“18. Kufanya Ibada za Ukuhani na Baraka,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).
“18. Kufanya Ibada za Ukuhani na Baraka,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla
18.
Kufanya Ibada za Ukuhani na Baraka
18.0
Utangulizi
Ibada na baraka ni vitendo vitakatifu vinavyofanywa kwa mamlaka ya ukuhani na katika jina la Yesu Kristo. Ibada za ukuhani na baraka zinatoa njia ya kufikia nguvu za Mungu (ona Mafundisho na Maagano 84:20).
Ibada na baraka zinapaswa kufanyika kwa imani kwa Baba wa mbinguni na Yesu Kristo na kulingana na mwongozo wa Roho Mtakatifu. Viongozi wanahakikisha kwamba ibada na baraka hufanywa kwa kibali sahihi (pale inapolazimu), kwa mamlaka yanayohitajika ya ukuhani, katika njia sahihi na wanaoshiriki wawe wenye kustahili (ona 18.3).
18.1
Ibada za Wokovu na Kuinuliwa
Ukuhani unajumuisha mamlaka ya kusimamia ibada za injili ambazo ni muhimu kwa ajili ya wokovu na kuinuliwa. Watu wanafanya maagano matakatifu na Mungu wakati wanapopokea ibada hizi. Ibada za wokovu na kuinuliwa zimeorodheshwa hapa chini:
-
Ubatizo
-
Uthibitisho na kipawa cha Roho Mtakatifu
-
Utunukiaji wa Ukuhani wa Melkizedeki na utawazo kwenye ofisi (kwa wanaume)
-
Endaumenti ya hekaluni
-
kuunganishwa hekaluni
Kama mtoto ambaye alizaliwa katika agano na akafa kabla ya umri wa miaka 8 hakuna ibada zinazohitajika au zinazofanywa. Kama mtoto hakuzaliwa katika agano, ibada pekee anayohitaji ni kuunganishwa na wazazi. Kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi, watoto wote ambao wanakufa kabla ya umri wa miaka 8 “wanaokolewa katika ufalme wa selestia wa mbinguni” (Mafundisho na Maagano 137:10; ona pia Moroni 8:8–12).
18.3
Kushiriki katika Ibada au Kubariki
Wale wanaofanya au kushiriki katika ibada au kubariki lazima wawe na mamlaka muhimu ya ukuhani na wawe wenye kustahili. Kiujumla, kiwango cha ustahili ni kile kinachohusiana na kuwa na kibali cha hekaluni. Hata hivyo, kwa kuongozwa na Roho na maelekezo katika sura hii, maaskofu na marais wa vigingi wanaweza kuwaruhusu akina baba na waume wanaoshikilia ofisi husika za ukuhani kufanya au kushiriki kwenye baadhi ya ibada na baraka hata kama wao sio wenye kustahili kikamilifu kuingia hekaluni. Anayeshikilia ukuhani ambaye ana dhambi kubwa yenye kuhitaji toba hapaswi kushiriki.
Kufanya au kupokea baadhi ya ibada na baraka kunahitaji kibali kutoka kwa kiongozi anayesimamia anayeshikilia funguo husika za ukuhani (ona 3.4.1). Kama itakavyohitajika, kibali kinaweza kutolewa na mshauri aliyeruhusiwa na kiongozi anayesimamia. Ona chati zifuatazo. Marejeleo kwa marais wa vigingi hutumika pia kwa marais wa misheni. Marejeleo kwa maaskofu hutumika pia kwa marais wa matawi.
Viongozi Gani Wanashikilia Funguo za Kutoa Kibali cha Kufanya au Kupokea Ibada za Wokovu na Kuinuliwa?
Ibada |
Nani anayeshikilia Funguo |
---|---|
Ibada Ubatizo | Nani anayeshikilia Funguo Askofu (kwa ajili ya watoto wa miaka 8 na kwa ajili ya watoto ambao wazazi wao au mmoja wa wazazi ni muumini wa Kanisa ambao wamefikisha miaka 9 na zaidi ambao ubatizo wao ulicheleweshwa kwa sababu ya ulemavu wa akili) Rais wa misheni (kwa ajili ya waongofu) |
Ibada Uthibitisho na kipawa cha Roho Mtakatifu | Nani anayeshikilia Funguo Askofu (kwa ajili ya watoto wa miaka 8 na kwa ajili ya watoto ambao wazazi wao au mmoja wa wazazi ni muumini wa Kanisa ambao wamefikisha miaka 9 na zaidi ambao ubatizo wao ulicheleweshwa kwa sababu ya ulemavu wa akili) Rais wa misheni (kwa ajili ya waongofu) |
Ibada Utunukiaji wa Ukuhani wa Melkizedeki na utawazo kwenye ofisi (kwa wanaume) | Nani anayeshikilia Funguo Rais wa kigingi |
Ibada Endaumenti ya hekaluni | Nani anayeshikilia Funguo Askofu na rais wa kigingi |
Ibada kuunganishwa hekaluni | Nani anayeshikilia Funguo Askofu na rais wa kigingi |
Viongozi gani Wanashikilia funguo za kutoa kibali cha Kufanya au Kupokea Ibada Zingine na Baraka?
