Maktaba
Maelekezo kwa ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti


“Maelekezo kwa ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Jipya 2023 (2023)

“Maelekezo kwa ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watoto: 2023

watoto wa Msingi wanaimba na kufanya vitendo kwa mikono

Maelekezo kwa ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti

Wapendwa Urais wa Msingi na Viongozi wa Muziki,

Nyimbo za Msingi ni zana yenye nguvu sana katika kuwasaidia watoto kujifunza kuhusu mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni na ukweli wa kimsingi wa injili ya Yesu Kristo. Wakati watoto wanapoimba kuhusu kanuni za injili, Roho Mtakatifu atashuhudia juu ya ukweli wa kanuni hizo. Maneno na muziki vitakaa katika akili na mioyo ya watoto maisha yao yote.

Tafuta msaada wa Roho unapojiandaa kufundisha injili kupitia muziki. Toa ushuhuda wako juu ya ukweli mnaoimba. Wasaidie watoto waone jinsi muziki unavyohusiana na kile wanachopitia na kujifunza nyumbani na katika madarasa ya Msingi. Watoto na familia zao watabarikiwa kwa juhudi zako za dhati za kuwasaidia watoto kuimba muziki mtakatifu.

Tunawapenda na tunatoa shukrani zetu kwa huduma ya kujitolea ambayo mnatoa ili kuwaimarisha na kuwalinda watoto wetu wa thamani.

Urais Mkuu wa Msingi

Maelekezo kwa ajili ya Muda wa Kuimba

Dakika 5 (Urais wa Msingi): Sala ya kufungua, andiko au makala ya imani, na hotuba moja

Dakika 20 (kiongozi wa muziki): Muda wa kuimba

Urais wa Msingi na kiongozi wa muziki huchagua nyimbo kwa kila mwezi ili kuimarisha kanuni watoto wanazojifunza katika madarasa na nyumbani. Orodha ya nyimbo ambazo zinaimarisha kanuni hizi imejumuishwa katika mwongozo huu. Nyimbo hizi pia zimependekezwa katika mihutasari katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi na Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.

Unapofundisha nyimbo kwa watoto, waalike waeleze kile ambacho tayari wamejifunza kuhusu hadithi na kanuni za mafundisho katika nyimbo unazofundisha. Unaweza kutaka kurejelea mihutasari ya Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi ambayo watoto wanajifunza katika madarasa yao. Hii itakusaidia wewe kuzijua hadithi na kanuni ambazo wanajifunza ili kwamba uweze kufikiria jinsi ya kuwasaidia kujifunza kupitia muziki.

Wakati wa kuimba, unaweza pia kurejelea nyimbo ambazo watoto walishajifunza hapo awali na nyimbo wanazofurahia kuziimba. Wakati ukifanya marejeo, waalike watoto kwa kifupi kutoa mawazo na hisia zao kuhusu kweli zinazopatikana katika nyimbo.

Kitabu cha Nyimbo za Watoto ni nyenzo ya msingi kwa ajili ya muziki katika Msingi. Nyimbo kutoka kitabu cha nyimbo za Kanisa na nyimbo kutoka kwenye gazeti la Rafiki au Liahona pia zinafaa. Mara chache watoto wanaweza kuimba nyimbo za kizalendo au za sikukuu ambazo zinafaa kwa ajili ya Jumapili na kwa umri wa watoto. Matumizi ya muziki wowote tofauti kwenye Msingi lazima yaidhinishwe na uaskofu (ona General Handbook: Serving in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, 12.3.4, ChurchofJesusChrist.org).

