2013
Tambua, Kumbuka, na Toa Shukrani
Agosti 2013


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Agosti 2013

Tambua, Kumbuka, na Toa Shukrani

Rais Henry B. Eyring

Mungu anauliza kwamba tumtolee shukrani kwa ajili ya baraka zozote tunazopokea kutoka Kwake. Ni rahisi kwetu kuwa wa kutofikiri katika maombi yetu ya shukrani, mara nyingi kurudia maneno yale yale lakini bila nia ya kutoa shukrani zetu kama kipawa cha moyo kwa Mungu. Tunapaswa kutoa shukrani katika Roho (M&M 46:32) ili tuweze kusikia shukrani ya kweli kwa yale Mungu ametupatia.

Tunawezaje kukumbuka hata sehemu ya yote Mungu ametufanyia sisi? Mtume Yohana aliandika kile Mwokozi alitufundisha kuhusu kipawa cha kukumbuka ambacho huja kupitia kipawa cha Roho Mtakatifu: “Lakini Msaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, yeye atawafundisha yote, na kuleta mambo yote kuwakumbusha, yote nimewaambia ninyi” (Yohana 14:26)

Roho Mtakatifu huleta kumbukumbu ya yale Mungu ametufundisha. Na mmojawapo wa njia ambayo Mungu hutufundisha ni kwa baraka zake, na hivyo, tukichagua kutumia imani, Roho Mtakatifu ataleta fadhili za Mungu kwenye kukumbuka kwetu.

Unaweza kujaribu hayo katika sala leo. Unaweza kufuata amri. “Nawe utamshukuru Bwana Mungu wako katika mambo yote” (M&M 59:7).

Rais Ezra Taft Benson (1899–1994) alipendekeza kwamba maombi hupatiana muda wa kufanya hivyo. Alisema: “Nabii Joseph alisema wakati mmoja kwamba moja ya dhambi kubwa ambayo Watakatifu wa Siku za Mwisho watakuwa na hatia ni dhambi ya kutokuwa na shukrani. Nadhania wengi wetu hatujawahi kufikiria kuwa hii ni dhambi kubwa. Tuna uzoefu mkubwa katika maombi yetu na katika uombezi wetu kwa Bwana kuomba baraka za ziada. Lakini wakati mwingine ninahisi tunahitaji kujishughulisha zaidi ya maombi yetu kwa kutoa shukrani na asante kwa baraka tulizopokea tayari. Tunafurahia mengi sana.1

Unaweza kuwa na uzoefu kama huo na kipawa cha Roho Mtakatifu leo. Unaweza kuanza sala ya kibinafsi kwa shukrani. Unaweza kuanza kuhesabu baraka zako na kisha kutua kwa muda. Ukikutumia imani, na kipawa cha Roho Mtakatifu, utakuta kwamba kumbukumbu ya baraka zingine zitafurika katika akili yako. Ukianza kutoa shukrani kwa kila moja yayo, maombi yako yanaweza kuchukua muda mrefu kidogo kuliko kawaida. Ukumbusho utakuja, na hivyo pia shukrani.

Unaweza kujaribu jambo hilo hilo unapoandika katika jarida lako. Roho Mtakatifu amewasaidia watu na jambo hilo tangu mwanzo wa wakati. Unakumbuka kwamba kitabu cha Musa kinasema, “Na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa, ambamo ndani yake kuliandikwa, katika lugha ya Adamu, kwa maana ilitolewa kwa wengi kwa kadiri walivyomlingana Mungu kuandika kwa roho wa mwongozo” (Musa 6:5).

Rais Spencer W. Kimball (1895–1985) alielezea mchakato huo wa kuongozwa katika kuandika “Wale ambao huweka kitabu cha ukumbusho huenda wakamweka Bwana katika kumbukumbu katika maisha yao ya kila siku. Jarida ni njia ya kuhesabu baraka zetu na ya kuacha hesabu ya baraka hizi kwa vizazi wetu.”2

Unapoanza kuandika, unaweza kujiuliza, Ni jinsi gani Mungu alinibariki na wale ninaowapenda leo? Ukifanya hivyo mara nyingi na kwa imani, utajipata ukikukumbuka baraka. Na wakati mwingine utakumbushwa vipawa ambavyo ulishindwa kugundua wakati wa mchana lakini ambavyo basi utajua zilikuwa mguso wa mkono wa Bwana katika maisha yako.

Naomba ili tupate kufanya juhudi kuendelea katika imani kwa kutambua, kukumbuka, na kutoa shukrani kwa yale Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu wamefanya na wanafanya kufungua njia kuenda nyumbani Kwao.

Muhtasari

  1. Ezra Taft Benson, God, Family, Country: Our Three Great Loyalties (1974), 199.

  2. Spencer W. Kimball, “Listen to the Prophets,” Ensign, Mai 1978, 77.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Katika ujumbe wake, Rais Eyring anatualika tukumbuke fadhili za Baba wa Mbinguni katika maombi yetu. Jadili na wale unaowafundisha jinsi kuomba kwa shukrani kunaweza kutusaidia kutambua mkono wa Mungu katika maisha yetu. Fikiria kupiga magoti kuomba na wale unaowafundisha na hupendekeze kwa yeyote anayetoa maombi kwamba atoe shukrani pekee yake.

Unaweza pia kusoma umuhimu wa shukrani kwa kusoma mistari hii kama ziada ya mistari ambayo Rais Eyring alitaja: Zaburi 100; Mosia 2:19–22; Alma 26:8; 34:38; Mafundisho na Maagano 59:21; 78:19; 136:28.