Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Septemba 2014
Wito Mtakatifu wa Yesu Kristo: Mfariji
Kwa maombi jifunze mambo haya na utafute kujua nini cha kushiriki. Kuelewa maisha na wajibu wa Mwokozi kunaweza kuongeza vipi imani yako Kwake na kubariki wale unaowaongoza kupitia ualimu tembelezi? Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye reliefsociety.lds.org.
Yesu Kristo aliahidi, “Sitawaacha kama yatima. Nitarudi kwenu.” (Yohana 14:18). Atatupa “taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo” (Isaya 61:3). Kwa sababu Kristo aliteseka Upatanisho kwa ajili ya kila mmoja wetu, Hatatusahau. “Mwokozi wetu amejitwalia uchungu wetu na mateso yetu na taabu zetu ili aweze kufahamu nini tunachohisi na jinsi ya kutufariji,” Alisema Linda S. Reeves, mshauri wa pili katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa kina Mama1
Kujua kwamba Kristo atatufariji kunaweza kutuletea amani na kutuhimiza kufuata mfano wake kwa kuwahudumia wengine. Rais Thomas S. Monson alisema: “Ufahamu wetu wa injili na upendo wa Baba Yetu wa Mbinguni na, wa Mwokozi utatufariji na kutuimarisha na kutuletea shangwe katika mioyo yetu tunapotembea kwa haki na kushika amri. Hapatakuwa na kitu katika dunia hii kitakachotushinda2
Kutoka kwenye Maandiko
Yohana 14:18, 23; Alma 7:11–13; Mafundisho na Maagano 101:14–16
Kutoka Kwenye Historia Yetu
Elaine L. Jack, Rais wa 12 wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama alisema, “Katika kutembeleana tunasaidiana” Mikono mara nyingi huzungumza kwa jinsi sauti haziwezi. Mkumbatio hueleza mengi. Kicheko kinatuunganisha. Fursa ya kushiriki huburudisha mioyo yetu. Hatuwezi daima kuinua uzito wa yule aliye na taabu, lakini tunaweza kumwinua ili aweze kuubeba vyema.”3
Akina dada wetu watangulizi wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama “walipata nguvu katika upendo na huruma ya kila mmoja” Walipoteseka majaribu ya ugonjwa na kifo, waliomba kwa imani kwa ajili ya kila mmoja na kufarijiana. “Upendo wa Mungu ulitiririka kutoka moyo hadi moyo, “Aliandika Helem Mar Whitney, “hadi mwovu akaonekana kutokuwa na nguvu katika juhudi zake za kututenganisha na Bwana na silaha zake za hila, mara nyingine, ziliondolewa uchungu wake.’”4
© 2014 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa Marekani. Kingereza kiliidhinishwa: 6/14. Tafsiri iliidhinishwa: 6/14. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, September 2014. Swahili. 10869 743