Muhtasari juu ya Msingi

Kila wiki, Msingi hujumuisha:

Muda wa kuimba:Dakika 25

Mapumziko:Dakika 5

Madarasa:Dakika 20

Viongozi wa Msingi wenye idadi kubwa ya watoto wanaweza kuwagawa katika makundi mawili na kuwa na kundi moja katika madarasa ya Msingi wakati kundi lingine wakiwa katika muda wa kuimba. Kisha makundi mawili haya yangeweza kubadilishana nafasi. Katika hali kama hizo, viongozi wanaweza kuhitaji kubadilisha muda uliooneshwa hapo juu ili kuendana na hali zao.

watoto wa Msingi wakiwa wameinua juu picha za Yesu

Muziki Uliopendekezwa kwa ajili ya Muda wa Kuimba

Januari

  • Come, Follow Me,” Nyimbo za Kanisa, na. 116

  • A Child’s Prayer,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13

  • Jesus Once Was a Little Child,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 55

Februari

  • Baptism,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 100–101

  • I Will Follow God’s Plan,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 164–65

  • He Sent His Son,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35

Machi

  • I’m Trying to Be like Jesus,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79

  • Did You Think to Pray?,” Kitabu cha Nyimbo za Kanisa, na. 140

  • Tell Me the Stories of Jesus,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 57

Aprili

  • Faith,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96–97

  • I Feel My Savior’s Love,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75

  • Jesus Has Risen,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 70

Mei

  • Keep the Commandments,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47

  • Families Can Be Together Forever,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 188

  • I am a Child of God,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3

Juni

  • Love One Another,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 136–37

  • Tazama Mkombozi Afa,” Nyimbo za Kanisa, na. 191

  • Did Jesus Really Live Again?,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64

Julai

  • Stand for the Right,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 159

  • I’ll Walk with You,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 140–41

  • I Know My Father Lives,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 5

Agosti

  • When I Am Baptized,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 103

  • The Holy Ghost,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 105

  • The Lord Gave Me a Temple,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 153

Septemba

  • When We’re Helping,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 198

  • A Child’s Prayer,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13

  • I Know That My Redeemer Lives,” Nyimbo za Kanisa, na. 136

Oktoba

  • When He Comes Again,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83

  • The Church of Jesus Christ,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77

  • I Love to See the Temple,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95

Novemba

  • Search, Ponder, and Pray,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 109

  • Tell Me, Dear Lord,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 176

  • Kindness Begins with Me,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,145

Disemba

  • My Heavenly Father Loves Me,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29

  • Choose the Right Way,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 160–61

  • When I Am Baptized,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 103

Kutumia Muziki Kufundisha Mafundisho

Muda wa kuimba umekusudiwa kuwasaidia watoto wausikie ushawishi wa Roho Mtakatifu wakati wanapojifunza ukweli juu ya injili. Mawazo yafuatayo yanaweza kusaidia.

Jaza nafasi zilizo wazi. Andika mstari wa wimbo ubaoni kwa kuacha baadhi ya maneno muhimu. Kisha waombe watoto waimbe wimbo huo, na kusikiliza maneno ambayo yatajaza nafasi zilizoachwa wazi. Wanapokuwa wakijaza kila nafasi iliyo wazi, waalike washiriki kanuni zipi za injili wanajifunza kutokana na maneno yanayokosekana.

Tumia nukuu kutoka kwa Viongozi wa Kanisa. Waalike watoto wasikilize nukuu kutoka kwa kiongozi wa Kanisa ambayo inafundisha kanuni sawa ya injili kama ile iliyoko kwenye wimbo wa Msingi. Waombe wainue mikono yao wakati wanaposikia kitu ambacho kinawasaidia wao kuelewa ukweli ambao wanauimba. Waombe kushiriki kile walichosikia.

Toa ushuhuda. Toa ushuhuda mfupi kwa watoto kuhusu ukweli wa injili unaopatikana kwenye wimbo wa Msingi. Wasaidie watoto waelewe kwamba kuimba ni njia mojawapo wanayoweza kutoa ushuhuda na kumsikia Roho.

Tumia picha. Waombe watoto wakusaidie kupata au kutengeneza picha ambazo zinaendana na maneno muhimu au virai katika wimbo. Waalike waeleze ni jinsi gani picha zinahusiana na wimbo na kitu ambacho wimbo unafundisha. Kwa mfano, kama unafundisha wimbo “I will Follow God’s Plan” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 164–65), ungeweza kuweka picha kuzunguka chumba zikionyesha maneno muhimu kutoka kwenye wimbo (kama vile zawadi, mbingu, nyumbani, dunia, na kuzaliwa). Waombe watoto wakusanye picha na wazinyanyue juu katika utaratibu sahihi wakati mkiimba wimbo kwa pamoja.

Shiriki chombo. Unaweza kutumia kitu ili kuhamasisha mjadala kuhusu wimbo. Kwa mfano, wimbo “Faith” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96–97 unaongelea kuhusu mbegu ndogo. Ungeweza kuwaonyesha watoto mbegu ili kuwasaidia kuelewa kwamba kiasi kidogo cha imani katika Yesu Kristo kinaweza kukua kadiri muda unavyoenda.

Unganisha wimbo na uzoefu binafsi. Wasaidie watoto waunganishe kanuni zilizofundishwa kwenye wimbo na uzoefu ambao wamekuwa nao wa kanuni hizo. Kwa mfano, kabla ya kuimba “I Love to See the Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95), ungeweza kuwaomba watoto kuinua mikono yao kama wamewahi kuona hekalu. Waalike wafikirie wakati wakiimba kuhusu jinsi wanavyoweza kujisikia wanapoliona hekalu.

Uliza maswali. Kuna maswali mengi ambayo unaweza kuuliza wakati mnaimba nyimbo. Kwa mfano, unaweza kuwauliza watoto wanajifunza nini kutoka kwenye kila mstari wa wimbo. Pia unaweza kuwaomba wafikirie maswali ambayo yanajibiwa na wimbo.

Sikiliza majibu. Waombe watoto kusikiliza majibu ya maswali kama vile “nani?” “nini?” “wapi?” “lini?” au “kwa nini?” Kwa mfano, katika wimbo “Baptism” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 100–101), wangeweza kusikiliza ni nani alimbatiza Yesu na wapi, lini, namna gani, na kwa nini Yeye alibatizwa. Pia ungeweza kuwaomba watoto kusikiliza maneno muhimu au kuhesabu katika vidole vyao ni mara ngapi wanaimba neno fulani.

watoto wakiimba katika mkutano wa sakramenti

Kuwasaidia Watoto Wajifunze na Wakumbuke Nyimbo za Msingi na Nyimbo za Kanisa

Watoto hujifunza wimbo kwa kusikiliza na kuuimba tena na tena. Mara zote yaimbe maneno ya wimbo mpya kwa watoto—usiyasome tu au kuyakariri. Hii huwasaidia watoto kuunganisha sauti ya muziki na maneno. Baada ya wimbo kufundishwa, urejelee wimbo katika njia tofauti za kufurahisha kwa mwaka mzima. Chini kuna baadhi ya mawazo ya kuwasaidia watoto kujifunza na kurejelea nyimbo.

Tengeneza mabango. Onesha mabango yakiwa na maneno kutoka kwenye kila mstari au picha ambayo huwakilisha maneno. Wakati watoto wakiimba, funika baadhi ya maneno au picha mpaka waweze kuimba mstari mzima bila bango. Pia unaweza kuwaalika watoto wakusaidie kutengeneza mabango.

Onesha kwa mfano mpangilio wa sauti. Ili kuwasaidia watoto kujifunza sauti ya muziki wa wimbo, weka mkono wako kwa upana, na wakati ukiimba maneno, peleka mkono wako juu kuonesha sauti ya juu na chini kuonesha sauti ya chini.

Mwangwi. Waalike watoto wawe mwangwi wa sauti yako kwa kurudia kile unachokiimba. Waimbie watoto kirai kifupi cha au mstari, kisha waache wakuimbie kwa kurudia.

