Vitabu vya Maelekezo na Miito
29. Mikutano katika Kanisa


“29. Mikutano katika Kanisa,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“29. Mikutano katika Kanisa,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

mama na binti kwenye mkutano wa sakramenti

29.

Mikutano katika Kanisa

29.0

Utangulizi

Watakatifu wa siku za mwisho wanakutana pamoja ili kuabudu, kuadilishana wao kwa wao, na kufundisha na kujifunza injili (ona Alma 6:6; Moromi 6:5–6). Mwokozi aliahidi, “walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao” (Mathayo 18:20). Kukutana pamoja ni njia mojawapo ambayo mioyo yetu inaweza “kuunganishwa pamoja katika umoja na upendo” (Mosia 18:21).

Hata hivyo, kufanya mkutano hakupaswi kuchukuwa nafasi ya kutumikiana na kuhudumiana kama Yesu Kristo alivyofanya.

29.1

Kupanga na Kuendesha Mikutano

Viongozi wanapanga na Kuendesha Mikutano “kadiri watakavyoongozwa na Roho Mtakatifu, kulingana na amri na mafunuo ya Mungu” (Mafundisho na Maagano 20:45; ona pia Moroni 6:9; Mafundisho na Maagano46:2). Wanatafuta njia za kualika ushawawishi wa Roho katika mikutano yao.

Viongozi wanahakikisha kwamba idadi na urefu wa mikutano havisababishi mizigo kwa waumini au familiaa zao.

29.2

Mikutano ya Kata

29.2.1

Mkutano wa Sakramenti

29.2.1.1

Kupanga Mkutano wa Sakramenti

Uaskofu unapanga na kuendesha mikutano ya sakramenti. Wanahakikisha kwamba fokasi ya mkutano ni juu ya sakramenti na kujenga imani katika Yesu Kristo.

Mkutano wa Sakramenti unadumu kwa saa moja. Unaweza kujumuisha yafuatayo:

  1. Muziki wa kabla ya ibada kuanza (ona 19.3.2 kwa miongozo).

  2. Kusalimia na kukaribishana.

  3. Utambuzi wa mamlaka zinazoongoza au viongozi wengine ambao wanatembelea.

  4. Matangazo. Haya yanapaswa kuwa machache.

  5. Wimbo wa ufunguzi na sala. Ona 19.5:2 na 29.6.

  6. Shughuli za kata na Vigingi, kama zifuatazo:

    • Kura ya kukubali na kuwapumzisha maafisa na walimu (ona 30.3 na 30.6).

    • Kuwasilisha majina ya akina kaka ili kutawazwa kwenye ofisi katika Ukuhani wa Haruni (ona 18.10.3).

    • Kuwatambua waumini wapya wa kata, pamoja na waongofu wa hivi karibuni.

  7. Kuwapa majina na kuwabariki Watoto (ona 18.6). Hii mara nyingi hufanywa kwenye mkutano wa mfungo na ushuhuda (ona 29.2.2).

  8. Kuwathibitisha waongofu wapya ona 18.8).

  9. Wimbo wa sakramenti na huduma ya sakramenti. Sakramenti ni fokasi kuu ya mkutano. Ibada hii ni fursa kwa ajili ya waumini kuelekeza mawazo yao kuelekea kwa Mwokozi na dhabihu Yake kwa ajili yao.

    Kwa zaidi kuhusu kuandaa, kubariki, na kupitisha sakramenti, ona 18.9.

  10. Ujumbe wa Injili na uimbaji wa mkusanyiko wa waumini au muziki mwingine.

  11. Wimbo wa kufunga na sala

  12. Muziki wa baada ya ibada.

29.2.1.4

Kuwachagua Wazungumzaji

Uaskofu unachagua wazungumzaji kwa ajili ya mkutano wa sakramenti. Mara nyingi wanawaalika waumini wa kata, pamoja na vijana.

Wazungumzaji wanatoa ushuhuda juu ya Yesu Kristo na kufundisha injili Yake kwa kutumia maandjko (ona Mafundisho na Maagano 42:12; 52:9).

29.2.2

Mkutano wa Mfungo na Ushuhuda

Katika mkutano wa mfungo na ushuhuda, hakuna uteuzi wa wazungumzaji au uchaguzi maalumu wa muziki. Badala yake, mtu anayeendesha anatoa ushuhuda mfupi. Kisha anawaalika washiriki wa mkutano kutoa shuhuda zao. Kutoa ushuhuda kunamaanisha kutangaza kweli za injili kama ziliyofunuliwa na Roho Mtakatifu.

