2013
Amani, Kaa Tuli
Machi 2013


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, MACHI 2013

Amani, Kaa Tuli

Rais Thomas S. Monson

Siku moja miaka michache iliyopita, baada ya kushughulikia mambo ofisini, nilihisi msukumo mkubwa wa kumtembelea mjane mzee ambaye alikuwa mgonjwa katika kituo cha utunzaji wa wakongwe katika Mji wa Salt Lake. Niliendesha gari huko moja kwa moja.

Nilipoingia kwenye chumba chake, nilikipata kikiwa tupu. Nikamuuliza mhudumu kuhusua pale alipo na nikaelekezwa hadi kwenye eneo la sebule. Hapa nikampata mjane huyu mwema akizungumza na dada yake na rafiki mwingine. Tukapata kuwa na mazungumzo mazuri pamoja.

Tulipokuwa tunaongea, akaja mtu mlangoni mwa chumba kupata soda kutoka kwenye mashini ya uchuuzi. Akanitazama na kusema, “Vipi, we ni Tom Monson.”

“Ndio,” nikamjibu. “Na wewe unaonekana kama Mhemingway.”

Akathibitisha kwamba yeye alikuwa ni Stephen Hemingway, mwana wa Alfred Eugene Hemingway, ambaye alikuwa amehudumu kama mshauri wangu nilipokuwa askofu miaka mingi iliyopita na ambaye nilimwita Gene. Stephen aliniambia kwamba baba yake alikuwa katika makao haya haya na alikuwa anakaribia kifo. Gene alikuwa anaita jina langu, na familia yake ilikuwa inataka kuwasiliana nami lakini haikuweza kupata nambari yangu ya simu.

Niliomba radhi mara moja na nikaondoka pamoja na Stephen hadi chumbani mwa mshauri wangu wa zamani, ambapo wengine wa watoto wake walikuwa pia wamekusanyika, mke wake akiwa ameaga miaka kadha iliyopita. Wanafamilia walichukulia kukutana kwangu na Stephen katika eneo la sebule kama jibu la Baba yetu wa Mbinguni kwa hamu yao kuu kwamba ningekuja kumwona baba yao kabla aage dunia na kujibu mwito wake. Nilihisi pia kwamba hivyo ndivyo ilivyokuwa, kwani kama Stephen hangeingia chumbani nilipokuwa nikizungumza wakati ule alipoingia, singejua kuwa Gene hata alikuwa kwenye yale makao.

Tulimpa yeye baraka. Roho ya amani ilienea. Tulikuwa na mazungumzo mazuri, baada ya hivyo nikaondoka.

Asubuhi iliyofutata simu iliyoita ilifunua kwamba Gene Hemingway alikuwa ameaga —dakika 20 tu baada ya yeye kupokea baraka kutoka kwa mwanawe nami.

Nilitoa sala za kimya za shukrani kwa Baba wa Mbinguni kwa ushawishi Wake wenye maongozi, ambao ulinisukuma kutembelea kituo cha utunzaji na kunielekeza kwa rafiki yangu mpendwa Alfred Eugene Hemingway.

Ningependa kufikiri kwamba fikra za Gene Hemingway jioni hio—tulipokuwa tunafurahia katika uangavu wa Roho, kushiriki katika maombi ya unyenyekevu, na kutangaza ombi la baraka la ukuhani—zikipiga mwangwi maneno yaliyotajwa katika wimbo “Bwana, Dhoruba Inavuma”:

Kawia, Ewe Mkombozi Mbarikiwa!

Usiniache mimi peke yangu tena,

Na kwa shangwe nitafika bandari ya baraka

Na nipumzike kwenye ufuo wa upepo wa furaha.

Mimi bado naupenda wimbo huo na kushuhudia ufariji unaootoa:

Hata ghadhabu ya bahari yenye tufani

Au mapepo au watu au chochote kitakachokuwa,

Hamna maji yanayoweza kumeza chombo pale alalapo

Bwana wa bahari na ardhi na mawingu.

Yote yatatii kwa upendo mapenzi yake:

Amani, Kaa Tuli.1

Kupitia majozi na majaribu, kupitia hofu na huzuni, kupitia kuumwa na moyo na upweke wa kupoteza wapendwa, kuna uhakika kwamba maisha ni ya milele. Bwana na Mwokozi wetu ni shahidi hai kwamba hivyo ndivyo.2 Maneno yake katika maandiko matakatifu yanatosha: “Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu”(Zaburi 46:10). Nashuhudia juu ya ukweli huu.

Muhtasari

  1. “Master, the Tempest Is Raging,” Hymns, no. 105.

  2. Ona Richard L. Evans, “So Let Us Live to Live Forever,” New Era, July 1971, 18.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Ujumbe huu unaweza kuwafariji wale ambao wamewapoteza mpendwa kwa kifo au wale ambao wanakumbana na majaribu. Kwa zaida ya ujumbe wa Rais Monson, fikiria kushiriki mojawapo wa maandiko yafuatayo, kulingana na yenye msingi wa mahitaji ya wale mnaofundisha: Ayubu 19:25–26;1 Wakorintho 15:19–22; Mosia 24:13–15; Mafundisho na Maagano 122:7–9. Kama ukipata msukumo, unaweza kushuhudia juu ya amani ambayo Mwokozi amekupatia katika majaribu yako.