Vitabu vya Maelekezo na Miito
4.Uongozi na Mabaraza katika Kanisa la Yesu Kristo


“4. Uongozi na Mabaraza katika Kanisa la Yesu Kristo,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2013).

“4. Uongozi na Mabaraza katika Kanisa la Yesu Kristo,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

mkutano wa baraza la kata

4.

Uongozi na Mabaraza katika Kanisa la Yesu Kristo

4.0

Utangulizi

Kama kiongozi katika Kanisa Wewe umeitwa kwa mwongozo wa kiungu kupitia watumishi wa Bwana waliopewa mamlaka. Unayo heshima ya kusaidia katika kazi ya Baba wa Mbinguni ya “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39).

4.2

Kanuni za Uongozi katika Kanisa

Wakati wa huduma Yake duniani, Mwokozi aliweka mfano wa uongozi kwa ajili ya Kanisa Lake. Kiini cha lengo lake kilikuwa kufanya mapenzi ya Baba yake wa Mbinguni na kuwasaidia wengine waelewe na waiishi injili Yake (ona Yohana 5:30; Mosia 15:7).

Tafuta mwongozo wa Bwana ili kukusaidia wewe ujifunze na utimize kazi za wito wako.

4.2.1

Jiandae Kiroho

Yesu alijiandaa Mwenyewe kiroho kwa ajili ya misheni yake ya duniani (ona Luka 4:1–2). Vivyo hivyo wewe pia jiandae kiroho kwa kusogea karibu na Baba wa Mbinguni kupitia sala, kusoma maandiko, na utii kwa amri Zake.

Tafuta ufunuo ili kuelewa mahitaji ya wale unaowaongoza na jinsi ya kutimiza kazi ambayo Mungu amekuita uifanye.

Bwana pia ameahidi kutunuku karama za kiroho kwa wale wanaozitafuta (ona Mafundisho na Maagano 46:8).

4.2.2

Watumikie Watoto wote wa Mungu

Wapende watu unaowahudumia kama Yesu alivyowapenda. Sali “kwa nguvu zote za moyo” ili ujazwe upendo Wake (Moroni 7:48).

Wasaidie watu binafsi waimarishe uongofu wao na waimarishe imani yao katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Wasaidie wajiandae kufanya maagano pale wanapopokea ibada yao inayofuata. Wahimize wayashike maagano yao waliyoyafanya na kushiriki baraka za toba.

4.2.3

Fundisha Injili ya Yesu Kristo

Viongozi wote ni walimu. Jitahidi kufuata mfano wa Mwokozi kama mwalimu (ona sura ya 17; Kufundisha katika Njia ya Mwokozi). Kupitia maneno na vitendo vyako, fundisha mafundisho ya Yesu Kristo na kanuni za injili Yake (ona 3 Nefi 11:32–33; Mafundisho na Maagano 42:12–14).

Fundisha kutoka kwenye maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho (ona Mafundisho na Maagano 52:9).

Kama umeitwa au kupangiwa kuongoza katika mkutano wa Kanisa au shughuli, hakikisha kwamba mafundisho yanaadilisha na ni sahihi kimafundisho (ona Mafundisho na Maagano 50:21–23).

4.2.4

Ongoza katika Haki

Kila afisa kiongozi anahudumu chini ya maelekezo ya mtu anayeshikilia funguo za ukuhani (ona 3.4.1). Muundo huu unatoa utaratibu na mipaka dhahiri ya majukumu na uwajibikaji katika kuifanya kazi ya Bwana.

Afisa kiongozi anaweza kunaibisha kwa mtu mwingine jukumu la muda mfupi la kuongoza.

Kiongozi anayeongoza katika kikundi cha Kanisa, mkutano au shughuli anahakikisha kwamba madhumuni ya Bwana yamekamilishwa. Kwa kufanya hivi, kiongozi anafuata kanuni za injili, sera za Kanisa, na maelekezo ya Roho Mtakatifu.

Wito au kazi ya kuongoza haimfanyi mtu anayeupokea wito huo kuwa wa muhimu zaidi au mwenye thamanii kuliko wengine.(ona Mafundisho na Maagano 84:109–10).

Siyo sahihi kutamani kuongoza katika kikundi chochote katika Kanisa la Bwana (ona Mafundisho na Maagano 121:34–37).

4.2.5

Naibisha Madaraka na Hakikisha Uwajibikaji

Mwokozi aliwapa wafuasi Wake kazi zilizokuwa za maana na majukumu (ona Luka 10:1). Pia aliwapa fursa ya uwajibikaji kwa ajili ya kazi waliyopewa kuifanya (Ona Luka 9:10).

Kama kiongozi, unaweza kuwasaidia wengine kukua kwa kukabidhi kwa muda kazi zako kwao . Jitahidi kushirikisha waumini wote katika kufanya kazi ya Mungu.

Kukaimisha majukumu kutafanya pia huduma yako iwe na tija zaidi. Tafuta mwongozo wa Roho kuhusu jukumu gani la kunaibisha ili uweze kufokasi kwenye vipaumbele vyako vya juu.