29.2.3

Mkutano wa Kata

29.2.4

Mkutano wa Uaskofu

Maswala ya kufikiriwa yangeweza kujumuisha:

  • Kuratibu kazi ya wokovu na kuinuliwa, katika kata.

  • Kuwaimarisha watu binafsi na familia katika kata—hususani vijana na watoto.

  • Kuwatambua waumini ambao wangeweza kujitayarisha kupokea ibada, ikiwa ni pamoja na utawazo kwenye ukuhani.

  • Kuwatambua waumini ili kuwaita kwenye nafasi za kata.

29.2.5

Mkutano wa Baraza la Kata

Askofu anapanga, anaongoza, na kuendesha mikutano ya baraza la kata. Baraza halifanyi maamuzi makubwa bila askofu.

Viongozi wa vikundi katika kata wanahudhuria mikutano ya baraza la kata katika nafasi mbili:

  1. Kama waumini wa baraza la kata wanaosaidia kubariki waumini wote wa kata.

  2. Kama wawakilishi wa vikundi vyao.

Wakati wanapokutana pamoja, washiriki wa baraza la kata wanajadiliana maswala ambayo yatanufaisha kutokana na juhudi za baraza zima. Kila mshiriki wa baraza anahimizwa kushiriki mawazo na ushawishi wake kwenye maswala haya.

Mikutano ya baraza la kata kwa kawaida haidumu zaidi ya saa moja. Wanaanza na sala na ripoti fupi juu ya majukumu kutoka kwenye mikutano iliyotangulia. Askofu anatoa kipaumbele kwenye maswala ambayo yanahitajika zaidi kuwabariki watu binafsi na familia.

  • Kuishi Injili ya Yesu Kristo. Kuwasaidia waumini wote wajenge imani, wapokee ibada za wokovu, na washike maagano yao.

  • Kuwajali wale wenye shida. Kushiriki nyenzo na ujuzi ili kuwabariki watu binafsi, familia, na jumuiya. Kuwasaidia waumini wa kata wawe wenye kujitegemea. (Ona sura ya 22.)

  • Kuwaalika wote waipokee injili. Kurejelea maendeleo ya wale wanaojifunza kuhusu injili, vile vile waumini wapya na wanaorejea. Kujadili njia ambazo kwazo waumini wanaweza kushiriki injili na wengine. (Ona sura ya 23.)

  • Kuziunganisha familia milele. Kurejelea maendeleo ya waumini wanaojitayarisha kupokea ibada za hekaluni. Kupanga njia za kuwasaidia zaidi waumini wastahili kwa ajili ya kibali cha hekaluni. Kujadili njia ambazo kwazo waumini wanaweza kushiriki katika kazi ya hekaluni na historia ya familia. (Ona sura ya 25.)

Washirik wa baraza lazima watunze siri kwa taarifa yoyote kibinafsi au taarifa nyeti (ona 4.4.6).

4:37

29.2.6

Mkutano wa Baraza la Vijana la Kata

Kabla ya kila mkutano, askofu na mtu anayeendesha wanarejelea vipengele vya kujadili.

  • Kazi ya Wokovu na kuinuliwa.

  • Mahitaji ya vijana katika kata na njia za kushughulika nayo.

  • Juhudi za kuwafikia vijana ambao hawashiriki kikamilifu au waumini wapya.

  • Shughuli, ikijumuisha fursa ya kuwahudumia wale walio katika shida. Mipango mingi hufanyika zaidi katika akidi au mikutano ya urais wa darasa (ona sura ya 20).

  • Uhudumiaji (ona sura ya 21.)

  • Kuwaelekeza urais mpya ulioitwa wa akidi na darasa.

29.2.8

Ratiba ya Mikutano ya Jumapili

Kata zinatumia moja ya ratiba ifuatayo ya masaa mawili kwa ajili ya mikutano ya Jumapili.

Mpango 1

Dakika 60

Mkutano wa Sakramenti

Dakika 10

Mabadiliko kwenda Madarasani na mikutanoni

Dakika 50

Jumapili zote: Msingi, ikijumuisha chekechea

Jumapili ya kwanza na ya tatu za mwezi: Shule ya Jumapili

Jumapili ya pili na ya nne: mikutano ya akidi za ukuhani, Muungano wa Usaidizi, na mikutano ya Wasichana.

