Vijana
Tafadhali Ponya Moyo Wangu
Katika makumbusho ya kifo cha kakangu , niliakisi wakati wangu tangu yeye alipokufa. Nilikumbuka siyo tu uchungu mkali niliohisi lakini pia baraka Mungu alinipatia .
Kamwe sikuelewa jinsi watu wanaweza kusema kwamba kifo cha mpendwa kinaweza kulete baraka. Sikuweza kuelewa jinsi ninaweza kuwa na shangwe na shukrani kwa kitu ambacho kinaniumiza sana hivi. Kuna usiku mmoja, hata hivyo, ambao ulibadilisha mtazamo wangu kabisa.
Niliamka katikati ya usiku nikiwa na moyo mzito sana kuliko ambavyo nimeshapata. Uchungu ulikuwa unaninyonga. Nilipiga magoti na kusali kwa majonzi kwa Baba yangu wa Mbinguni. Maishani mwangu mwote nilikuwa nimefunzwa kuhusu Upatanisho na uwezo wa Yesu Kristo kuponya kimiujiza. Sasa imani yangu ilikuwa inajaribiwa. Je! Kwa kweli niliamini ? Nilimuomba Baba yangu wa Mbinguni aponye moyo wangu tafadhali. Uchungu ulikuwa mkali sana kwangu kukabiliana nao peke yangu.
Kisha hisia ya amani, faraja, na upendo ikazangaa mwilini mwangu wote. Nilihisi kama Mungu alikuwa amenikumbatia kwa mikono Yake na alikuwa ananikinga mimi kutoka kwa uchungu mkali niliyokuwa nimehisi. Bado mimi ninampeza kakangu , lakini niliweza kuona kwa macho tofauti. Kulikuwa na mengi sana kwangu ya kujifunza kutoka kwa uzoefu huu.
Najua upendo na amani ya Bwana inapatikana. Tunahitaji tu kushiriki.