Vitabu vya Maelekezo na Miito
36. Kutengeneza, Kubadili, na Kutoa Majina ya Vitengo Vipya


“36. Kutengeneza, Kubadili, na Kutoa Majina ya Vitengo Vipya,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“36. Kutengeneza,Kubadili,na Kutoa Majina ya Vitengo Vipya,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Mwanamume akizungumza katika mkutano wa sakramenti

36.

Kutengeneza, Kubadili, na Kutoa Majina ya Vitengo Vipya

36.0

Utangulizi

Waumini wa Kanisa wanakuwa sehemu ya kusanyiko kulingana na mahali wanapoishi (ona Mosia 25:17–24.). Mikusanyiko hii ni muhimu kwa ajili ya kupanga na kufanya kazi ya Kanisa chini ya mamlaka sahihi ya ukuhani.

Mikusanyiko ya Kanisa (pia inaitwa vitengo) ikijumuisha vigingi, wilaya, kata, na matawi. Vinatengenezwa, kubadilishwa, au kuachwa, tu kama inavyohitajika.

Viongozi wanafanya kazi kuongeza uimara wa kiroho wa waumini kabla ya kupendekeza kutengeneza kitengo kipya au kubadili mipaka ya kitengo. Vitengo vipya vinapaswa kutengenezwa tu pale ambapo vitengo vilivyopo ni imara vya kutosha.

Kwa ajili ya msaada nchini Marekani na Kanada, piga 1-801-240-1007. Nje ya Marekani na Kanada, piga simu kwenye ofisi ya eneo.