Miito ya Ziada
Majukumu


mwanamume akizungumza na msichana

Wito Wangu kama Mtaalamu wa Ulemavu

Majukumu

Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Waumini wenye Ulemavu

“Waumini wa Kanisa wanahimizwa kufuata mfano wa Mwokozi wa kutoa tumaini, uelewa, na upendo kwa watu walio na ulemavu” (Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 38.8.27). Fokasi yako kama mtaalamu wa ulemavu katika kata ni kuwasaidia watu binafsi wajiandae kufanya na kushika maagano matakatifu.

Mtaalamu wa Ulemavu

Mtaalamu wa ulemavu huwahudumia waumini na viongozi kwa kuwajua watu wenye ulemavu na familia zao; kujibu maswali yanayohusiana na ulemavu na wasiwasi kutoka kwa walezi, viongozi, na wengine; na kuwasaidia watu binafsi wafikie nyenzo za Kanisa, mikutano, na shughuli. Mtaalamu pia anaweza kusaidia kutambua fursa zenye maana kwa ajili ya waumini wenye ulemavu kuhudumu. (Ona 38.8.27.9.)

Majukumu ya Ziada

Watambue na jifunze kuwahusu waumini katika kata yako walio na ulemavu. Kwa sala tafuta mwongozo wa kiungu kuhusu jinsi waumini hawa na familia zao au watoa huduma wanavyoweza kujumuishwa na kusaidiwa. Jitolee kuhudhuria mikutano ya baraza la kata ili kuwasaidia viongozi waelewe jinsi wanavyoweza kuwasaidia waumini wenye ulemavu. Kwa nyenzo za ziada, ona disability.ChurchofJesusChrist.org.

Miongozo na Sera

Kwa ajili ya miongozo juu ya kuwasaidia waumini katika hospitali au vituo vya utunzaji, ona sehemu ya 38.8.43 katika Kitabu cha Maelezo ya Jumla. Kwa ajili ya miongozo juu ya ibada kwa ajili ya watu walio na ulemavu wa kiakili au kimwili, ona sehemu ya 38.2.4 na 38.2.5.