Kumtafuta Kristo kwenye Giza la Ponografia
Katika kuandaa makala kwa ajili ya vijana wakubwa, tunatumia muda mwingi kufikiria kuhusu masuala wanayokabiliana nayo sasa. Yako mengi sana. Lakini tulipokuwa tukipeana mawazo kwa ajili ya mwezi huu, tuliongozwa kwenye mada ambayo imetuathiri sisi binafsi, rafiki zetu, na wengine wasio na idadi: miadi na ponografia. Tulijua kwamba kupanga sehemu hii lingekuwa ni jambo gumu. Hata hivyo ponografia huathiri watu wengi katika kuvunjika mioyo, wakati mwingine katika njia za kuharibu maisha. Na kwa vijana wakubwa waseja, inaweza kufanya wakati ujao uonekane hata usio na uhakika kuliko ambavyo tayari unaonekana, hasa katika kujiandaa kwa ajili ya ndoa.
Kwa kweli tumeona mkono wa Baba wa Mbinguni ukiongoza kazi yetu wakati tulipoanza kupokea hadithi kutoka kwa vijana wakubwa ambao mahusiano yao yameathiriwa na ponografia. Na tunaona kwamba kuna zaidi ya mwangaza hafifu wa tumaini kwenye ndoa za milele zenye furaha, zisizo na uraibu. Kwa nini? Kwa sababu kila hadithi hushuhudia juu ya badiliko la-maisha, uwepo wa-tumaini, nguvu ya uponyaji ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake.
Hivyo ukijikuta katika uhusiano ambao umeathiriwa na ponografia, tunakualika kusoma sehemu ya mwezi huu, yenye makala zilizotolewa na wengine ambao wanajua vyema kwamba mapambano dhidi ya ponografia ni halisi. Makala hizi zinajumuisha mada kama vile jinsi ya kuzungumzia ponografia wakati wa miadi na jinsi ya kuikabili (ukurasa wa 44), jinsi ya kujibu wakati mtu anapokiri kupambana na ponografia (kidijitali pekee), jinsi msamaha na uponyaji vinavyowezekana kwa wote wawili (kidijitali pekee), na jinsi Roho anavyoweza kukuongoza kujua jinsi ya kuendelea katika uhusiano wako (kidijitali pekee).
Tunajua kwamba ikiwa utamtegemea Mwokozi na kumualika Roho katika maisha yako pale unapotafuta majibu, Baba wa Mbinguni atakuongoza kwenye uelekeo sahihi kwa ajili ya hali yako ya kipekee. Giza la ponografia linaweza kuwa limekithiri ulimwenguni, lakini nuru ya Mwokozi ya uponyaji inang’ara juu ya giza lolote. Yote tunayopaswa kufanya ni kumtafuta Yeye.
Kwa moyo wa dhati,
Chakell Wardleigh na Mindy Selu
Mhariri wa Majarida ya Kanisa sehemu ya vijana wakubwa.
Tafuta makala hizi na nyingine zaidi:
-
Katika Vijana Wakubwa kila wiki (kwenye sehemu ya Vijana Wakubwa katika app ya Maktaba ya Injili)
-
Kwenye facebook.com/liahona
Shiriki Hadithi Yako
Je, una hadithi ya kushiriki? Au je, unataka kuona makala kuhusu mada fulani? Unaweza kuwasilisha makala yako au jibu lako kwenye liahona.ChurchofJesusChrist.org.