2011
Chini ya Ukuhani na kulingana na Mpangilio wa Ukuhani
Machi 2011


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Machi 2011

Chini ya Ukuhani na kulingana na Mpangilio wa Ukuhani

Soma kifaa hiki, na kama inavyostahili kizungumzie pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Picha
Relief Society seal

Imani • Familia • Usaidizi

Dada zangu wapendwa, mmebarikiwa jinsi gani! Sio tu kwamba sisi tu washiriki wa Kanisa, lakini pia tu washiriki wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama —“kitengo cha Bwana cha wanawake.”1 Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ni ushahidi wa upendo wa Mungu kwa mabinti zake.

Je moyo wako hauchangamki unapokumbuka kuanzilishwa kwa kusisimua kwa kikundi hiki? Mnamo Machi 17, 1842, Nabii Joseph Smith aliwapangia kina dada “Chini ya Ukuhani na kulingana na Mpangilio wa Ukuhani.”2

Kupangiliwa “chini ya ukuhani” kuliwapatia kina dada mamlaka na mwelekeo. Eliza R. Snow, rais wa pili mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alifunza kwamba Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama “hauwezi kuwa bila ya ukuhani, kutoka na ukweli kwamba unapata mamlaka yake yote na uwezo wake kutoka kwa chanzo hicho.”3 Mzee Dallin H. Oaks wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alieleza, “Mamlaka yatakayo tumiwa na maofisa na waalimu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama … yalikuwa ni mamlaka ambayo yatatiririka kupitia kitengo chao kikiunganishwa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho na kupitia kutengwa kwao kibinafsi chini ya mikono ya viongozi wa ukuhani ambao wamewaita.”4

Kupaniliwa “kulingana na mpangilio wa ukuhani” kuliwapatia kina dada majukumu matakatifu. Julie B. Beck, rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alieleza: “Tunatenda katika njia ya ukuhani—ambayo inamaanisha tunatafuta, tunapokea na kutenda kuhusu ufunuo; kufanya uamuzi katika mabaraza; na kujishughulisha na kutunza watu binafsi mmoja kwa mmoja. Yetu ni madhumuni ya ukuhani ya kujitayarisha wenyewe kwa baraka za maisha ya milele kwa kufanya na kuweka maagano. Kwa hivyo, kama ndugu zetu wanaoshikilia ukuhani, yetu ni kazi ya wokovu, huduma, na kuwa watu watakatifu.”5

Barbara Thompson, Mshauri wa Pili katika urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama.

Kutoka kwa Maandiko

1 Wakorintho 11:11; Mafundisho na Maagano 25:3; 121:36–46

Kutoka kwa Historia Yetu

Wakati wa ujenzi wa Hekalu la Nauvoo, kikundi cha kina dada walitaka kujipanga kusaidia jukumu la ujenzi. Eliza R. Snow aliandika sheria za kikundi hiki kipya. Alipomwonyesha Nabii Joseph, alijibu: “Waambie kina dada matoleo yao yamekubaliwa na Bwana, na ana jambo bora kwao. … Nitawapangia wanawake chini ya ukuhani kulingana na mpangilio wa ukuhani.”6 Muda mfupi baadaye, Nabii aliuambia Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama: “Sasa nawapatia ufunguo katika jina la Mungu, na hiki kikundi kitafurahia, na elimu na uerevu utatiririka kwenu kuanzia wakati huu.”7 Kina dada wanatarajiwa kuinuka hadi kwenye viwango vipya vya utakatifu na kujitayarisha kwa maagizo ya ukuhani yatakayoandaliwa karibuni katika hekalu.

Muhtasari

  1. Spencer W. Kimball, “Relief Society—Its Promise and Potential,” Ensign, Mar. 1976, 4.

  2. Joseph Smith, imedondolewa katika Sarah Granger Kimball, “Auto-biography,” Woman’s Exponent, Sept. 1, 1883, 51.

  3. Eliza R. Snow, “Female Relief Society,” Deseret News, Apr. 22, 1868, 81.

  4. Dallin H. Oaks, “The Relief Society and the Church,” Ensign, May 1992, 36.

  5. Julie B. Beck, “Relief Society: A Sacred Work,” Liahona, Nov. 2009, 111.

  6. Joseph Smith, imedondolewa katika Kimball, “Auto-biography,” 51.

  7. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 451.

Naweza kufanya nini?

  1. Ninawezaje kuwasaidia kina dada ninaowatembelea kusherehekea baraka za kazi takatifu ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama?

  2. Nitafanya nini mwezi huu kuongeza uwezo wangu wa kupokea ufunuo wa kibinafsi?

Chapisha