Jumapili za tano: mikutano kwa ajili ya vijana na watu wazima. Uaskofu Simamizi unaamua mada na unateua walimu.

Mpango 2

Dakika 50

Jumapili zote: Msingi, pamoja na chekechea

Jumapili ya kwanza na ya tatu za mwezi: Shule ya Jumapili

Jumapili ya pili na ya nne: mikutano ya akidi za ukuhani, Muungano wa Usaidizi, na mikutano ya Wasichana.

Jumapili za tano: mikutano kwa ajili ya vijana na watu wazima. Uaskofu Simamizi unaamua mada na unateua walimu.

Dakika 10

Mabadiliko kwenda mikutano ya sakramenti

Dakika 60

Mkutano wa Sakramenti

29.3

Mikutano ya Kigingi

29.3.1

Mkutano wa kigingi

29.3.2

Mkutano Mkuu wa Ukuhani wa Kigingi

29.3.3

Mkutano wa Uongozi wa Ukuhani katika Kigingi

29.3.4

Mkutano wa Uongozi wa Kigingi

29.3.5

Mkutano wa Akidi ya Makuhani Wakuu katika Kigingi

29.3.6

Mkutano wa Urais wa Kigingi

29.3.7

Mkutano wa Baraza Kuu.

29.3.8

Mkutano wa Baraza la Kigingi

29.3.9

Mkutano wa Kamati ya Uongozi ya watu wazima ya kigingi

29.3.10

Mkutano wa Kamati ya Uongozi ya Vijana katika Kigingi

29.3.11

Mkutano wa Baraza la Maaskofu katika Kigingi

29.5

Mazishi na Huduma Nyinginezo kwa ajili ya Marehemu

29.5.1

Kanuni za Jumla

Dhumuni kubwa la huduma za Kanisa kwa ajili ya wafu ni kushuhudia juu ya mpango wa wokovu, hususani Upatanisho wa Mwokozi na Ufufuko. Huduma hizi zinapaswa kuwa za heshima, uzoefu wa kiroho.

Viongozi wa Kanisa hawapaswi kujumuisha matambiko ya makanisa mengine au vikundi katika huduma za kanisa kwa ajili ya wafu.

29.5.2

Kutoa Msaada kwa Familia

Kama wafuasi wa Yesu Kristo, viongozi wa Kanisa na waumini “huomboleza na wale wanaoomboleza … na kuwafariji wale ambao wanahitaji kufarijiwa” (Mosia 18:9). Wakati muumini anapofariki, askofu anaitembelea familia ili kuwafariji.

Askofu anatoa msaada kutoka kwa waumini wa kata, ikijumuisha akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi.

29.5.4

Huduma za Mazishi (kwenye sheria za Mila)

Mazishi yanayoendeshwa na askofu, iwe katika jengo la Kanisa au mahali pengine popote pale, ni mkutano wa Kanisa na ni huduma ya kidini. Unapaswa kuwa tukio la kiroho.

Mazishi yanapaswa kuanza kwa wakati. Kwa kawaida, hayapaswi kudumu zaidi ya saa1.30, kwa heshima ya wale waliohudhuria.

Huduma za mazishi kwa kawaida hazifanywi siku ya Jumapili.

29.6

Sala katika Mikutano ya Kanisa

Sala katika mikutano ya Kanisa zinapaswa ziwe fupi, za kawaida, na zilizoelekezwa na Roho. Muumini yeyote wa Kanisa aliyebatizwa anaweza kutoa sala ya ufunguzi na ya kufunga. Watoto ambao hawajabatizwa wanaweza kusali katika Msingi.

29.7

Kutiririsha Mikutano na Kufanya Mikutano Kwa Njia ya Mitandao

Askofu anaweza, kama jambo la kipekee kuruhusu utiririshaji wa mikutano ya sakramenti na mazishi na harusi iliyofanyika katika nyumba ya mkutano.

Utiririshaji wa mikutano ya sakramenti haupaswi kujumuisha huduma ya sakramenti.

Kwa baadhi ya mikutano, askofu au rais wa kigingi anaweza kuruhusu waumini ambao hawawezi kuhudhuria binafsi washiriki kwa njia ya mtandao. Mikutano hii inaweza kujumuisha:

  • Mikutano ya uongozi, kama vile mikutano ya urais au mikutano ya baraza.

  • Akidi, Muungano wa Usaidizi, na mikutano ya Wasichana.

  • Darasa la Shule ya Jumapili.

  • Madarasa ya Msingi na muda wa kuimba.