2019
Miadi na Ponografia
Oktoba 2019


Miadi na Ponografia

Msaada na tumaini katika kukabili ponografia kwenye mahusiano ya miadi.

young man speaking to a young woman

Picha na taswira kutoka Getty Images, imetumika kwa malengo ya kielelezo, imeandaliwa kwa mtindo

Kama vijana wakubwa, sote tunajua kwamba miadi inaweza kuwa ya kuvutia, ya kuogopesha, ya kuridhisha, na ya kutia hofu vyote kwa pamoja. Pale tunapoanza kuwa wawazi kila mtu kwa mwenzake, kiuhalisia tunatamani kujua mengi zaidi kuhusu kila mmoja, na kuongeza uwazi ni muhimu katika kujenga na kukuza mahusiano. Ni nini ndoto zetu, hofu, na imani? Tunahisi vipi kuhusu ndoa na familia? Ni changamoto zipi tumekutana nazo hapo nyuma au sasa ambazo tunapaswa kuzishiriki?

Jinsi ilivyo ya kuogopesha kuzungumzia (au kuuliza) kuhusu matatizo ya ponografia kunavyoweza kuwa, kuto kuzungumzia kunaweza kupelekea matatizo ya kuteketeza baadaye. Kila tatizo la ponografia la mtu ni la kipekee na lenye changamoto, na unaweza hata usijue ikiwa ni tatizo au jinsi ya kulizungumzia pamoja na mtu uliye na miadi naye, hivyo ni muhimu kwamba utafute mwongozo kutoka kwa Roho. Hakuna suluhisho moja kwa kila hali, lakini katika makala hii, tunatoa baadhi ya mapendekezo kwa wale kati yenu mnaoweza kuwa mnauliza:

  • Ni kwa jinsi gani ninaweza kuzungumzia mada ya ponografia na mtu niliye na miadi naye? Na ni wakati gani muafaka kuuliza/kusema?

  • Ni kwa jinsi gani ninaweza kujua ikiwa ninapaswa kusonga mbele katika uhusiano na mtu ambaye ana historia ya matumizi ya ponografia?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kushirikiana pamoja kushinda ponografia?

Kwa Wale Ambao Wamepambana au Ambao Wanapambana

Ikiwa umepambana na ponografia kipindi cha nyuma au ikiwa unapambana sasa, wazo la kuwa na miadi linaweza kukuletea hisia ya kukosa tumaini au wasiwasi. Lakini ikiwa una hamu ya dhati ya kuondoa ponografia kutoka katika maisha yako (au tayari umeiondoa), jua kwamba kwa juhudi zako mwenyewe na kwa msaada kutoka kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, uhusiano wa kudumu, wenye siha unawezekana kwako. Fikiria maswali yafuatayo unapoanzisha uhusiano.

1. Je, Tunahitaji Kweli Kulizungumzia?

Swali la kawaida ni, “Je, ninahitaji kweli kushiriki historia yangu ya matumizi ya ponografia pamoja na mtu niliye na miadi naye, hata kama nimetubu kwa ajili ya hilo?” Au “Je ninahitaji kuzungumzia matatizo yangu ya sasa ya ponografia na mtu niliye na miadi naye?” Kwa ujumla, suala hili linahitaji kujadiliwa—katika muda sahihi na katika njia nyeti. Unapokuwa na mazungumzo haya, weka akilini kanuni kadhaa muhimu:

  • Muda—Mazungumzo yanapaswa kufanyika wakati uhusiano unaendelea katika hali ya dhati ambayo itauhitaji.

  • Uwazi—Mahusiano yanapaswa kujengeka katika uaminifu na uwazi. Japokuwa mtu uliye na miadi naye anaweza kuchagua kusitisha uhusiano, wanahitaji kuelewa asili ya tatizo, maendeleo yako ya sasa katika kulishughulikia, na mpango wako katika kulishughulikia ikiwa litatokea tena siku za baadaye.

