidi kuitakasa siku ya Sabato, kote nyumbani na kanisani; kuhudhuria mikutano yako; kujiandaa na kupokea sakramenti kwa kustahili; na kuishi maisha yako sawa sawa na sheria na amri za injili?
Je, unajitahidi kuwa mwaminifu katika yote unayofanya?
Je, wewe ni mlipa zaka kamili?
Je, unaelewa na kutii Neno la Hekima?
Je, kuna dhambi nzito katika maisha yako ambazo zinahitaji kushughulikiwa na mamlaka ya ukuhani kama sehemu ya toba yako?
Je, unajiona kuwa ni mwenye kustahili kuingia katika nyumba ya Bwana na kushiriki katika ibada za hekaluni?
Dhima ya Wasichana
Mimi ni binti mpendwa wa wazazi wa Mbinguni, mwenye asili takatifu na hatima ya milele.
Kama mfuasi wa Yesu Kristo, ninajitahidi kuwa kama Yeye. Ninatafuta na kufanyia kazi ufunuo binafsi na kuwahudumia wengine katika jina Lake takatifu.
Nitasimama kama shahidi wa Mungu nyakati zote na katika vitu vyote na katika mahali popote.
Ninapojitahidi kuwa mwenye kustahili kuinuliwa, ninathamini zawadi ya toba na kutafuta kuwa bora kila siku. Kwa imani, nitaimarisha nyumba na familia yangu, kufanya na kushika maagano matakatifu, na kupokea ibada na baraka za hekalu takatifu.
Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni
Mimi ni mwana mpendwa wa Mungu na Yeye anayo kazi ya kufanywa na mimi.
Kwa moyo, uwezo, akili na nguvu zangu zote, nitampenda Mungu, nitashika maagano yangu na kutumia ukuhani Wake ili kuwatumikia wengine, nikianzia nyumbani mwangu mwenyewe.
Ninapojitahidi kuhudumu, kutumia imani, kutubu na kujiboresha kila siku, nitastahili kupokea baraka za hekaluni na furaha ya kudumu ya injili.
Nitajitayarisha kuwa mmisionari mwenye juhudi, mume mwaminifu na baba mwenye upendo kwa kuwa mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo.
Nitasaidia kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya kurudi kwa Mwokozi kwa kuwaalika wote kuja kwa Kristo na kupokea baraka za Upatanisho Wake.
Amri Kumi
Usiwe na miungu mingine ila mimi.
Usijifanyie sanamu yoyote ya kuchonga.
Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako.
Ikumbuke siku ya sabato, uitakase.
Waheshimu baba yako na mama yako.
Usiue.
Usizini.
Usiibe.
Usishuhudie uongo.
Usitamani.
Ona Kutoka 20:3–17.