Vitabu vya Maelekezo na Miito
10. Akidi za Ukuhani wa Haruni


“10. Akidi za Ukuhani wa Haruni,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“10. Akidi za Ukuhani wa Haruni,“ Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
wavulana ndani ya Kanisa

10.

Akidi za Ukuhani wa Haruni

10.1

Dhumuni na Muundo

10.1.1

Dhumuni

Dhumuni la akidi ni kuwasaidia wanaoshikilia ukuhani kufanya kazi kwa pamoja ili kukamilisha kazi ya wokovu na kuinuliwa.

10.1.2

Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni

“Mimi ni mwana mpendwa wa Mungu na Yeye anayo kazi ya kufanywa na mimi.

“Kwa moyo wangu wote, uwezo, akili na nguvu zangu zote, nitampenda Mungu, nitashika maagano yangu na kutumia ukuhani Wake ili kuwatumikia wengine, nikianzia nyumbani kwangu mwenyewe.

“Ninapojitahidi kuhudumu, kutumia imani, kutubu na kujiboresha kila siku, nitastahili kupokea baraka za hekaluni na furaha ya kudumu ya injili.

“Nitajitayarisha kuwa mmisionari mwenye juhudi, mume mwaminifu na baba mwenye upendo kwa kuwa mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo.

“Nitasaidia kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya kurudi kwa Mwokozi kwa kuwaalika wote kuja kwa Kristo na kupokea baraka za Upatanisho Wake.”

10.1.3

Akidi

10.1.3.1

Akidi ya Mashemasi

Vijana wanaijunga na akidi ya mashemasi kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 12. Wakati huu wao pia wanastahili kutawazwa kuwa mashemasi kama wamejiandaa na wanastahili.

Kazi za shemasi zimeelezwa kwenye Mafundisho na Maagano 20:57–59; 84:111. Kazi zingine ni pamoja na kupitisha sakramenti na kumsaidia askofu katika “kusimamia mambo yote ya kimwili” (Mafundisho na Maagano 107:68).

10.1.3.2

Akidi ya Walimu

Vijana wanaijunga na akidi ya walimu kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha umri wa miaka 14. Wakati huu wao pia wanastahili kutawazwa kuwa walimu kama wamejiandaa na wanastahili.

Walimu wana kazi zile zile kama za mashemasi. Pia wanatayarisha sakramenti na kuhudumu kama akina kaka wahudumiaji. Kazi za ziada zimeainishwa katika Mafundisho na Maagano 20:53–59; 84:111.

10.1.3.3

Akidi ya Makuhani

Vijana wanaijunga na akidi ya makuhani kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 16. Wakati huu wao pia wanastahili kutawazwa kuwa makuhani kama wamejiandaa na wanastahili.

Makuhani wana kazi zile zile kama za mashemasi na walimu. Kazi za ziada zimeainishwa katika Mafundisho na Maagano 20:46–52 73–79.

10.1.4

Funguo za Ukuhani

Kwa maelezo kuhusu funguo hizi, ona 3.4.1

10.1.5

Kurekebisha Akidi Kulingana na Mahitaji ya Mahali Husika

Katika kata au tawi lenye wavulana wachache, akidi za Ukuhani wa Haruni zinaweza kukutana pamoja kwa ajili ya masomo na shughuli.

10.2

Kushiriki katika Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa

10.2.1

Kuishi Injili ya Yesu Kristo

10.2.1.2

Kujifunza Injili

Mikutano ya Akidi inafanyika katika Jumapili ya pili na ya nne ya mwezi. Inadumu kwa dakika 50. Mshiriki wa urais wa akidi (au mmoja wa wasaidizi wa askofu katika akidi ya makuhani) anaendesha. Anaongoza akidi katika kukariri dhima na kushauriana pamoja kuhusu kazi, majukumu, na mambo mengine.

Mshiriki wa akidi au kiongozi mtu mzima kisha anaongoza masomo ya injili.

10.2.1.3

Huduma na Shughuli

Huduma na shughuli zinapaswa kujenga shuhuda, kuimarisha familia, kukuza umoja wa akidi, na kutoa fursa za kuwabariki wengine.

Baadhi ya huduma na shughuli zinapaswa kujumuisha wote wavulana na wasichana, hususani kwa ajili ya vijana wakubwa.

Shughuli za Mwaka. Kwa nyongeza kwenye shughuli za kawaida za vijana, wavulana wanaweza pia kushiriki katika yafuatayo kila mwaka:

  • Kambi ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni (ona Mwongozo wa Kambi ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni.).

  • Mkutano wa vijana wa kata au kigingi au Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana (KNV).

10.2.1.4

Maendeleo Binafsi

Katika juhudi zao za kuwa zaidi kama Mwokozi, Vijana wanaalikwa kuweka malengo ili kukua kiroho, kijamii, kimwili na kiakili (ona Luka 2:52).

Kwa maelezo zaidi, ona ChildrenandYouth.ChurchofJesusChrist.org.

