“Zawadi Maalumu,” Rafiki, Agosti 2023, 18–19.
Zawadi Maalumu
“Huyu lazima awe ni Roho Mtakatifu” Mehrimah aliwaza.
Hadithi hii ilitokea huko Ufaransa.
“Mehrimah! Fatima! “Wamisionari wamefika!” Mama aliita.
Mehrimah alifunga kitabu chake cha hadithi za maandiko na kukimbilia sebuleni. Wamisionari walikuwa wakiifundisha familia yao kuhusu Yesu Kristo. Mehrimah na familia yake walikuwa wabatizwe hivi karibuni. Hangeweza kungoja!
Mehrimah aliketi chini pamoja na familia yake.
“Leo tunakwenda kuzungumza kuhusu Roho Mtakatifu,” Mzee Moea’i alisema. “Yeye hutusaidia tuhisi amani na faraja kutoka kwa Baba wa Mbinguni.”
“Yeye pia hutuhimiza tufanye mambo mema,” Mzee Campbell aliongezea. “Na Yeye hutusaidia tujue kile kilicho kweli. Pengine mmewahi kumhisi Roho Mtakatifu hapo awali.”
Mehrimah alifikiria kuhusu wakati alipojifunza kuhusu Kitabu cha Mormoni. Alijihisi mwenye amani na mwenye furaha. Hivyo ndivyo alijua kilikuwa ni cha kweli. Je, Huyo alikuwa ni Roho Mtakatifu?
“Baada ya kubatizwa, unapatiwa kipawa cha Roho Mtakatifu,” Mzee Moea’i alisema. “Hiyo humaanisha Yeye daima anaweza kuwa pamoja na wewe ili kukusaidia na kukuongoza.”
“Wiki hii, zingatia mawazo na hisia zako,” Mzee Campbell alisema. “Tafuta nyakati ambapo Roho Mtakatifu anazungumza nawe.”
Usiku huo wakati wa maombi ya familia, Mehrimah aligundua jinsi alivyohisi ndani yake. Alihisi mtulivu na mwenye furaha. Ilikuwa kama vile mtu alikuwa akimpa kumbatio kubwa. Huyu lazima ni Roho Mtakatifu, aliwaza.
Kanisani siku ya Jumapili, Mehrimah alisikiliza wimbo kuhusu Yesu Kristo. Alihisi furaha sana. Ilimfanya atake kuwasaidia watu wengine. Huyu lazima atakuwa Roho Mtakatifu, aliwaza.
Kabla ya kulala, Mehrimah alisoma kitabu chake cha hadithi za maandiko. Dada yake, Fatima, aliomba zamu. Mehrimah alisema hapana.
Mehrimah aliendelea kusoma. Lakini alihisi vibaya kwa kutompa.
“Samahani,” alimwambia Fatima. “Unataka tusome pamoja?”
Fatima akakaa kando yake. Walifanya zamu kusoma. Mehrimah alihisi vizuri na furaha. Huyu lazima ni Roho Mtakatifu, aliwaza.
Mwishowe siku ya ubatizo wao ilifika. Mehrimah na familia yake walienda kwenye jengo la Kanisa na kubadilisha na kuvaa mavazi meupe.
Mehrimah alikuwa wa kwanza kubatizwa. Maji yalikuwa ya baridi, lakini alifurahia kufanya agano na Baba wa Mbinguni. Mama yake alimfunika kwa taulo. Kisha akawatazama Mama, Baba, na Fatima wakibatizwa.
Mehrimah alibadilisha na kuvaa mavazi yaliyokauka. Na sasa ulikuwa wakati wake wa kuthibitishwa.
Wamisionari waliweka mikono yao juu ya kichwa cha Mehrimah. “Tunakuthibitisha kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho,” Mzee Campbell alisema, “na ninakuambia, mpokee Roho Mtakatifu.” Mehrimaha alihisi joto kote mwilini alipokuwa anasikiliza baraka yote.
Baada ya Mehrimah kuthibitishwa, Mama alimkumbatia. “Je, unahisije?”
“Vizuri kweli,” Mehrimah alisema. Baada ya wao kuweka mikono yao juu ya kichwa changu, nilihisi kitu fulani, na ilihisi kama amani. Alitabasamu. “Ilionekana kama mtu alikuwa ananiambia kuishi maisha mazuri, kuwasaidia watu, na kushika amri.
Je, unajua kile ulichokuwa unahisi? Mama aliuliza.
“Ndiyo, ninajua,” Mehrimah alisema, macho yake yaking’aa. “Huyo alikuwa Roho Mtakatifu!”