Tumia njia tofauti tofauti. Imba nyimbo katika njia tofauti tofauti, kama vile kwa kunong’ona, kwa kuvuma, kwa kupiga makofi mapigo ya muziki, kwa kubadilisha kasi ya muziki, au kuimba ukiwa umekaa au kusimama.

Imbeni katika makundi. Lipe kila darasa au mtu mmoja mmoja kirai cha kuimba wakati wamesimama, na kisha waache wabadilishane virai hivyo mpaka kila darasa au kila mtu awe amepata zamu ya kuimba kila kirai.

Tumia matendo ya mikono. Waalike watoto wafikirie kuhusu matendo rahisi ya mikono ili kuwasaidia kukumbuka maneno na ujumbe wa wimbo. Kwa mfano, unapoimba “Reverently, Quietly” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 26), ungeweza kuwaalika watoto kukunja mikono yao, kuinamisha vichwa vyao, na kugusa mioyo yao wakati wanapoimba mistari husika katika wimbo.

Wasichana wanaimba, wavulana wanaimba. Chora picha ya mvulana na picha ya msichana, na zibandike katika fimbo tofauti. Wakati mkiupitia upya wimbo, inua mojawapo ya picha kuonesha nani anatakiwa kuimba sehemu hiyo ya wimbo.

Oanisha picha na kirai. Andika kila mstari wa wimbo kwenye kipande tofauti cha karatasi, na kisha tafuta picha ambayo inawakilisha kila mstari. Weka picha kwenye upande mmoja wa chumba na karatasi upande mwingine. Imbeni wimbo, na waombe watoto waoanishe picha na maneno.

Miongozo kwa ajili ya Mawasilisho ya Watoto kwenye Mkutano wa Sakramenti

3:3

Chini ya maelekezo ya askofu, mawasilisho ya watoto kwenye mkutano wa sakramenti kwa kawaida hufanyika katika robo ya nne ya mwaka. Kama urais wa Msingi na kiongozi wa muziki, pangeni kukutana mapema katika mwaka pamoja na mshauri katika uaskofu mwenye kusimamia Msingi ili kuanza kujadili mipango ya mawasilisho. Mnapokuwa mmekamilisha mipango, pata ruhusa yake kwa ajili ya mawasilisho hayo.

Mawasilisho sharti yawaruhusu watoto kuwasilisha kile ambacho wao na familia zao wamejifunza kutoka kwenye Agano Jipya nyumbani na katika Msingi, ikijumuisha nyimbo za Msingi walizoimba katika mwaka. Kwa sala fikiria kanuni zipi za injili na nyimbo zinaunga mkono kile ambacho wamejifunza. Katika mwaka mzima, weka kumbukumbu ya hotuba za watoto na uzoefu binafsi kwa ajili ya matumizi wakati wa mawasilisho. Waalike watoto kushiriki maandiko, hadithi na shuhuda zao katika mawasilisho. Wakati ukipanga mawasilisho, fikiria njia ambazo zitasaidia mkusanyiko kufokasi kwa Baba wa Mbinguni na kwa Mwokozi na mafundisho Yao.

Matawi yenye idadi ndogo ya watoto yanaweza kufikiria njia ambazo wanafamilia wanaweza kushiriki pamoja na watoto wao. Mshiriki wa uaskofu anaweza kuhitimisha mkutano kwa hotuba fupi.

Wakati ukiandaa mawasilisho, kumbuka mwongozo ufuatao:

  • Mazoezi yasichukue muda usio wa lazima kutoka kwenye madarasa ya Msingi au familia.

  • Vitu vya kuona, mavazi maalumu, na mawasilisho ya kimtandao havifai kwa ajili ya mkutano wa sakramenti

Ona General Handbook: Serving in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, 12.2.1.2, ChurchofJesusChrist.org.