  • Msamaha—Kuwa muwazi kuhusu matumizi yako ya ponografia na mtu uliye na miadi naye haimaanishi unahitaji kwenda kwenye maelezo ya undani wakati wa kulijadili. Ikiwa umetubu na unahisi umesamehewa, hupaswi kuhisi hatia kuhusu hilo tena. Bwana hakumbuki dhambi zetu pale tunapokuwa tumetubu (ona Mafundisho na Maagano 58:42), hivyo majadiliano yako na mtu uliye na miadi naye si zaidi kuhusu “kuungama” bali zaidi kuhusu kujenga uaminifu, kushiriki mipango yenu kwa ajili ya uponyaji endelevu, na kupata uungaji wao mkono.

  • Uponyaji—Hata ikiwa umetubu, matumizi ya muda mrefu au ya kiwango cha juu ya ponografia yanaweza kuwa na madhara ya muda mrefu ya kibiolojia, kisaikolojia, kijamii, na kiroho. Mchakato wa uponyaji unaweza kuwa juhudi kubwa na inayochukua muda mrefu, lakini uponyaji kamili na halisi unawezekana. Kupitia mchakato huo, utahitaji msaada na uungaji mkono unaofaa, ambao unapaswa kujumuisha mwenza wako mtarajiwa.

2. Je, Niko Tayari kwa Uhusiano wa Dhati?

Moja ya tofauti kubwa kati ya mtu ambaye yuko tayari kwa ajili ya uhusiano wa dhati na mtu ambaye hayuko tayari ni utayari wao kuwa wawazi kwa mtu waliye na miadi naye. Ikiwa unapambana na ponografia, unaweza aidha kuacha hofu ipeleke uhusiano wako mahala pasipo na uaminifu au kutumia imani kutatua changamoto pamoja.

Japokuwa inaweza kuwa yenye kuleta wasiwasi na ya kuogopesha kushiriki historia yako ya ponografia, kuiepuka kutaongeza tu hisia zako za woga na aibu. Woga wako wa kumpoteza mtu huyo unaweza hata kukusababisha ukatae au kuepuka kushiriki hadithi yote, suala ambalo linaweza kuvunja uaminifu na kuharibu uhusiano wako baadaye.

Kwa upande mwingine, wakati unapoheshimu uhuru wa kuchagua wa mtu uliye na miadi naye, utaheshimu uchaguzi wao wa kubaki katika uhusiano wakijua yote mema na mabaya. Unaweza bado kuwa na hofu juu ya matokeo, lakini ni muhimu kutambua kwamba, kwa kupata taarifa zote, mtu mwingine anaweza pia kukusaidia katika juhudi zako na hamu ya kuondoa ponografia kwenye maisha yako. Lakini haijalishi ikiwa uhusiano wako unaimarika au la, kwa msaada wa Mungu, unaweza kuendelea katika njia ya uponyaji.

Kwa Wale Ambao Wana Miadi na Mtu Ambaye Amepambana

Kwa sababu wastani wa umri wa utambulisho wa kwanza kwenye ponografia ni miaka 11 na ni rahisi sana kufikia ponografia, idadi kubwa ya vijana wakubwa wamepata uzoefu wa ponografia katika njia fulani mpaka kufikia miaka 18. Hii inaweza kuwa kadiri miadi inavyokuwa. Lakini utambulisho si sawa na uraibu, na kuna viwango tofauti vya kujihusisha na ponografia (ona Dallin H. Oaks, “Kupona kutokana na Mtego wa Ponografia,” Liahona, Okt. 2015, 50–55). Lakini habari njema ni kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo unaweza kutoa nguvu na uponyaji kwa wote wanaoutafuta. Haya ni baadhi ya maswali ya kuzingatia wakati uhusiano wako unapoendelea.

1. Lini na Kwa jinsi gani Ninapaswa Kuuliza kuhusu Ponografia?

Kuamua lini na kwa jinsi gani kuongelea hili pamoja na mtu uliye na miadi naye linaweza kuwa jambo la kujadili pamoja na wazazi wako, ndugu zako wakubwa, viongozi wa Kanisa, au yeyote ambaye unadhani atatoa ushauri mzuri. Tafuta njia ambayo inaonekana kuwa sahihi kwako na kisha kuwa na mazungumzo hayo katika wakati muafaka, pale unapojitoa au kuweka maana zaidi katika uhusiano wako.

