Uganda: Mpangilio wa Matukio ya Kanisa
-
Januari 1969–Aprili 1973 • UgandaDiaspora Watakatifu wa Siku za Mwisho waliokuwa wakiishi nchini Uganda walianza kufanya mikutano ya mara kwa mara katika nyumba ya Bessie na Farrel J. Olsen.
-
Juni 8, 1978 • Jijini Salt Lake, Utah, MarekaniUrais wa Kwanza ulitangaza kwamba “haki na baraka zote ambazo injili inatoa sasa zingeweza kupatikana kwa waumini wote wa Kanisa na wanaume wote wenye kustahili wangeweza kutawazwa kwenye ukuhani bila kujali asili au rangi” (Tamko Rasmi 2).
-
1987–90 • UgandaWaganda, ikijumlisha Edward Ojuka, Mary Jean Akello na Charles Osinde, walijiunga na Kanisa wakati wakiishi nje ya nchi kwa ajili ya kazi na elimu. Wengi wao baadaye walirudi Uganda, ambapo walianzisha mikutano katika nyumba zao.
-
Agosti 25, 1990 • Entebbe, UgandaMwongofu wa kwanza mwenyeji wa Uganda alibatizwa ndani ya nchi.
-
Oktoba 29, 1990 • Kampala, UgandaMkutano wa kwanza wa mafunzo ya stadi za nyumbani wa Muungano wa Usaidizi ulifanyika nchini Uganda katika nyumba ya Jean Akello huko Kampala, ukiwajumuisha Mary Jean Akello, Peggy Denton, LuDean Worthen, Julian Mbabazi na Loyce Asio katika mahudhurio.
-
Machi 3, 1991 • KampalaTawi la Kampala lilianzishwa. Likiwa na mahudhurio ya zaidi ya watu 30, waumini walianza kukutana shuleni badala ya kukutana nyumbani kwa Osinde.
-
Aprili 23, 1991 • Kampala na Jinja, UgandaKanisa lilisajiliwa rasmi huko Kampala na Jinja. Takribani mwaka mmoja baadaye, mnamo Juni 16, 1992, Kanisa lilipokea utambulisho wa kitaifa kutoka kwa Bodi ya Taifa ya Taasisi Zisizo za Kiserikali.
-
Juni 2, 1991 • KampalaCharles Osinde na Waganda wengine watano walitawazwa kwenye Ukuhani wa Melkizedeki. Charles aliitwa kama rais wa Tawi la Kampala, akiwa Mganda mwenyeji wa kwanza kuwa rais wa tawi.
-
Oktoba 23, 1991 • KampalaWatakatifu wa Siku za Mwisho wenyeji walikusanyika katika Hoteli ya Sheraton huko Kampala kwa ajili ya uwekaji wakfu wa nchi ya Uganda kwa ajili ya kuhubiriwa injili na Mzee James E. Faust wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
-
Februari 16, 1992 • KampalaWilaya ya Kampala Uganda ilianzishwa huko Colline House Kampala.
-
Mei 16, 1992 • KampalaMary Jean Akello akawa mwalimu wa kwanza wa seminari, na Alice Tiberonda akawa mwalimu wa kwanza wa chuo nchini Uganda. Muda mfupi baadaye, Sam Nabeta akawa mwalimu wa seminari huko Jinja.
-
Desemba 1992 • UgandaAmos Tumwesigye na Robert Kagabo walikuwa watu wa kwanza kutoka Uganda kukubali wito wa kuwa wamisionari, wakihudumu katika Misioni ya Kenya Nairobi. Alice Katagwa, mmisionari wa kwanza wa kike kutoka Uganda, pia aliitwa kuhudumu katika Misioni ya Kenya Nairobi.
-
Februari 1993 • KampalaChristopher Mugimu alianza kuchapisha jarida la Kanisa, likijumuisha historia ya Kanisa nchini Uganda kutoka mwaka 1989 hadi 1992 na waumini wa mwanzo Jean Akello na Robert Kagabo.
-
Juni 20, 1993 • Mukono, UgandaTawi la Mukono lilianzishwa, na Byalusaago Mugimu kama rais wa tawi na Harriet Walusimbi kama rais wa Muungano wa Usaidizi.
-
Desemba 5, 1993 • JinjaWilaya ya Jinja Uganda ilianzishwa.
-
Machi 2000 • UgandaKanisa lililazimika kusajiliwa upya nchini Uganda kwa mwaka mmoja na kisha kuomba kuendeleza usajili hadi wakati ambapo lingeweza kupokea idhini ya miezi 60. Kazi ya umisionari ilipungua kasi, kwani wachunguzi hawakutaka kujihusisha na Kanisa ambalo liko chini ya uchunguzi au ambalo halikusajiliwa.
-
Mei 2006 • Johannesburg, South AfricaSafari ya kwanza iliyopangwa ya kwenda hekaluni ilikuwa na familia tatu na watu binafsi wanane kutoka Uganda ambao walienda Hekalu la Johannesburg, Afrika Kusini kupokea ibada zao za hekaluni.
-
Januari 17, 2010 • KampalaKigingi cha Kampala Uganda kilianzishwa, na Jimmy Carter Okot kama rais na Giles Odongo kama patriaki.
-
Julai 30, 2013 • KampalaWaumini wa mikusanyiko ya Kololo, Nsabya, Makindye, Mutungo na Ntinda walishiriki katika mradi wa Mikono Saidizi kwenye Shule ya Chekechea na ya Msingi ya Earnest.
-
Desemba 2014 • KampalaMkutano wa vijana wakubwa waseja, “Born to Lead,” uliwaleta pamoja zaidi ya Watakatifu wa Siku za Mwisho 180 kutoka makabila na lugha na mikoa tofauti ya Uganda.
-
2015 • KampalaMilly Elwor, Harriet Susan Atim, Christine Nayiga na Anita Nabudde wa urais wa Muungano wa Usaidizi wa Tawi la Ntinda walianzisha harakati za kila mwaka za kukusanya mahitaji ya msingi kama vile nguo, viatu na vyombo vya kupikia; kuviweka katika stoo; ili vitumiwe na wale wanaoweza kuvitumia.
-
Agosti 2016 • KampalaVituo vipya vitano vya historia ya familia vilifunguliwa Kampala.
-
2017 • Kajjansi, UgandaTawi la Kajjansi ya Pili lilianzisha “Mbio za Ghala la Askofu,” ambapo waumini walishiriki katika mbio za masaa mawili, kuanzia kwenye jengo la kanisa na kupita kwenye jumuiya yote. Kila mshiriki alibeba chakula ili kutoa kwenye ghala la askofu.
-
Julai 27, 2019 • KampalaKigingi cha Kampala Uganda North kilifanya mkutano wa wanandoa juu ya kuimarisha uhusiano wa ndoa kwenye nyumba ya mikutano ya Kata ya Ntinda.
-
Novemba 2, 2019 • KampalaFrederick M. Kamya, rais wa Kigingi cha Kansanga, alikaribisha mamia ya wageni kwa ajili ya kuzuru nyumba ya mikutano ya Kansanga. Mgeni rasmi alikuwa Owek. Charles Peter Mayiga, waziri mkuu wa Ufalme wa Buganda.