Ibada na Baraka |
Nani anayeshikilia Funguo |
---|---|
Ibada na Baraka Kuwapa Majina na Kuwabariki Watoto | Nani anayeshikilia Funguo Askofu |
Ibada na Baraka Sakramenti | Nani anayeshikilia Funguo Askofu |
Ibada na Baraka Utunukiaji wa Ukuhani wa Haruni na utawazo kwenye ofisi (kwa ajili wavulana na wanaume) | Nani anayeshikilia Funguo Askofu |
Ibada na Baraka Kusimikwa kwa waumini ili kuhudumu kwenye miito | Nani anayeshikilia Funguo Ona 30.8 |
Ibada na Baraka Kuweka Wakfu Mafuta | Nani anayeshikilia Funguo Kibali hakihitajiki |
Ibada na Baraka Kuwahudumia Wagonjwa | Nani anayeshikilia Funguo Kibali hakihitajiki |
Ibada na Baraka Baraka za faraja na ushauri, ikijumuisha baraka za baba | Nani anayeshikilia Funguo Kibali hakihitajiki |
Ibada na Baraka Kuweka wakfu nyumba | Nani anayeshikilia Funguo Kibali hakihitajiki |
Ibada na Baraka Kuweka wakfu makaburi | Nani anayeshikilia Funguo Kiongozi wa ukuhani anayesimamia huduma |
Ibada na Baraka Baraka za patriaki | Nani anayeshikilia Funguo Askofu |
18.4
Ibada kwa ajili ya Watoto Chini ya Umri wa Miaka 18
Mtoto chini ya miaka 18 anaweza tu kubarikiwa, kubatizwa, kuthibitishwa, kutawazwa kwenye ofisi ya ukuhani au kusimikwa kwenye wito kwa kibali cha (1)wazazi walio na haki kisheria kushiriki katika uamuzi au (2) walezi kisheria.
18.6
Kuwapa Majina na Kuwabariki Watoto
Watoto kwa kawaida wanapewa majina na kubarikiwa wakati wa mkutano wa mfungo na ushuhuda kwenye kata ambapo wazazi wao wanaishi.
18.6.1
Nani Anatoa Baraka
Ibada ya kutoa jina na kubariki mtoto inafanywa na wenye ukuhani wa Melkizedeki, kama ilivyo katika Mafundisho na Maagano 20:70.
Mtu au familia inayotamani kwamba mtoto apokee jina na baraka anaratibu ibada hiyo na askofu. Askofu anashikilia funguo za ukuhani kwa ajili ya kutoa majina na kuwabariki watoto katika kata.
Askofu anaweza kumruhusu baba anayeshikilia ukuhani wa Melkizedeki kumpa jina na kumbariki mtoto wake hata kama baba hastahili kikamilifu kwa ajili ya kuingia hekaluni (ona 18.3). Maaskofu wanawahimiza akina baba wajiandae wenyewe kuwabariki watoto wao.
18.6.2
Maelekezo
Chini ya maelekezo ya uaskofu, wanaoshikilia ukuhani wa Melkizedeki hukusanyika katika mduara kumpa jina na kumbariki mtoto. Wanaweka mikono yao chini ya mtoto, au wanaweka mikono yao kwa wepesi juu ya kichwa cha mtoto ambaye ni mkubwa. Kisha yule anayezungumza:
-
Anamwita Baba wa Mbinguni kama ilivyo katika sala.
-
Anasema kwamba baraka inafanywa kwa mamlaka ya Ukuhani wa Melkizedeki.
-
Anampa mtoto jina.
-
Anamwita mtoto.
-
Anatoa baraka kwa mtoto kama atakavyoongozwa na Roho.
-
Anafunga katika jina la Yesu Kristo.
18.6.3
Fomu ya Kumbukumbu ya Mtoto na Cheti cha Baraka
Kabla mtoto hajabatizwa, karani anatumia Leader and Clerk Resources (LCR) kutayarisha Fomu ya Kumbukumbu ya Mtoto Baada ya baraka, anatengeneza kumbukumbu ya uumini katika mfumu huo na kutayarisha Cheti cha Baraka. Cheti hiki kinasainiwa na askofu na kupewa kwa wazazi wa mtoto au walezi.
Jina kwenye kumbukumbu ya uumini na cheti linapaswa kufanana na cheti cha kuzaliwa, usajili wa kuzaliwa wa serikali au jina la kisheria la sasa.
18.7
Ubatizo
Ubatizo kwa kuzamishwa kwenye maji na mtu nwenye mamlaka ni muhimu kwa ajili ya mtu kuwa muumini wa Kanisa na kupokea Roho Mtakatifu. Wote wanaotafuta kuinuliwa lazima wafuate mfano wa Mwokozi, kwa kupokea ibada hizi.
18.7.1
Kibali kwa ajili ya Mtu Kubatizwa na Kuthibitishwa
18.7.1.1
Watoto Ambao Ni Waumini kwa Kumbukumbu
Askofu anashikilia funguo za ukuhani kwa ajili ya kuwabatiza waumini wa kumbukumbu wenye umri wa miaka 8 katika kata. Watoto hawa wanapaswa kubatizwa na kuthibitishwa kwenye siku yao ya kutimiza miaka 8 ya kuzaliwa au punde tu baada ya kutimiza miaka 8 ya kuzaliwa kwao kama inavyofaa (ona Mafundisho na Maagano 68:27)). Hawa ni watoto ambao kumbukumbu za uumini wao wa Kanisa tayari zipo (ona 33.6.2). Wanapofika umri wa miaka 8 askofu anahakikisha wana kila fursa ya kuikubali injili na kubatizwa na kuthibitishwa.
Askofu au mshauri aliyepewa jukumu anawasaili watoto wa kumbukumbu kwa ajili ya ubatizo na uthibitisho. Maelekezo yapo kwenye 31.2.3.1.
Kwa maelezo kuhusu kujaza Kumbukumbu za Ubatizo na Uthibitisho, ona 18.8.3.
18.7.1.2
Waongofu
Rais wa misheni anashikilia funguo za ukuhani kwa ajili ya kuwabatiza waongofu katika misheni. Kwa sababu hii, wamisionari huwasaili waongofu kwa ajili ya ubatizo na uthibitisho.
18.7.2
Huduma za Ubatizo
Huduma ya ubatizo inapaswa kuwa ya kawaida, fupi na ya kuinua kiroho. Inaweza kujumuisha yafuatayo:
-
Muziki kabla ya ibada kuanza
-
Ukaribisho mfupi kutoka kwa kaka anayeendesha huduma
-
Wimbo wa ufunguzi na sala
-
Ujumbe mmoja au jumbe mbili fupi juu ya mada za injili, kama vile ubatizo na kipawa cha Roho Mtakatifu.
