Watoto na Vijana
Matarajio


“Matarajio,” Mwongozo wa Utangulizi kwa ajili ya Watoto na Vijana wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho (2019)

“Matarajio,” Mwongozo wa Utangulizi kwa ajili ya Watoto na Vijana wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho

Matarajio

Picha
Yesu Kristo

Kuimarisha imani yako katika Yesu Kristo na kukusaidia wewe na familia yako kuendelea katika njia ya agano unapokabiliana na changamoto za maisha.

Tafuta Ufunuo

Picha
msichana akisali

Unaweza kujifunza wewe mwenyewe—hivi sasa katika umri wako—jinsi ya kupokea ufunuo binafsi. Na hakuna kitakacholeta tofauti kubwa zaidi katika maisha yako kuliko hilo!

—Rais Russell M. Nelson, “Tumaini la Israeli,” ibada ya vijana duniani kote, Juni 3, 2018, nyongeza kwenye New Era na Ensign,2, ChurchofJesusChrist.org

Tumia Uhuru wa Kujiamulia

Picha
vijana wakitembea karibu na hekalu

Nia huamua vipaumbele vyetu, vipaumbele vinajenga chaguzi zetu, na chaguzi huamua matendo yetu. Nia tunazozifanyia kazi huamua badiliko letu, kufanikiwa kwetu, na kuwa kwetu.

—Rais Dallin H. Oaks, “Nia,” Ensign au Liahona, Mei 2011, 42

Jenga Mahusiano

Picha
watu wakizungumza

Kila mmoja wetu anahitaji marafiki wa kweli wa kutupenda, kutusikiliza, kutuonesha njia, na kushuhudia ukweli kwetu ili tuweze kudumisha wenza wa Roho Mtakatifu. Ni sharti uwe rafiki huyo wa kweli.

—Rais Henry B. Eyring, “Marafiki wa Kweli,” Ensign Mei 2002, 29

Chapisha