Hiyo haina maana kwamba unahitaji kuanza kila miadi ya kwanza kwa swali kuhusu maisha yao ya nyuma, lakini pale uhusiano wenu unapokua, unaweza kutafuta mwongozo wa Roho kukusaidia kujua namna gani na wakati gani wa kuuliza kuhusu historia yao ya ponografia.

hands holding two torn pieces of a photograph

2. Je, Ninapaswa Kujibu Vipi?

Wakati wewe na mtu uliye na miadi naye mnapoanza kushiriki hisia zenu za uaminifu, inaweza kuleta uponyaji. Ni muhimu kuwa makini juu ya mawazo yako mwenyewe na hisia pale matumizi ya ponografia yanapofichuliwa—inaweza kukufanya uwe mkosoaji, mwenye hasira, kushikwa na ganzi, au kuhisi kudanganywa. Lakini wakati huohuo, kufichua kwao kunaweza pia kuongeza uaminifu, huruma, upendo, na uelewa kati yenu. Fikiria hisia zao na za kwako mwenyewe wakati unapojibu.

3. Ni Kwa Jinsi Gani Ninasonga Mbele?

Kugundua kwamba mtu uliye na miadi naye anapambana na ponografia inapaswa kuwa sababu ya wasiwasi, lakini usisaliti uaminifu wao kwa kushiriki mapambano yao binafsi kwa watu wengine. Kuzungumza kwa ujasiri na askofu au mtaalamu, au, na rafiki au kiongozi wa kuaminika kwa ruhusa ya mtu uliye na miadi naye, kunaweza pia kusaidia.

Wakati wa kuamua ikiwa utaendelea na uhusiano au la, unapaswa daima kutafuta mwongozo kutoka kwa Roho. Lakini mapendekezo yafuatayo yangeweza pia kusaidia:

  • Waulize ni kiasi gani cha ponografia kimeathiri maisha yao na wapi wapo katika mchakato wa uponyaji. Wanahitaji kuwa wameonesha hamu yao ya kuondoa ponografia kutoka katika maisha yao kwa kuchukua hatua yoyote muhimu inayofaa.

  • Tambua kwamba baadhi ya aina za matumizi ya ponografia (kwa mfano, ponografia ya mtoto) ni kiashirio kikuu kwamba mtu huyo anahitaji msaada wa kitaalamu na anaweza kuwa hayuko salama.

  • Tambua kwamba nguvu ya Upatanisho wa Mwokozi ni halisi. Unaweza kusamehe, na wanaweza kuponywa.

  • Amua kwamba hutatafuta chochote zaidi ya uaminifu mkamilifu katika uhusiano wako na kustahili kufunga ndoa hekaluni.

  • Elewa kwamba uponyaji utachukua muda. Kurudia tena kunaweza kutokea, na wale wanaojaribu kupona watahitaji uungaji wako mkono. Hii hujumuisha kufahamu vichocheo vyao (mambo yanayoweza kuwasababisha kugeukia ponografia) na kuwasaidia au kusaidia kuanzisha ulinzi unaofaa.

  • Ikiwa uhusiano wako unaendelea kuelekea kwenye ndoa, hakikisha kwamba nyote wawili mnakubali kwamba ponografia haikubaliki na haiakisi uhusiano wa kujamiiana wenye siha.

Sehemu muhimu zaidi ya kusonga mbele ni kutegemea kile Roho Mtakatifu anachokupa msukumo kufanya, ambacho kinaweza kuwa chochote mbali na kuendeleza uhusiano ukiwa na uelewa kwamba matumizi ya ponografia lazima yasitishwe kwenye kusitisha uhusiano lakini kuendelea kuunga mkono juhudi za kubadilika. Chochote unachoamua, mtu uliye na miadi naye anapaswa kuelewa kwamba mambo yanaweza kubadilika kutegemeana na maendeleo yao au kutoendelea kwao katika kushinda ponografia.