-
Chaguzi za nyimbo za kuimba
-
Ubatizo
-
Wakati wa unyenyekevu wakati wale walioshiriki katika ubatizo wakibadilisha nguo (nyimbo za dini au nyimbo za msingi zinaweza kupigwa au kuimbwa wakati huu)
-
Uthibitisho wa waumini wa kumbukumbu wenye miaka 8; uthibitisho wa waongofu kama itaamuliwa na askofu (ona 18.8)
-
Waongofu kutoa ushuhuda, kama inafaa
-
Wimbo wa kufunga na sala
-
Muziki wa baada ya ibada ya ubatizo
Wakati mtoto wa kumbukumbu anapojiandaa kubatizwa, mshiriki wa uaskofu na urais wa msingi wanashauriana na familia kupanga na kuratibu huduma ya ubatizo. Mshiriki wa urais anaendesha huduma. Ikiwa mtoto zaidi ya mmoja watabatizwa katika mwezi mmoja, wanaweza kujumuishwa katika huduma moja ya ubatizo.
Katika kata zenye watoto wengi wa kumbukumbu, watoto kutoka kata mbalimbali wanaweza kushiriki huduma moja ya ubatizo. Mshiriki wa urais wa kigingi au mshauri mkuu aliyepewa jukumu anaendesha huduma.
Ubatizo wa mwanafamilia haupaswi kucheleweshwa mpaka baba aweze kupokea ukuhani na kufanya ubatizo huo.
Chini ya mwongozo wa uaskofu, kiongozi wa misheni wa kata (kama yupo) au mshiriki wa urais wa akidi ya wazee anayeongoza kazi ya umisionari katika kata anapanga na anaendesha huduma ya ubatizo kwa ajili ya waongofu. Wanaratibu zoezi hili pamoja na wamisionari.
18.7.3
Nani Anafanya Ibada
Ibada ya ubatizo inafanywa na kuhani au mwenye Ukuhani wa Melkizedeki. Mtu anayefanya ubatizo lazima apewe kibali na askofu (au na rais wa misheni ikiwa mmisionari anafanya ubatizo).
Askofu anaweza kumruhusu baba ambaye ni kuhani au mwenye Ukuhani wa Melkizedeki ambatize mtoto wake hata kama baba hastahili kikamilifu kwa ajili ya kuingia hekaluni (ona 18.3). Maaskofu huwahimiza akina baba wajiandae wenyewe kuwabatiza watoto wao.
18.7.4
Wapi pa Kufanya Ibada
Ubatizo unapaswa kufanywa katika kisima cha ubatizo kama kinapatikana. Kama hakuna kisima, sehemu salama yenye maji iinaweza kutumika.
Kwa usalama, mtu mzima anayeweza kuwajibika lazima awepo wakati kisima kikijazwa na kubakia mpaka kitapoondolewa maji, kusafishwa na kuwa salama. Kisima kinapaswa kuondolewa maji mara baada ya kila huduma ya ubatizo. Milango ielekeayo kwenye kisima cha ubatizo inapaswa kufungwa wakati kisima kinapokuwa hakitumiki.
18.7.5
Mavazi
Mtu anayebatiza na mtu anayebatizwa wanavaa mavazi meupe ambayo hayaoneshi mwili pale yanapokuwa yameloa. Mtu aliyepata endaumenti anavaa vazi la ubatizo juu ya gamenti ya hekaluni wakati anapofanya ubatizo. Vitengo vya eneo husika hununua nguo za ubatizo kwa pesa za bajeti na hawatozi pesa kwa ajili ya matumizi ya nguo hizi.
18.7.6
Mashahidi
Mashahidi wawili, waliopitishwa na kiongozi anayesimamia, wanaangalia kila ubatizo kuhakikisha kwamba unafanywa vyema. Waumini wa Kanisa waliobatizwa, ikijumuisha watoto na vijana, wanaweza kuhudumu kama mashahidi.
Ubatizo lazima urudiwe kama maneno hayakusemwa sawasawa kama yalivyotolewa katika Mafundisho na Maagano 20:73. Ni lazima pia kurudiwa kama sehemu ya mwili wa yule mtu, nywele au vazi havijazamishwa kabisa majini.
18.7.7
Maelekezo
Ili kufanya ibada ya ubatizo, kuhani au mwenye Ukuhani wa Melkizedeki:
-
Anasimama ndani ya maji na mtu anayebatizwa.
-
Anashika kiganja cha mkono wa kulia cha yule mtu kwa mkono wake wa kushoto (kwa ajili ya wepesi wa kubatiza na usalama). Mtu anayebatizwa anashika kiganja cha mkono wa kushoto cha yule mwenye ukuhani kwa mkono wake wa kushoto.
-
Mwenye ukuhani anainua mkono wake wa kulia juu kwenye pembe mraba.
-
Anatamka jina kamili la mtu yule na kusema, “Kwa mamlaka niliyopewa na Yesu Kristo, ninakubatiza katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina” (Mafundisho na Maagano 20:73).
-
Kisha mtu anayebatizwa anaziba pua yake kwa mkono wa kulia (kwa hali inayofaa); kisha mwenye ukuhani anaweka mkono wake wa kulia kwenye mgongo wa anayebatizwa na kumzamisha kikamilifu, ikijumuisha mavazi.
-
Mwenye ukuhani anamsaidia yule mtu kuja juu ya maji.
18.8
Uthibitisho na Kipawa cha Roho Mtakatifu
Baada ya mtu kubatizwa anathibitishwa kuwa muumini wa Kanisa na kupokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono (ona Mafundisho na Maagano 20:41; Matendo ya mitume 19:1–6). Mtu anakuwa muunini wa Kanisa baada ya ibada hizi mbili kukamilika na kuwekwa kumbukumbu kwa usahihi (ona Yohana 3:5; Mafundisho na Maagano 33:11; 3 Nefi 27:20).
Askofu anasimamia huduma ya uthibitisho. Watoto wenye umri wa miaka minane kwa kawaida huthibitishwa siku wanayobatizwa. Waongofu kwa kawaida huthibitishwa katika mkutano wowote wa sakramenti katika kata wanakoishi, hasa Jumapili baada ya ubatizo wao.
