2013
Utendaji
Machi 2013


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Machi 2013

Utendaji

Soma kifaa hiki kwa maombi na, kama ifaavyo, ukijadili pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe. Kwa taarifa zaidi, nenda kwenyewww.reliefsociety.lds.org.

Imani, Familia, Usaidizi

Nabii wetu, Rais Thomas S. Monson, ametuhimiza sisi “kuenenda mbele kuwaokoa wale wanaohitaji usaidizi wetu na kuwainua hata kwenye barabara ya juu na njia bora. Hii ni kazi ya Bwana, na wakati tunapokuwa katika kazi ya Bwana, tuna haki ya usaidizi wa Bwana.”1

Miaka mingi iliyopita La Vene Call na mwenzi wake wa utembelezi walimtembelea dada aliyekuwa si mshiriki kamili. Waligonga mlango na kumpata mama kijana akiwa amevaa nguo ya kushinda nyumbani. Alionekana kuwa mgonjwa, lakini punde waligudua shida yake ilikuwa ni pombe. Kina dada watembelezi walikaa chini na kuongea na yule mama kijana aliyekuwa na shida.

Baada ya wao kuondoka, walisema, “Yeye ni mtoto wa Mungu. Sisi tunajukumu la kumsaidia yeye.” Kwa hivyo walimtembela kila mara. Kila mara, waliweza kuona na kuhisi mabadiliko kwa wema. Walimuomba dada huyo kuhudhuria Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Ingawaje kwa kusitasita, baadaye alihudhuria kila mara. Baada ya uhimizo, yeye na mmewe na binti yao walihudhuria kanisa. Mmewe alihisi Roho Mtakatifu. Alisema, “Nitafanya kile askofu anapendekeza.” Sasa wanashiriki kikamili Kanisani na wamefunganishwa katika hekalu.2

Kutoka kwa Maandiko

3 Nefi 18:32; Mafundisho na Maagano 84:106; 138:56

Kutoka kwa Historia Yetu

Kuwasaidia wale ambao wamepotoka kurudi kwenye injili ya Yesu Kristo daima imekuwa sehemu ya kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho na mshiriki wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Rais Brigham Young (1801–77) alisema, “Acha tuwe na uenzi wa mmoja kwa mwingine, … na acha wale ambao tunaweza kuona tuwaongoze vipofu mpaka wao waweze kuona njia wao wenyewe.”3

Eliza R. Snow, rais mkuu wa pili wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, kwa shukrani alitambua juhudi za kina dada katika Ogden, Utah, USA, kuimarishana mmoja na mwingine. “Mimi nafahamu vyema kwamba kiwango kikubwa kinachangiwa [kwa hali ya huduma] ambacho kamwe hakifikii vitabu vya [kumbukumbu],” alisema. Lakini kutambua kwamba kumbukumbu za mbinguni zinawekwa za kazi za kina dada wanapoenenda mbele kuwafikia wale mioyo yao imekuwa baridi, alisema: “Rais Joseph Smith alisema muungano huu ulipangwa kuokoa nafsi. Kitabu kingine kinawekwa kuhusu imani yako, ukarimu wako, matendo yako mema, na maneno yako. Hakuna chochote kilichopotea.”4

Muhtasari

  1. Thomas S. Monson, “The Sacred Call of Service,” Liahona, May 2005, 55, 56.

  2. Barua kwa Urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kutoka kwa binti wa LaVene Call.

  3. Brigham Young, katika Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 107.

  4. Eliza R. Snow, katika Daughters in My Kingdom, 83.

Ninaweza Kufanya Nini?

  1. Je! Mimi nina imani ya kumuuliza dada asiyeshiriki kikamili kuhudhuria mkutano wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama pamoja nami?

  2. Je! Kina dada ninaowatunza wanahisi vyema kuniuliza mimi maswali kuhusu injili?

Chapisha