4.2.6

Waandae Wengine kuwa Viongozi na Walimu

Unapofikiria nani angeweza kuhudumu katika miito au majukumu ya Kanisa, kuwa mwenye kusali. Kumbuka kwamba Bwana atawastahilisha wale Anaowaita. Kile ambacho ni muhimu sana ni kwamba wapo tayari kuhudumu, watatafuta kwa unyenyekevu msaada wa Mungu, na wanajitahidi kuwa wenye kustahili.

4.2.7

Panga Mikutano, Masomo, na Shughuli zenye Malengo Dhahiri

Tafuta mwongozo wa Roho katika kupanga mikutano, masomo, na shughuli zenye malengo dhahiri. Malengo haya yanapaswa kuwaimarisha watu binafsi na familia, kuwaleta karibu na Kristo, na kusaidia kukamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa (ona sura za 1 na 2).

4.2.8

Kutathmini Juhudi Zako

Mara kwa mara rejelea majukumu yako na ukuaji wako wa kiroho kama kiongozi. Fikiria pia ukuaji wa wale unaowaongoza.

Mafanikio yako kama kiongozi yanapimwa kimsingi na dhamira yako ya kuwasaida watoto wa Mungu kuwa wafuasi waaminifu wa Yesu Kristo. Unaweza kujua kwamba Bwana anapendezwa na juhudi zako unapohisi Roho akifanya kazi kupitia wewe.

4.3

Mabaraza katika Kanisa

Bwana amewaelekeza viongozi wa Kanisa Lake kushauriana pamoja katika kuifanya kazi Yake (ona Mafundisho na Maagano 41:2-3). Mabaraza yanatoa fursa kwa ajili wajumbe wa baraza kupokea ufunuo wanapotafuta kuelewa mahitaji ya watoto wa Mungu na kupanga jinsi gani ya kusaidia kuyatimiza.

4.4

Kanuni za Mabaraza yenye Tija

4.4.1

Madhumuni ya Mabaraza

Mabaraza yanatoa mkazo maalumu ili kuwasaidia waumini wapokee ibada na kushika maagano yanayohusiana na ibada hizo.

4.4.2

Matayarisho kwa ajili ya Mikutano ya Baraza

Urais na Mabaraza yanatarajiwa kukutana mara kwa mara. Viongozi hawa wanatafuta mwongozo wa Bwana katika kupanga mikutano ya baraza. Pia wanatafuta michango ya mawazo kutoka kwa wajumbe wa baraza katika kuamua nini cha kujadili.

Viongozi wanawaruhusu wajumbe wa baraza wajue mada kabla kwa ajili ya majadiliano. Wajumbe wa baraza wanajiandaa kushiriki utambuzi kuhusu mada hizi.

4.4.3

Majadiliano na Maamuzi

Wakati wa mkutano wa baraza, kiongozi (au mtu ambaye kiongozi amempangia) anaelezea mada iliyo mezani. Kiongozi kisha anahimiza majadiliano miongoni mwa wajumbe wote wa baraza, akiwauliza maswali na kutafuta mawazo.

Wajumbe wanashiriki mapendekezo na kusikilizana kwa heshima. Wanapotafuta kujua mapenzi ya Bwana, roho wa mwongozo wa kiungu na umoja anaweza kushinda.

Katika baraza linalojumuisha wanawake na wanaume, kiongozi anatafuta kupata umaizi na mawazo kutoka kwa jinsia zote mbili. Wanawake na wanaume mara nyingi wana mitazamo tofauti ambayo inatoa uwiano unaotakiwa.

Kiongozi anatoa mwongozo wa majadiliano ya baraza. Hata hivyo, yeye anapaswa kusikiliza zaidi kuliko kuzungumza.

Baada ya majadiliano, kiongozi anaweza ama kuamua hatua ya kuchukua au kuahirisha uamuzi wakati akitafuta taarifa na mwongozo wa ziada.

4.4.4

Umoja

Wajumbe wa baraza wanatafuta kuwa wamoja katika matamanio na kusudi pamoja na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Wanajitahidi kuwa na umoja katika majadiliano na maamuzi yao.

4.4.5

Hatua na Uwajibikaji

Wajumbe wa baraza wanafanya kiasi kikubwa cha kazi yao kabla na baada ya mikutano ya baraza. Wakati wa mikutano, wanatafuta mwongozo wa kiungu katika kutengeneza mipango ili kutekeleza maamuzi. Kiongozi wa baraza anawaalika wajumbe kukamilisha kazi zinazohusiana na mipango hii.

Wajumbe wa baraza wanatoa ripoti juu ya kazi zao. Maendeleo kwa kawaida yanahitaji usikivu unaokubalika na ufuatiliaji wa majukumu hayo.

4.4.6

Usiri

Viongozi wanatumia busara wakati wanaposhiriki taarifa binafsi kwa baraza. Kwa kawaida wanatafuta ruhusa ya mjumbe husika ili kushiriki taarifa hii.

Wajumbe wa baraza hawapaswi kushiriki taarifa binafsi nje ya baraza isipokuwa iwe inahitajika kukamilisha kazi kutoka kwa kiongozi wa baraza.

Baadhi ya mada ni nyeti mno kuzileta mbele ya baraza zima.