Mshiriki wa uaskofu anafuata miongozo katika 29.2.1.1 wakati wa kuwatambulisha waumini wapya.
18.8.1
Nani Anafanya Ibada
Mwenye kushikilia Ukuhani wa Melkizedeki pekee ambaye anastahili kwa ajili ya kuingia hekaluni anaweza kuwa kama sauti kwa ajili ya uthibitisho. Hata hivyo askofu anaweza kumruhusu baba anayeshikilia ukuhani wa Melkizedeki kusimama katika duara kwa ajili ya uthibitisho wa mtoto wake hata kama baba sio mwenye kustahili kikamilifu kwa ajili ya kuingia hekaluni (ona 18.3).
Angalau mshiriki mmoja wa uaskofu anashiriki katika ibada hii. Ikiwa wamisionari wamemfundisha mwongofu, askofu huwaalika kushiriki.
18.8.2
Maelekezo
Chini ya maelekezo ya uaskofu, mmoja au zaidi ya wenye Ukuhani wa Melkizedeki wanaweza kushiriki katika uthibitisho. Wanaweka mikono yao kwa wepesi juu ya kichwa cha mtu huyo. Kisha yule anayezungumza:
-
Anamwita mtu yule kwa jina lake kamili.
-
Anasema kwamba ibada inafanyika kwa mamlaka ya Ukuhani wa Melkizedeki.
-
Anamthibisha yule mtu kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.
-
Anasema “pokea Roho Mtakatifu” (siyo “pokea kipawa cha Roho Mtakatifu”).
-
Anatoa maneno ya baraka kama atakavyoongozwa na Roho.
-
Anafunga katika jina la Yesu Kristo.
18.8.3
Kumbukumbu ya Ubatizo na Uthibitisho na Cheti
Kabla mtoto ambaye ni muumini wa kumbukumbu hajasailiwa kwa ajili ya ubatizo, karani anatumia (LCR) kutayarisha Fomu ya Ubatizo na Uthibitisho. Askofu au mshauri aliyepewa jukumu anaendesha usaili na anasaini fomu. Baada ya ubatizo na uthibitisho, karani anatumia fomu hii kusasisha kumbukumbu ya uumini wa mtoto katika LCR.
Wakati mmisionari anamsaili mwongofu kwa ajili ya ubatizo, anajaza Kumbukumbu ya Ubatizo na Uthibitisho kwa kutumia aplikesheni ya Kitabu cha Mpango wa Eneo (ABP) app Baada ya ubatizo na Uthibitisho, wamisionari wanaweka kumbukumbu ya taarifa katika ABP na kuituma kielektroniki kwa karani wa kata. Karani wa kata anaipitia upya taarifa katika LCR na kutengeneza kumbukumbu ya uumini.
Baada ya kumbukumbu ya uumini kutengenezwa, karani anatayarisha cheti za Ubatizo na Uthibitisho. Cheti hiki kinasainiwa na askofu na kupewa mtu huyo.
Jina kwenye kumbukumbu ya uumini na cheti linapaswa kufanana na cheti cha kuzaliwa, usajili wa kuzaliwa wa serikali au jina la kisheria la sasa.
18.9
Sakramenti
Waumini wa Kanisa wanakutana siku ya sabato kumwabudu Mungu na kushiriki sakramenti (ona Mafundisho na Maagano 20:75); 59:9; moroni 6:5–6) Wakati wa ibada hii, wanashiriki mkate na maji kukumbuka dhabihu ya Mwokozi ya mwili wake na damu na kuyafanya upya maagano yao matakatifu (ona Mathayo 26:26–28; Tafsiri ya Joseph Smith, Marko 14:20–25; Luka 22:15–20; 3 Nefi 18; Moroni 6:6).
18.9.1
Kibali cha Kuhudumia Sakramenti
Askofu anashikilia funguo za ukuhani kwa ajili ya kuhudumia sakramenti katika kata. Wote wanaoshiriki katika kuandaa, kubariki na kupitisha sakramenti lazima wapate kibali kutoka kwake au mtu fulani chini ya maelekezo yake.
18.9.2
Nani Anafanya Ibada
-
Walimu, makuhani na wenye Ukuhani wa Melkizedeki wanaweza kuiandaa sakramenti.
-
Makuhani na wenye Ukuhani wa Melkizedeki wanaweza kubariki sakramenti.
-
Mashemasi, walimu, makuhani na wenye Ukuhani wa Melkizedeki wanaweza kupitisha sakramenti.
18.9.3
Miongozo kwa ajili ya Sakramenti
Kwa sababu ya utakatifu wa sakramenti, viongozi wa ukuhani wanapaswa kujiandaa kwa makini ili iwe katika mpangilio na unyenyekevu.
Wale wanaohudumia sakramenti wanapaswa kufanya hivyo katika njia ya kutukuza, wakitambua kwamba wanamwakilisha Bwana.
Kupitisha sakramenti kunapaswa kuwa kwa njia ya asili na siyo sana katika kufuata utaratibu rasmi.
Ingawa sakramenti ni kwa ajili ya waumini wa Kanisa, hakuna kinachopaswa kufanywa kuwazuia wengine wasishiriki.
18.9.4
Maelekezo
-
Wale wanaoandaa, kubariki au kupitisha sakramenti kwanza waoshe mikono yao kwa sabuni au vifaa vingine vya kusafishia mikono.
-
Walimu, makuhani, au wenye Ukuhani wa Melkizedeki wanahakikisha kwamba trei zenye mkate ambao haujamegwa, trei za maji na vikombe vya maji safi, vitambaa safi vya mezani viko mahala pake kabla ya mkutano.
-
Wakati waumini wa kata wanaimba wimbo wa sakramenti, wale ambao watabariki sakramenti kwa unyenyekevu wanasimama, wanatoa kitambaa kinachofunika trei za mikate, na kumega mkate katika vipande vidogo vidogo.
