“11. Wasichana,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).
“11. Wasichana,“ Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla
11.
Wasichana
11.1
Dhumuni na Muundo
11.1.1
Dhumuni
Kikundi cha Wasichana kinawasaidia wasichana wafanye na washike maagano matakatifu na kuzidisha uongofu wao kwa Yesu Kristo na injili Yake.
11.1.2
Dhima ya Wasichana
“Mimi ni binti mpendwa wa wazazi wa Mbinguni, mwenye asili takatifu na hatima ya milele.
“Kama mfuasi wa Yesu Kristo, ninajitahidi kuwa kama Yeye. Ninatafuta na kufanyia kazi ufunuo binafsi na kuwahudumia wengine katika jina Lake takatifu.
“Nitasimama kama shahidi wa Mungu nyakati zote na katika vitu vyote na katika mahali popote.
“Ninapojitahidi kuwa mwenye kustahili kuinuliwa, ninathamini zawadi ya toba na kutafuta kuwa bora kila siku. Kwa imani, nitaimarisha nyumba yangu na familia yangu, kufanya na kushika maagano matakatifu, na kupokea ibada na baraka za hekalu takatifu.”
11.1.3
Madarasa
Wasichana wanakuwa washiriki wa darasa la wasichana kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 12.
Uaskofu na viongozi watu wazima wa Wasichana kwa sala wanaamua jinsi ya kupanga madarasa kulingana na umri. Kila darasa, bila kujali ukubwa, linapaswa kuwa na rais na, pale inapowezekana, mshauri mmoja au wawili na katibu.
11.2
Kushiriki katika Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa
11.2.1
Kuishi Injili ya Yesu Kristo
11.2.1.2
Kujifunza Injili
Mikutano ya darasa inafanyika katika Jumapili ya pili na ya nne ya mwezi. Inadumu kwa dakika 50. Mshiriki wa urais wa darasa anaendesha. Anaongoza darasa katika kukariri dhima na kushauriana pamoja kuhusu majukumu, na mambo mengine.
Mshiriki wa darasa au kiongozi mtu mzima kisha anaongoza mafundisho ya injili.
11.2.1.3
Huduma na Shughuli
Huduma na shughuli zinapaswa kujenga shuhuda, kuimarisha familia, kukuza umoja wa darasa na kutoa fursa za kuwabariki wengine.
Baadhi ya huduma na shughuli zinapaswa kujumuisha wote wavulana na wasichana, hususani kwa vijana wakubwa.
Shughuli za Mwaka. Kwa nyongeza kwenye shughuli za kawaida za vijana, wasichana wanaweza pia kushiriki katika yafuatayo kila mwaka:
-
Kambi ya wasichana (ona Mwongozo wa Kambi kwa Wasichana).
-
Mkutano wa vijana wa kata au kigingi au mkutano wa Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana (KNV).
11.2.1.4
Maendeleo Binafsi
Katika juhudi zao za kuwa zaidi kama Mwokozi, Vijana wanaalikwa kuweka malengo ili kukua kiroho, kijamii, kimwili na kiakili (ona Luka 2:52).
Kwa maelezo zaidi, ona ChildrenandYouth.ChurchofJesusChrist.org.
11.2.2
Kuwajali Wale Wenye Mahitaji.
Wasichana wanapaswa kuwa na fursa za mara kwa mara za kuwahudumia wengine katika familia, na pamoja na familia zao, wakati wa shughuli za vijana, na wakiwa wao wenyewe.
11.2.2.1
Uhudumiaji
Wasichana wanaweza kupokea majukumu ya uhudumiaji waliyopangiwa kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 14. Kwa maelezo zaidi, ona sura ya 21.
11.2.3
Kuwaalika Wote Waipokee Injili
Wasichana wanawaalika wote waipokee injili pale “wanaposimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote, na katika vitu vyote, na katika mahali popote” (Mosia 18:9).
Wazazi na viongozi wanaweza kuwasaidia wasichana wajiandae kushiriki injili maisha yao yote.
11.2.4
Kuziunganisha Familia Milele
Wasichana wanaweza kusadia kuziunganisha familia kwa ajili ya milele katika njia nyingi.
-
Kuwaheshimu wazazi wao na kwa kuweka mfano wa kuishi kama Kristo katika nyumba zao.
-
Kujiandaa kupokea ibada za hekaluni, ikijumuisha ndoa ya milele.
-
Kuwatambua mababu ambao wanahitaji ibada za hekaluni (ona FamilySearch.org).
