2016
Kweli katika Imani
Julai 2016


Vijana

Kweli katika Imani

Rais Monson anasimulia hadithi kuhusu familia moja ya waanzilishi na kisha ananukuu hotuba ya Rais George Albert Smith: ”Je, ninyi mtaishi wakweli katika imani ya babu zenu? … Jitahidini muwe wastahiki wa dhabihu zote walizofanya kwa ajili yenu.” Hata ikiwa wewe una nasaba ya uanzilishi ama wewe ni muumini wa Kanisa kizazi cha kwanza, je wewe hutafuta mifano ya imani kwa mwongozo na nguvu? Hapa kuna njia ambayo unaweza kuanza:

1. Tengeneza orodha ya watu10 unaowaenzi. Wanaweza kuwa ni wana familia yako mwenyewe (wenda zao ama wa sasa) marafiki, viongozi wa Kanisa, ama watu katika maandiko.

2. Andika sifa walizonazo ambazo unazipenda. Je, mama yako ni mvumilivu sana? Labda rafiki yako ni makrimu kwa wengine. Labda unapenda ujasiri wa Kapteni Moroni.

3. Chukua sifa moja kutoka kwenye orodha na ujiulize mwenyewe, Ninaweza vipi kupata sifa hii? Je, ninahitajika kufanya nini kuikuza katika maisha yangu?”

4. Andika mipango yako kwa ajili ya kuendeleza sifa hii na kuiweka mahali unapoweza kuiona kila mara, ili kukukumbusha lengo lako. Sala kwa ajili ya msaada wa Baba wa Mbinguni na utazame maendeleo yako kila mara. Mara unapohisi umeendeleza vya kutosha sifa hii, unaweza kuchagua sifa ingine ya kufanyia kazi.

Kumbuka kwamba tunapoendeleza sifa kuu ndani yetu, si tu tunaheshimu imani ya mababu zetu na dhabihu walizofanya, bali pia tunaweza kuwa na ushawishi mzuri kwa wale walio karibu nasi.

Chapisha