-
Baada ya wimbo mtu anayebariki anapiga magoti na anasema sala ya Sakramenti kwa ajili ya mkate (ona Mafundisho na Maagano 20:77).
-
Askofu anahakikisha sala za sakramenti zinatamkwa kwa uwazi, usahihi na kwa heshima. Kama mtu fulani anafanya makosa katika maneno na anajisahihisha mwenyewe hakuna masahihisho zaidi yanayohitajika. Kama mtu hasahihishi kosa lake, askofu kwa upole anamwomba arudie sala sala.
-
Baada ya sala, wenye ukuhani kwa unyenyekevu wanapitisha mkate kwa waumini. Kiongozi anayesimamia anaupokea kwanza, baada ya hapo hakuna utaratibu uliowekwa. Mara trei zinapowafikia waumini, wanaweza kupitishiana wao kwa wao.
-
Waumini wanashiriki kwa mkono wao wa kulia pale inapowezekana.
-
Wakati mkate ukiisha kupitishwa kwa waumini wote, wale wanaopitisha sakramenti wanarudisha trei kwenye meza ya sakramenti. Wale wanaobariki sakramenti wanafunika trei za mkate na kufunua trei za maji.
-
Mtu anayebariki maji anapiga magoti na anasema sala ya sakramenti kwa ajili ya maji (ona Mafundisho na Maagano 20:79). Anatumia neno maji badala ya divai.
-
Baada ya sala, wenye ukuhani kwa unyenyekevu wanapitisha maji kwa waumini. Kiongozi anayesimamia anayapokea kwanza, baada ya hapo hakuna utaratibu uliowekwa.
-
Maji yanapokuwa yamepitishwa kwa waumini wote, wale wanaopitisha sakramenti wanarudisha trei kwenye meza ya sakramenti. Wale waliobariki sakramenti wanafunika trei za maji na wale waliobariki na kupitisha sakramenti kwa unyenyekevu wanarejea kwenye nafasi zao za awali.
-
Baada ya mkutano, wale walioandaa sakramenti wanasafisha, kukunja vitambaa vya mezani na kuondoa mkate wowote ambao haukutumika.
18.10
Kutunukia Ukuhani na Kusimikwa kwenye Ofisi
Kuna aina mbili za ukuhani: Ukuhani wa Haruni na melkizedeki ( ona 3.3; Mafundisho na Maagano 107:1, 6). Wakati ukuhani unapotunukiwa kwa mtu, pia anasimikwa kwenye ofisi katika ukuhani ule. Baada ya mojawapo ya kuhani hizi kutunukiwa, mtu anahitaji kusimikwa tu kwenye ofisi zingine katika ukuhani huo.
18.10.1
Ukuhani wa Melkizedeki
Rais wa kigingi anashikilia funguo za ukuhani kwa ajili ya kutunukia Ukuhani wa Melkizedeki na kusimika kwenye ofisi za mzee na kuhani mkuu. Hata hivyo, askofu kwa kawaida anatoa mapendekezo kwa ajili ya kutunukiwa huku.
18.10.1.1
Wazee
Akina kaka wanaostahili wanaweza kupokea Ukuhani wa Melkizedeki na kutawazwa wazee wakati wanapokuwa na umri wa miaka18 au zaidi. Kutegemeana na hali ya mtu binafsi, askofu anaamua kama mvulana anapaswa kupendekezwa ili kusimikwa kuwa mzee mara baada ya mwaka wake wa 18 wa kuzaliwa au kubaki na akidi ya makuhani kwa muda mrefu.
Katika kufanya uamuzi huu, askofu anashauriana kwanza na mvulana huyo na wazazi wake au walezi wake. Wanaume wanaostahili wanapaswa kutawazwa wazee kwenye umri wa miaka 19 au kabla hawajaondoka nyumbani kuhudhuria chuo, kuhudumu misheni, kuhudumu katika jeshi au kukubali ajira ya kudumu.
Wanaume waliobatizwa hivi karibuni wenye umri wa miaka 18 na zaidi wanatawazwa kuwa wazee baada ya:
-
Kupokea ukuhani wa Haruni na kuhudumu kama kuhani.
-
Kukuza uelewa wa kutosha wa injili.
-
Kuonesha ustahili wao.
Hakuna muda maalumu kama muumini wa Kanisa unaotakiwa.
18.10.1.2
Makuhani Wakuu
Wanaume wanatawazwa kuwa makuhani wakuu wakati wanapoitwa kwenye urais wa kigingi, baraza kuu, au uaskofu.
18.10.1.3
Kusaili na kuidhinisha
Kwa kibali cha urais wa kigingi, askofu anamsaili kaka kama ilivyoelekezwa kwenye Kumbukumbu ya Utawazo kwenye Ukuhani wa Melkizedeki. Kisha mshiriki wa urais wa kigingi pia anamsaili. Kwa idhini kutoka kwa rais wa misheni, rais wa wilaya anaweza kumsaili kaka anayetarajia kutawazwa kuwa mzee (ona 6.3).
18.10.2
Ukuhani wa Haruni
Askofu anashikilia funguo za ukuhani kwa ajili ya kutunukia Ukuhani wa Haruni na utawazo kwenye ofisi za shemasi, mwalimu na kuhani. Akinakaka wanaostahili kwa kawaida wanatawazwa kwenye ofisi hizi katika umri ufuatao, lakini siyo kabla ya umri huo:
-
Shemasi mwanzoni mwa mwaka wao wa miaka 12
-
Mwalimu mwanzoni mwa mwaka wao wa miaka 14
-
Kuhani mwanzoni mwa mwaka wao wa miaka 16
Askofu au mshauri aliyepewa jukumu anawasaili wale ambao wanatakiwa kutawazwa kama mashemasi au walimu ili kuamua kama wamejiandaa kiroho. Askofu anawasaili akina kaka ambao watatawazwa kuwa makuhani.
Kabla ya kumsaili kijana kwa ajili ya kutawazwa kuwa kuhani, mshiriki wa uaskofu anatafuta ruhusa kutoka kwa wazazi au walezi wa kijana. Kama wazazi wametalikiana, anapata ruhusa kutoka kwa wazazi wenye ulezi wake kisheria.