-
Kushiriki katika ubatizo na kuthibitishwa kwa niaba ya wafu mara nyingi kadiri hali zitakavyoruhusu.
11.3
Uongozi wa Wasichana katika Kata
11.3.1
Uaskofu
Wajibu muhimu zaidi wa askofu ni kuwatunza wasichana na wavulana katika kata yake. Yeye na washauri wake wanajifunza majina yao na kuelewa hali za nyumbani kwao. Wanakutana na kila msichana angalau mara mbili kwa mwaka (ona 31.3.1).
Askofu anawajibika kwa kikundi cha wasichana katika kata. Anakutana mara kwa mara na rais wa wasichana.
Askofu na washauri wake mara kwa mara wanashiriki kwenye mikutano, huduma na shughuli za Wasichana.
11.3.2
Urais wa Wasichana wa Watu Wazima
Askofu anamwita na kumsimika mwanamke mtu mzima kuhudumu kama rais wa Wasichana katika kata. Kama kitengo ni kikubwa vya kutosha, anapendekeza kwake mwanamke mmoja au wawili kuitwa kama washauri wake (ona sura ya 30).
Katika kitengo kidogo, rais wa wasichana anaweza kuwa kiongozi mtu mzima mmoja pekee aliyeitwa katika kikundi cha Wasichana. Katika hali hii, anafanya kazi na wazazi kuandaa maelekezo na shughuli kwa ajili ya wasichana.
Kama tawi halina rais wa Wasichana, rais wa Muungano wa Usaidizi anaweza kuandaa maelekezo kwa ajili ya wasichana mpaka rais wa Wasichana atakapokuwa ameitwa.
Rais wa Wasichana ana majukumu yafuatayo. Washauri wake wanamsaidia.
-
Kuhudumu kwenye baraza la kata.
-
Anahudumu kama mshiriki wa baraza la Vijana la kata (ona 29.2.6).
-
Anamhudumia kila msichana binafsi.
-
Anawafundisha viongozi wengine wa Wasichana na marais wa madarasa juu ya wajibu wao.
-
Anashauriana na wasichana kuhusu changamoto ambazo hazimhitaji askofu au hazihusiani na udhalilishaji (ona 32,3, 31.3.1, na 38.6.2).
11.3.4
Uraisi wa Darasa na Katibu
11.3.4.1
Wito, Kukubaliwa, na Kusimikwa
Kila darasa la Wasichana linapaswa kuwa na urais wa darasa.
Mshiriki wa uaskofu anamwita msichana kuhudumu kama rais wa darasa Wakati kunapokuwa na wasichana wa kutosha kuhudumu, kwa sala msichana anawafikiria washiriki wa darasa ili kuwapendekeza kama washauri na katibu.
Baada ya kutoa miito hii, mshiriki wa uaskofu anawawasilisha wasichana hao mbele ya darasa lao kwa ajili ya kura ya kukubaliwa. Askofu au mshauri aliyepangiwa anawasimika wasichana hao.
11.3.4.2
Majukumu
Marais wa darasa wanahudumu kwenye baraza la Vijana la kata (ona 10.3.4.4). Urais wa darasa pia wana majukumu yafuatayo:
-
Kuongoza juhudi za darasa za kushiriki katika kazi ya wokovu na kuinuliwa (ona sura ya 1).
-
Kupata kumjua na kumhudumia kila msichana, ikijumuisha wale ambao hawahudhurii mikutano ya darasa.
-
Kupanga na kuendesha mikutano ya darasa ya Jumapili (ona 11.2.1.2).
-
Kupanga na kutekeleza huduma na shughuli za darasa (ona 11.2.1.3).
11.3.4.3
Mkutano wa Urais wa Darasa
Urais wa darasa la Wasichana hukutana mara kwa mara. Rais wa darasa huendesha mikutano hii. Viongozi wanawake watu wazima waliopangiwa kusaidia urais wa darasa pia wanahudhuria.
11.3.4.4
Baraza la Vijana katika Kata
Ona 29.2.6 kwa ajili ya maelezo zaidi kuhusu baraza la vijana la kata.
11.6
Miongozo ya Ziada na Sera
11.6.1
Kuwalinda Vijana
Wakati watu wazima wanapochangamana na vijana katika mipangilo ya Kanisa, angalau watu wazima wawili wanaoweza kuwajibika wanapaswa kuwepo. Inaweza kuwa ya lazima kuunganisha madarasa ili kufanya hii iwezekane.
Watu wazima wote wanaofanya kazi na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya ulinzi wa watoto na vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org).