10.2.2

Kuwajali Wale Wenye Mahitaji

Wenye ukuhani wa Haruni wanamsaidia askofu katika “kusimamia mambo yote ya kimwili” (Mafundisho na Maagano 107:68). Wanapaswa kuwa na fursa za mara kwa mara za kuwahudumia wengine ndani ya familia na pamoja na familia zao, wakati wa shughuli za vijana, na wakiwa wao wenyewe.

10.2.2.1

Uhudumiaji

Wenye ukuhani wa Haruni wanapokea majukumu ya kuhudumu kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 14. Kwa maelezo zaidi, ona sura ya 21.

10.2.3

Kuwaalika Wote Waipokee Injili

Wenye ukuhani wa Haruni wana kazi ya “kuwakaribisha wote kuja kwa Kristo” (Mafundisho na Maagano 20:59).

Wazazi na viongozi wawahimize wavulana kujiandaa kuhudumu umisionari na kushiriki injili maisha yao yote.

10.2.4

Kuziunganisha Familia Milele

Wenye ukuhani wa Haruni wanaweza kusaidia kuziungasha familia milele katika njia nyingi.

  • Kuheshimu wazazi wao na kuweka mfano wa kuishi kama Kristo katika nyumba zao.

  • Kujiandaa kupokea ibada za hekaluni, pamoja na ndoa ya milele.

  • Kuwatambua mababu ambao wanahitaji ibada za hekaluni (ona FamilySearch.org).

  • Kushiriki katika ubatizo na kuthibitishwa kwa niaba ya wafu mara nyingi kadiri hali zitakavyoruhusu.

10.3

Uaskofu

Wajibu wa kwanza kwa umuhimu kwa askofu ni kuwatunza wavulana na wasichana katika kata yake. Anajifunza majina yao na kuelewa hali ya nyumbani kwao. Anahudhuria shughuli zao na mikutano yao ya Jumapili mara kwa mara.

Askofu ni rais wa akidi ya makuhani.

Mshauri wa kwanza katika uaskofu anawajibika kwa ajili ya akidi ya walimu. Mshauri wa pili anawajibika kwa ajili ya akidi ya mashemasi.

Uaskofu una majukumu ya ziada yafuatayo kwa ajili ya akidi za Ukuhani wa Haruni:

  • Kukutana na kila mvulana angalau mara mbili kwa mwaka ona 31.3.1).

  • Kuwasaidia wavulana wajiandae kupokea Ukuhani wa Melkizedeki.

  • Kusimamia kumbukumbu, ripoti, na fedha za Ukuhani wa Haruni.

Washauri wa Akidi na wataalamu wanasaidia katika majukumu haya kama watakavyoombwa.

10.4

Viongozi wa Akidi ya Vijana

10.4.1

Wito, Kukubaliwa, na Kusimikwa

Askofu anamwita kuhani mmoja au wawili kuwa wasaidizi wake katika kuongoza akidi ya makuhani.

Mshiriki wa uaskofu anawaita marais wa akidi ya mashemasi na walimu. Wakati kuna wenye ukuhani wa Haruni wa kutosha kuhudumu, wavulana hawa kwa sala wanawafikiria washiriki wa akidi ili kuwapendekeza kama washauri na katibu.

Baada ya kutoa miito hii, mshiriki wa uskofu anawatambulisha rasmi viongozi wa Akidi ya vijana kwa ajili ya kura ya kuwakubali katika mkutano wao wa akidi. Askofu anawasimika wasaidizi wake na marais wa akidi za mashemasi, na walimu. Anatunukia funguo za ukuhani juu ya marais wa akidi. Anaweza kuwapangia washauri wake kuwasimika washauri wengine wa urais na makatibu.

10.4.2

Majukumu:

  • Kuongoza juhudi za akidi kushiriki katika kazi ya wokovu na kuinuliwa (ona sura ya 1).

  • Kumjua na kumhudumia kila mshiriki wa akidi, ikijumuisha wale ambao hawahudhurii mikutano ya akidi.

  • Kuhudumu kwenye baraza la vijana la kata (ona 10.4.4).

  • Kuafundishe washiriki wa akidi kazi zao za ukuhani (ona Mafundisho na Maagano 107: 85–88).

  • Kupanga na kuendesha mikutano ya akidi (ona 10.2.1.2).

  • Kupanga na kutekeleza huduma na shughuli za akidi (ona 10.2.1.3).

10.4.3

Mkutano wa Urais wa Akidi

Urais wa akidi za Ukuhani wa Haruni hukutana mara kwa mara. Rais wa akidi huendesha mikutano hii. Angalau watu wazima wawili wanahudhuria—mshiriki wa uaskofu na mshauri, au mtaalamu.

10.4.4

Baraza la Vijana la Kata

Ona 29.2.6 kwa ajili ya maelezo zaidi kuhusu baraza la vijana la kata.

10.8

Miongozo ya Ziada na Sera

10.8.1

Kuwalinda Vijana

Wakati watu wazima wanapochangamana na vijana katika mipangilo ya Kanisa, angalau watu wazima wawili wanaoweza kuwajibika wanapaswa kuwepo.

Watu wazima wote wanaofanya kazi na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya ulinzi wa watoto na vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org).

Chapisha