18.10.3
Kumtambulisha Muumini ili Aidhinishwe kabla Hajatawazwa
Baada ya kaka kusailiwa na kuonekana anastahili kutawazwa kwenye ofisi ya ukuhani, anatambuliswa kwa ajili ya kuidhinishwa (ona Mafundisho na Maagano 20:65, 67). Akina Kaka wanaotarajiwa kutawazwa kuwa wazee au makuhani wakuu wanatambulishwa na mshiriki wa urais wa kigingi katika kikao cha mkutano mkuu wa Kigingi (ona 6.3 kwa ajili ya maelekezo kwa marais wa wilaya). Akina kaka wanaotarajia kutawazwa kuwa mashemasi, walimu au makuhami wanatambulishwa na mshauri wa uaskofu katika mkutano wa sakramenti.
Mtu ambaye anaongoza kuidhinisha anamwomba kaka asimame. Anatangaza pendekezo la kumtunukia ukuhani wa Haruni au Melkizedeki (kama inahitajika) na kumtawaza kaka huyo kwenye ofisi ya ukuhani. Kisha anawaalika waumini wathibitisha pendekezo. Kwa mfano, ili kumtambulisha kaka anayetarajia kutawazwa kuwa mzee, angeweza kutumia maneno kama haya:
“Tunapendekeza kwamba [jina] apokee Ukuhani wa Melkizedeki na atawazwe kuwa mzee. Wote wanaokubali wanaweza kuonesha kwa kuinua mkono. [Kaa kimya kwa muda mfupi.] Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza pia kuonesha. [Kaa kimya kwa muda mfupi.]”
Kama mshiriki mwenye msimamo mzuri anapinga utawazo huo, kiongozi msimamizi au kiongozi mwingine wa ukuhani aliyepewa jukumu anakutana naye kwa faragha baada ya mkutano. Kiongozi anatafuta kuelewa kwa nini muumini anapinga. Anatafuta kujua kama muumini anajua tabia ambayo ingeweza kumzuia mtu yule kutotawazwa kwenye ofisi ya ukuhani.
Katika baadhi ya masuala, kaka anaweza kuhitaji kutawazwa kuwa mzee au kuhani mkuu kabla hajatambulishwa katika mkutano mkuu wa kigingi. Hii inapotokea, anatambulishwa katika mkutano wa sakramenti wa kata yake kwa ajili ya kukubaliwa. Kisha anatambulishwa katika mkutano mkuu wa kigingi unaofuata ili kuthibitisha utawazo huo (ukifuata mchakato wa kuidhinisha, kama ilivyoelezwa hapo juu).
18.10.4
Nani Anafanya Ibada
Rais wa kigingi au mwenye Ukuhani wa Melkizedeki chini ya maelekezo yake anaweza kumtawaza mtu kwenye ofisi ya mzee. Kwa idhini kutoka kwa rais wa misheni, rais wa wilaya au mtu fulani chini ya maelekezo yake anaweza kutekeleza utawazo huo (ona 6.3). Wale wenye Ukuhani wa Melkizedeki pekee ndio wanaweza kusimama katika mduara.
Rais wa kigingi au kuhani mkuu chini ya maelekezo yake anaweza kumtawaza mtu kwenye ofisi ya kuhani mkuu. Makuhani wakuu pekee ndiyo wanaoweza kusimama katika mduara.
Mtu anayemtawaza mtu mwingine kwenye ofisi ya Ukuhani wa Melkizedeki anapaswa kuwa mwenye kustahili kuingia hekaluni. Rais wa kigingi au mtu mwingine anayemteua lazima awepo.
Kuhani au mwenye Ukuhani wa Melkizedeki anaweza kumtawaza kaka kwenye ofisi ya shemasi, mwalimu au kuhani. Lazima awe ameruhusiwa na askofu. Askofu au mtu mwingine anayemteua lazima awepo.
Kushiriki katika utawazo wa Ukuhani wa Haruni, mtu lazima awe kuhani, au mwenye Ukuhani wa Melkizedeki.
Askofu anaweza kumruhusu baba ambaye ni kuhani au mwenye Ukuhani wa Melkizedeki kumtawaza mtoto wake kwenye ofisi ya shemasi, mwalimu au kuhani hata kama baba hastahili kikamilifu kwa ajili ya kuingia hekaluni (ona 18.3). Maaskofu wanawahimiza akina baba wajiandae ili kuwatawaza watoto wao wenyewe.
18.10.5
Maelekezo
Ili kumtunukia ukuhani na kumtawaza mtu kwenye ofisi ya ukuhani, mwenye ukuhani mmoja au zaidi walioruhusiwa wanaweka mikono yao kwa wepesi juu ya kichwa cha mtu. Kisha yule anayezungumza:
-
Anamwita mtu yule kwa jina lake kamili.
-
Anasema mamlaka ambayo yeye binafsi anayo kwa ajili ya kufanya ibada (labda ya Ukuhani wa Haruni au Melkizedeki).
-
Anamtunukia ukuhani wa Haruni au Melkizedeki, isipokuwa tu awe tayari ametunukiwa.
-
Anamtawaza mtu kwenye ofisi katika ukuhani wa Haruni au wa Melkizedeki na kumpatia haki, nguvu na mamlaka ya ofisi ile.
-
Anatoa maneno ya baraka kama atakavyoongozwa na Roho.
-
Anafunga katika jina la Yesu Kristo.
Kumtawaza mtu kwenye ofisi ya ukuhani baada ya kuwa tayari alipata ukuhani husika kutunukiwa juu yake, mtu anayefanya utawazo huo anaruka hatua ya 3.
18.10.6
Kumbukumbu na cheti cha Utawazo
Kabla kaka hajasailiwa ili kutawazwa kwenye ofisi katika ukuhani wa Haruni, karani anatumia (LCR) kutayarisha Kumbukumbu ya Utawazo kwenye Ukuhani wa Haruni. Askofu au mshauri aliyepewa jukumu anaendesha usaili na kusaini fomu kama masharti yote ya kuwa mwenye kustahili yametimia.
