Miito ya Ziada
Karibu


Picha
mchoro wa Yesu amembeba mwanakondoo

Karibu

Karibu kwenye wito wako mpya. Tunashukuru kwa upendo na kujitolea ulivyovionesha kwa Baba wa Mbinguni kwa utayari wako wa kuwatumikia watoto Wake. Kupitia wewe, anaweza kugusa mioyo, kuimarisha uongofu na kuwaongoza wana na mabinti Zake katika njia ya agano.

Nyenzo za Kujua

Kitabu cha Maelezo ya Jumla cha Kanisa na nyenzo za Wito Wangu zitakusaidia uujue wito wako. Soma maelezo hapa chini ili kuelewa vizuri jinsi ya kutumia nyenzo hizi mbili.

Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho hutoa maelekezo ya kina juu ya majukumu yako mbalimbali. Tafadhali tumia kitabu hiki cha maelezo katika huduma yako yote na kwa sala zingatia mwongozo unaotolewa na kitabu hiki.

Wito Wangu: Wito Wangu hutoa muhtasari wa majukumu yako mapya. Viunganishi kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla vimejumuishwa pamoja na mihutasari hii kwa ajili ya taarifa zaidi.

Chapisha