Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Julai 2016
Kweli katika Imani ya Babu Zetu
John Linford alikuwa na umri wa miaka 43 wakati yeye na mkewe, Maria na wana wao watatu walifanya uamuzi wa kuacha nyumba yao huko Gravely, Uingereza, na kusafiri maelfu ya maili kujiunga na Watakatifu katika bonde la Great Salt Lake. Walimuacha mwana wao wa nne, ambaye alikuwa anahudumu misheni, na kuuza mali yao, na huko Liverpool wakaabiri meli Thornton.
Safari yao ya baharini hadi Jijini New York, na kisha ya nchi kavu hadi Iowa, haikuwa na matatizo. Hata hivyo, shida zilijitokeza, punde baada ya kina Linford na Watakatifu wa Siku za Mwisho wengine ambao walikuwa wamesafiri kwenye Thornton walipoondoka Mji wa Iowa mnamo July 15, 1856. kama sehemu ya kikosi cha mkokoteni cha James G. Wlillie kulichokumbwa na shida.
Hali ya hewa kali na safari ya sulubu iliwaumizi wengi katika kikosi hicho, ikijumuisha John. Hatimaye akawa mgonjwa sana na myonge hata kwamba asiweze kuvuruta mkokoteni. Kufikia wakati kikosi hiki kilipowasili Wyoming, hali yake ilikuwa imezorota sana. Timu ya wakombozi kutoka Jijini Salt Lake ilifika Oktoba 21, masaa machache tu baada ya safari ya John hapa duniani kumalizika. Aliaga dunia mapema asubuhi hiyo karibu na kingo za Mto Sweetwater.
Je, John alighadhibika kwa sababu aliacha faraja na starehe na kuchukua shida, ufukara, na dhiki kwa ajili ya kuipeleka familia yake Sayuni?
“La Hasha,” alimwambia mkewe kabla tu ya hajaaga. “Nina shukrani tulikuja. Mimi sitakuwa hai kufika Salt Lake, lakini wewe na wavulana mtafika, na sijuti yale yote tumeyapitia kama wavulana wetu wataweza kukua na kulea familia zao katika Sayuni.”1
Maria na wanawe walimaliza safari yao. Wakati Maria alipoaga dunia takriban miaka 30 baadaye, yeye na John waliacha nyuma urithi wa imani, wa huduma, wa uchaji, wa dhabihu.
Kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho ni kuwa mwanzilishi, kwani maelezo ya mwanzilishi ni “mtu anayetangulia mbele ili kuandaa au kutengeneza njia kwa wengine kufuata.”2 Na kuwa mwanzilishi ni kuwa umejitoa dhabihu. Ijapokuwa waumini wa Kanisa sasa hawaombwi kuacha nyumba zao na kufanya safari kwenda Sayuni, mara zote sharti waache tabia za awali, desturi zizokita mizizi, na marafiki wapendwa. Baadhi yao hufanya maamuzi ya kuwaacha wana familia ambao wanapinga ushiriki wao katika Kanisa. Watakatifu wa Siku za Mwisho husonga mbele, hata hivyo, wakiomba kwamba wapendwa wao wataelewa na kukubali.
Mapito ya waanzilishi si rahisi, lakini tunafuata katika nyayo za Mwanzilishi mkuu—hata Mwokozi—ambaye alitangulia mbele yetu, alituonyesha njia ya kufuata.
“Njoo, unifuate,”3 Alialika.
“Mimi ndimi njia, na kweli na uzima.”4 Alisema.
“Uje kwangu,”5 Aliita.
Njia hii inaweza kuwa ngumu sana. Wengine wanaipata kuwa vigumu kustahimili matamshi yenye dhihaka na uchafu ya wale wajinga ambao wanakejeli usafi, uaminifu na utii kwa amri ya Mungu. Lakini ulimwengu umedunisha uzingatiaji wa kanuni. Wakati Nuhu alipoamuriwa kujenga safina, wale watu wajinga walitazama anga kavu na kisha kudhihaki na kucheka—hadi mvua ikaja.
Katika bara Amerika karne nyingi zilizopita, watu walitilia shaka, wakabishana, na kukaidi mpaka mto ulipoichoma Zarahemla, mchanga kufunika Moroniha, na maji yalipozonga Moroni. Kuzomea, kejeli, upunjufu, na dhambi havikuwepo tena. Badala ilikuwa kimya kizito, giza totoro. Subira ya Mungu ilikuwa imeisha, ratiba Yake akatimia.
Maria Linford kamwe hakupoteza imani licha ya mateso huko Uingereza, ungumu wa safari yake kwenda “mahali ambapo Mungu … alikuwa ametayarisha,”6 na majaribu yaliyotokea baadaye akayamvulia kwa ajili ya familia yake na Kanisa.
Mnamo 1937 kwenye sherehe ya maadhimisho ya Maria, Mzee George Albert Smith (1870–1951) aliuliza uzao wake: “Je, ninyi mtaishi wakweli katika imani ya babu zenu? … Jitahidini muwe wastahiki wa dhabihu zote walizofanya kwa ajili yenu.”7
Tunapojaribu jaribu kujenga Sayuni katika mioyo yetu, katika jamii yetu, na katika nchi zetu, acheni tukumbuke ujasiri thabiti na imani ya kudumu ya wale ambao walitoa vyao vyote ili kwamba tuweze kufurahia baraka za injili ya urejesho, kwa matumaini yake na ahadi kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.
© 2016 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa USA. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/16. Tafsiri iliidhinishwa: 6/16. Tafsiri ya First Presidency Message, July 2016. Swahili. 12867 743