Baada ya utawazo, askofu au mshauri aliyepewa jukumu anakamilisha fomu na kumpa karani. Karani anaweka kumbukumbu ya utawazo huo katika LCR na anatayarisha cheti cha utawazo.
Jina la sasa la kisheria la mtu linapaswa kutumika kwenye rekodi ya utawazo na cheti.
18.11
Kuwasimika Waumini ili Watumikie katika Miito
Waumini wanaoitwa na kukubaliwa katika nafasi nyingi za Kanisa wanapaswa kusimikwa ili kuhudumia katika nafasi hiyo (ona Yohana 15:16; Mafundisho na Maagano 42:11; ona pia 3.4.3.1 katika Kitabu hiki cha maelezo ya jumla). Wakati wa kusimikwa, mtu anapewa (1) mamlaka ya kutenda katika wito huo na (2) maneno ya baraka kadiri Roho atakavyoongoza.
Marais wa vigingi, maaskofu na akidi za marais wanapokea funguo za urais wakati wanaposimikwa (ona 3.4.1.1). Hata hivyo, neno funguo halipaswi kutumika wakati wa kuwasimika waumini kuhudumu katika miito mingine, ikijumuisha washauri katika urais.
18.11.1
Nani Hufanya Usimikaji Huo
Kusimika kunafanywa na mwenye Ukuhani wa Melkizedeki. Lazima apokee kibali kutoka kwa kiongozi anayeshikilia funguo halali za ukuhani. Wale ambao wameruhusiwa kuwasimika waumini wameoneshwa katika 30.8. Mtu kwenye ofisi ya mzee hapaswi kuwa msemaji au kusimama kwenye mduara wakati mwanamume anaposimikwa kwenye ofisi ambayo inamhitaji awe kuhani mkuu.
Chini ya maelekezo ya kiongozi anayesimamia, mtu mmoja au zaidi wenye Ukuhani wa Melkizedeki anaweza kushiriki katika kusimika. Marais wanasimikwa mbele ya washauri wao.
Kiongozi anayesimamia anaweza kumruhusu mume au baba mwenye Ukuhani wa Melkizedeki asimame katika duara kwa ajili ya kusimikwa kwa mkewe au watoto hata kama hastahili kikamilifu kwa ajili ya kuingia hekaluni (ona 18.3).
18.11.2
Maelekezo
Mtu mmoja au zaidi wanaoshikilia Ukuhani wa Melkizedeki walioruhusiwa wanaweka mikono yao kwa wepesi kwenye kichwa cha mtu. Kisha yule anayezungumza:
-
Anamwita mtu yule na jina lake kamili.
-
Anasema kwamba anafanya kwa mamlaka ya Ukuhani wa Melkizedeki.
-
Anamsimika mtu huyo kwenye wito katika kigingi, kata, akidi au darasa.
-
Anampa funguo kama mtu anapaswa kuzipokea.
-
Anatoa maneno ya baraka kama atakavyoongozwa na Roho.
-
Anafunga katika jina la Yesu Kristo.
18.12
Kuweka wakfu Mafuta
Wenye Ukuhani wa Melkizedeki lazima waweke wakfu mafuta ya mzeituni kabla hayajatumika kumpaka mgonjwa au wanaoteseka (ona Yakobo 5:14). Hakuna mafuta mengine yanayoweza kutumika.
Waumini hawapaswi kunywa mafuta yaliyowekwa wakfu au kutumia kwenye sehemu za mwili zilizoumia.
18.12.1
Nani Anafanya Ibada
Mtu mmoja au zaidi wanaoshikilia Ukuhani wa Melkizedeki wanaweza kuweka wakfu mafuta. Hawahitaji kupata kibali kutoka kwa kiongozi wa ukuhani.
18.12.2
Maelekezo
Ili kuweka wakfu mafuta, mwenye Ukuhani wa Melkizedeki:
-
Anashikilia chupa iliyo wazi ya mafuta ya mzeituni.
-
Anamwita Baba wa Mbinguni kama katika sala.
-
Anasema kwamba anafanya kwa mamlaka ya Ukuhani wa Melkizedeki.
-
Anaweka wakfu mafuta (siyo chombo) na kuyapa upekee kwa ajili ya kuwapaka na kuwabariki wagonjwa na wanaoteseka.
-
Anafunga katika jina la Yesu Kristo.
18.13
Kuwahudumia Wagonjwa
Kuwahudumia wagonjwa “kwa kuweka mikono juu yao” kuna sehemu mbili: kupaka mafuta na kufunga mpako huo wa mafuta kwa kutoa baraka. Kama mafuta yaliyowekwa wakfu hayapatikani, baraka inaweza kutolewa kwa mamlaka ya Ukuhani wa Melkizedeki bila mpako wa mafuta.
18.13.1
Nani Anatoa Baraka kwa Wagonjwa
Wenye Ukuhani wa Melkizedeki wanaostahili pekee wanaweza kutoa baraka kwa mgonjwa na anayeteseka. Hawahitaji kupata kibali kutoka kwa kiongozi wa ukuhani. Kama inawezekana, baba mwenye Ukuhani wa Melkizedeki anaweza kumhudumia mwanafamilia yake ambaye ni mgonjwa.
Kwa kawaida, watu wawili au zaidi wenye Ukuhani wa Melkizedeki wanamhudumia mgonjwa. Hata hivyo, mmoja anaweza kufanya vyote kupaka mafuta na kufunga mpako kwa baraka.
18.13.2
Maelekezo
Kupaka mafuta kunafanywa na mtu mmoja mwenye Ukuhani wa Melkizedeki. Yeye:
-
Anaweka tone la mafuta yaliyowekwa wakfu juu ya kichwa cha mtu.
-
Anaweka mikono yake kwa wepesi juu ya kichwa cha mtu na kumwita mtu huyo kwa jina lake kamili.
-
Anasema kwamba anafanya kwa mamlaka ya Ukuhani wa Melkizedeki.
