Vitabu vya Maelekezo na Miito
16. Kuishi Injili ya Yesu Kristo


“Kuishi Injili ya Yesu Kristo,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2013).

“Kuishi Injili ya Yesu Kristo,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

wanandoa wakisali

16.

Kuishi Injili ya Yesu Kristo

Kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa inafokasi kwenye majukumu matakatifu manne yaliyowekwa (ona 1.2). La kwanza kati ya haya ni kuishi Injili ya Yesu Kristo. Tunaishi injili wakati:

  • Tunapoonesha imani katika Yesu Kristo.

  • Tunapotubu kila siku.

  • Tunapofanya maagano na Mungu wakati tunapopokea ibada za wokovu na kuinuliwa

  • Tunapovumilia hadi mwisho kwa kuyashika maagano hayo.

Kuishi injili kunajumuisha vipengele vingine vya kazi ya wokovu na kuinuliwa.