Vijana
Nimeunganishwa Milele na Familia Yangu
Mwandishi anaishi Utah, Marekani.
Wakati nilipokuwa naasiliwa nikiwa na umri wa miaka mitatu, mamangu aliyenizaa alikubali kitendo hicho cha kuasili kukamilika tu kama wazazi wangu wapya watakubali kufanya ibada zangu za Kanisa baada ya kufikia umri wa miaka 12. Alifikiria nilihitaji kuwa mkubwa wa kutosha ili kufanya uchaguzi mimi mwenyewe, lakini ilikuwa vigumu sana kungojea.
Ndio, ilikuwa vigumu kuona marafiki wangu wengi wakibatizwa walipofikia umri wa miaka minane , lakini kile kilichokuwa kigumu zaidi kilikuwa kujua nisingeweza kuunganishwa na wazazi wangu walioniasili na ndugu zangu watano wakubwa hadi nilipofika umri wa miaka 12. Niliogopa kwamba kitu fulani kingeweza kunitokea na nisingeweza kuunganishwa nao.
Kumbukumbu ya 12 ya kuzaliwa kwangu ilipokaribia, tulianza kupanga ubatizo wangu na kuunganishwa na familia yangu. Wazazi wangu waliniacha nichague ni hekalu gani tungeunganishiwa. Daima nilikuwa nimefikiria kwamba Hekalu la San Diego California lilikuwa la kupendeza zaidi, hivyo basi familia yangu yote ilikubali kusafiri hadi California kwa ajili ya kuunganishwa.
Nisingengoja kuwa familia ya milele pamoja na wazazi wangu na ndugu zangu. Wakati wa kuunganishwa kwangu, nilihisi Roho wa Mungu kwa nguvu sana hata kwamba ni vigumu kusema kwa maneno. Sasa kwa vile hatimaye nimeunganishwa na familia yangu, hisia zangu za hofu zimebadilishwa na kuwa faraja na amani, nikijua sasa nimeunganishwa nao milele.