Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Mwaminifu hadi Mwisho
Mei 2024


Kikao cha Jumamosi Jioni

Mwaminifu hadi Mwisho

Dondoo

bango

Pakua PDF

Wapendwa marafiki wadogo, leo ningependa kuzungumza nanyi moja kwa moja—vijana wa Kanisa. …

Wakati Daudi akitumia jiwe moja tu kumuua Goliathi, alikuwa ameandaa matano.

Vipi kama kila jiwe la Daudi liliwakilisha nguvu tuliyohitaji kuwa washindi katika maisha yetu? Je, mawe hayo matano yanaweza kuwa ni nini? Nimefikiria uwezekano wa haya:

Kwanza, jiwe la upendo wangu kwa Mungu.

Upendo wetu kwa Mungu na uhusiano wetu wa karibu pamoja Naye hutupatia nguvu tunayohitaji ili kubadili mioyo yetu na kwa urahisi zaidi kushinda changamoto zetu.

Pili, jiwe la imani katika Mwokozi wetu, Yesu Kristo. … Kuwa na imani katika Yesu Kristo humaanisha kwa ukamilifu kutumainia hekima Yake, muda Wake, upendo Wake na nguvu Zake kwa ajili ya kulipia dhambi zetu.

Namba tatu, jiwe la maarifa ya utambulisho wangu wa kweli. …

Kila kitu hubadilika ninapojua mimi ni nani. …

Nne, jiwe la toba yangu ya kila siku. …

Hakuna kitu kinachotuweka huru zaidi kuliko kuhisi msamaha wa Mungu na kujua kwamba tu wasafi na tumepatanishwa Naye.

Jiwe la tano ni jiwe la ufikiaji wangu wa nguvu za Mungu.

Tunawezaje kuchota nguvu hii ya Yesu Kristo? Kutii maagano yetu na kuongeza imani yetu katika Yesu Kristo ndio ufunguo.

Kwa kweli natamani Daudi angekuwa na jiwe moja zaidi; hilo lingekuwa jiwe la ushuhuda wangu. …

Marafiki wapendwa, Kristo ni mwenye shauku ya kutusindikiza kwenye safari ya maisha yetu. …

… Kuna shangwe katika kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo.