Kikao cha Jumapili Asubuhi
Nia ya Mungu ni Kukuleta Nyumbani
Dondoo
Kila kitu kuhusu mpango wa Baba kwa ajili ya watoto Wake wapendwa kimesanifiwa ili kumleta kila mtu nyumbani. …
Je, hii inamaanisha kwamba kila kitu huendana na jinsi tunavyoishi maisha yetu? Hapana, si hivyo. … Kinachojitokeza kimsingi katika mafundisho Yake yote ya kuishi kwenye uwanda wa juu zaidi wa tabia ya maadili ni wito wa maendeleo binafsi, imani katika Kristo yenye kugeuza, kuwa badiliko kuu la moyo. …
Kama tunaamini nia ya mpango wa Baba wenye kuwafikia wote ni kutuokoa sisi, kutukomboa, kutupatia rehema, na kwa hiyo kutuletea sisi furaha, ni ipi nia ya Mwana na kupitia kwa nani mpango huu mkubwa unatimizwa? …
Mapenzi ya Yesu ndiyo mapenzi ya ukarimu ya Baba! Yeye anataka kufanya iwezekane kwa ajili ya kila mmoja wa watoto wa Baba kupokea lengo la mwisho la mpango—uzima wa milele pamoja Nao. Hakuna aliyezuiwa kutokana na uwezekano huu mtakatifu.
Mwokozi, Mchungaji Mwema, anaenda akiwatafuta kondoo wake waliopotea mpaka anawapate. …
Hapana, Yeye haweki vizuizi na vikwazo barabarani; Yeye huviondoa. Hakuachi wewe nje; Yeye anakukaribisha ndani. …
Hii ndiyo habari njema! Mimi nina shukrani isiyo na kifani kwa ajili ya kweli hizi rahisi. Usanifu wa Baba, mpango Wake, dhumuni Lake, nia Yake, matakwa Yake, na matumaini Yake yote ni kukuponya wewe, yote ni kukupa wewe amani, yote kukuleta wewe na wale unaowapenda nyumbani.