-
Anasema kwamba anampaka mafuta ambayo yamewekwa wakfu kwa ajili ya kuwapaka na kuwabariki wagonjwa na wanaoteseka.
-
Anafunga katika jina la Yesu Kristo.
Kufunga mpako wa mafuta, mtu mmoja au zaidi wenye Ukuhani wa Melkizedeki wanaweka mikono yao kwa wepesi juu ya kichwa cha mtu. Kisha yule anayefunga mpako:
-
Anamwita mtu yule na jina lake kamili.
-
Anasema kwamba anafunga mpako wa mafuta kwa mamlaka ya Ukuhani wa Melkizedeki.
-
Anatoa maneno ya baraka kama atakavyoongozwa na Roho.
-
Anafunga katika jina la Yesu Kristo.
18.14
Baraka za Faraja na Ushauri, Ikijumuisha Baraka za Baba
18.14.1
Nani Anatoa Baraka
Mwenye Ukuhani wa Melkizedeki anaweza kutoa baraka za faraja na ushauri kwa mwanafamilia na kwa wengine ambao wanaziomba.
Baba mwenye Ukuhani wa Melkizedeki anaweza kutoa baraka za baba kwa watoto wake. Wazazi wanawahimiza watoto wao watafute baraka za baba nyakati za mahitaji. Baraka za baba zinaweza kurekodiwa kwa ajili ya matumizi binafsi.
Mwenye Ukuhani wa Melkizedeki hahitaji kutafuta kibali kutoka kwa kiongozi wa ukuhani kutoa baraka za faraja na ushauri au baraka ya baba.
18.14.2
Maelekezo
Kutoa baraka za faraja na ushauri au baraka ya baba, mtu mmoja au wawili wenye Ukuhani wa Melkizedeki wanaweka mikono yao kwa wepesi juu ya kichwa cha mtu. Kisha yule anayezungumza:
-
Anamwita mtu yule kwa jina lake kamili.
-
Na kusema kwamba baraka inafanywa kwa mamlaka ya Ukuhani wa Melkizedeki.
-
Anatoa maneno ya baraka, faraja na ushauri kama atakavyoongozwa na Roho.
-
Anafunga katika jina la Yesu Kristo.
18.15
Kuweka Wakfu Makazi
Waumini wa Kanisa wanaweza kuweka wakfu nyumba zao kwa mamlaka ya ukuhani wa Melkizedeki.
18.15.2
Maelekezo
Kuweka wakfu nyumba, mwenye Ukuhani wa Melkizedeki:
-
Anamwita Baba wa Mbinguni kama katika sala.
-
Anasema kwamba anatenda kwa mamlaka ya Ukuhani wa Melkizedeki.
-
Anaweka wakfu nyumba kama mahali patakatifu ambapo Roho Mtakatifu anaweza kuishi na anatoa maneno mengine kama anavyoongozwa na Roho.
-
Anafunga katika jina la Yesu Kristo.
18.16
Kuweka Wakfu Makaburi
18.16.1
Nani Anaweka Wakfu Makaburi
Mtu anayeweka wakfu makaburi anapaswa kuwa na Ukuhani wa Melkizedeki na awe ameruhusiwa na kiongozi wa ukuhani anayeendesha huduma.
18.16.2
Maelekezo
Kuweka wakfu kaburi, mwenye Ukuhani wa Melkizedeki:
-
Anamwita Baba wa Mbinguni kama katika sala.
-
Anasema kwamba anafanya kwa mamlaka ya Ukuhani wa Melkizedeki.
-
Anaweka wakfu na kufanya eneo la maziko kuwa mahali pa kupumzika kwa mwili wa marehemu.
-
Anasali kwamba mahali patatakaswa na kulindwa mpaka Ufufuko (kama itafaa).
-
Anamwomba Baba wa Mbinguni kuifariji familia na kutoa mawazo kama anavyoongozwa na Roho.
-
Anafunga katika jina la Yesu Kristo.
Kama mwili wa muumini wa Kanisa umechomwa, kiongozi anayesimamia anatumia busara yake kuamua ikiwa aweke wakfu mahali ambapo majivu yanatunzwa.
18.17
Baraka za Patriaki
Kila muumuni aliyebatizwa anayestahili ana haki ya kupokea Baraka ya Patriaki, ambayo inatoa maelekezo ya kutia moyo kutoka kwa Baba wa Mbinguni (ona Mwanzo 48:14–16; 49; 2 nefi 4:3–11).
Askofu au mshauri aliyepewa jukumu anawasaili waumini wanaotamani kupokea baraka ya Patriaki. Kama muumini anastahili, anayesaili anatayarisha Kibali cha Baraka ya Patriaki. Anakiwasilisha kupitia Mfumo wa Baraka ya Patriaki kwenye ChurchofJesusChrist.org.
Mtu anayetoa Kibali cha Baraka ya Patriaki anahakikisha kwamba muumini amepevuka vya kutosha kuelewa umuhimu na asili tukufu ya baraka.
18.17.1
Kupokea Baraka ya Patriaki
Baada ya kupokea kibali, muumini anawasiliana na patriaki kupanga ahadi ya kupokea baraka ya patriaki. Siku ya miadi, muumuni anapaswa kwenda kwa patriaki akiwa na mtazamo wa sala na katika mavazi ya Jumapili.
Kila baraka ya patriaki ni takatifu, ya siri na binafsi. Kwa hiyo, inatolewa kwa faragha isipokuwa kwa idadi yenye ukomo ya wanafamilia ambao wanaweza kuwepo.
Mtu anayepokea baraka ya patriaki anapaswa kuthamini sana maneno ya baraka, kuyatafakari na kuishi kwa kustahili kupokea baraka zilizoahidiwa katika maisha haya na milele.
Waumini wa Kanisa hawapaswi kufananisha baraka na hawapaswi kuzishiriki isipokuwa kwa wanafamilia wa karibu. Baraka za patriaki hazipaswi kusomwa katika mikutano ya Kanisa au mikusanyiko mingine ya umma.