Kushirikiana Pamoja Kushinda Ponografia

Kushinda ponografia kunaweza kuchukua muda na kuwa vigumu, lakini kunawezekana. Na hatimaye, kushirikiana pamoja katika kuishinda kunaweza kuimarisha uhusiano wenu pale nyote wawili mnapopata uelewa wa kina wa Upatanisho wa Yesu Kristo na kujifunza kuungana mkono kupitia majaribu. Zingatia yafuatayo mnaposhirikiana pamoja kuishinda:

  • Ukurasa wa mtandao wa Kanisa overcomingpornography.ChurchofJesusChrist.org unatoa rasilimali nyingi (ikijumuisha taarifa juu ya programu ya Kanisa ya kupona kutokana na uraibu) ambazo zinaweza kuwasaidia nyote wawili kutafuta mchakato huu wa uponyaji.

  • Fikiria kuwa na mahala na muda maalumu ili kujadili ponografia ili kwamba isiwe fokasi ya uhusiano wenu. Pale mnapolizungumzia, usishushe hadhi au kusimanga. Uhusiano wako unapaswa kuwa sehemu salama ambapo nyote mnaweza kuhisi kupendwa na kuungana mkono, si kuhojiwa au kushushwa hadhi.

  • Matendo ya kiroho yanaweza kusaidia kutoa ulinzi dhidi ya majaribu. Himizaneni kuendeleza na kuimarisha tabia za mara kwa mara za kiroho—ikijumuisha usomaji wa maandiko wenye maana na kuabudu hekaluni (inapowezekana), kuitakasa siku ya Sabato, kuwatumikia wengine, kufunga mara kwa mara, na sala ya dhati—pamoja na ongezeko la hamu ya kuimarisha uhusiano wenu na Mwokozi na Baba wa Mbinguni. Uhusiano huo unaweza kusaidia kupunguza nguvu ya ponografia katika maisha yenu. Ufuasi unatafutwa kote katika maisha, na nguvu tunayopata kama wafuasi wa Kristo itatusaidia kushinda changamoto zetu zote katika maisha, si tu ponografia.

  • Ikiwa juhudi zako mwenyewe hazioneshi kufanikiwa, usiogope au kuona aibu kutafuta msaada wa mtaalamu wa afya katika masuala ya uraibu wa ngono. Wanaweza kukusaidia kupata utambuzi zaidi kwenye kushughulikia matumizi ya ponografia na kukomesha visababishi vyake.

  • Kumbukeni kwamba tumezungukwa na vyombo vya habari visivyofaa ambavyo hutushawishi kufanya dhambi. Ikiwa mtu uliye na miadi naye amerudia tena, haraka jinsi gani wanarudi kwenye njia ni ishara nzuri ya kujitolea kwao kuondoa ponografia katika maisha yao. Lakini ikiwa utaanza kuhisi kama unapata msukumo zaidi wa kuona badiliko kuliko wao wanavyohisi, unapaswa kufikiria upya kuendeleza uhusiano wako.

  • Ushawishi wako kwa mtu uliye na miadi naye unaweza kuwa na nguvu kubwa, lakini haupaswi kuwa sababu ya msingi kwenye badiliko lao la tabia. Hamu ya msingi ya kubadilika inatakiwa kutoka ndani, si kutoka kwako.

Zaidi ya yote, tafuta mwongozo kutoka kwa Baba wa Mbinguni na kumbuka kwamba daima kuna tumaini kupitia Mwokozi. Neema Yake inatosha kutuponya na kutubadilisha. Upatanisho Wake upo kwenu nyote kwa ajili ya kuwapa nguvu, kuwasaidia kusamehe. Hata hivyo, mtu anayepambana na ponografia anapaswa kutafuta usaidizi wa Mwokozi wao wenyewe ili kuishinda. Hakuna yeyote anayeweza kufanya hivyo peke yake. Kuwa na imani, na mtumainie Baba wa Mbinguni. Yeye atakuongoza katika hali yako ya kipekee.