Ujumbe wa Mwalimu Mtembeleaji, Julai 2016
Uwezo Wetu katika Uzazi
Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute kujua kitu cha kushiriki. Je, kuelewa “Tangazo kwa Ulimwengu” kutazidisha vipi imani yako katika Mungu na kubariki wale unaowachunga kupitia ualimu wa kutembelea? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.
“Ilikuwa muhimu kwamba watoto wa Mungu kuzaliwa kimwili na kuwa na nafasi ya kuendelea mbele hata uzima wa milele,” alifunza Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. “Katika nuru hii ya madhumuni ya msingi ya mpango mkuu wa furaha, mimi naamini kwamba hazina ya msingi hapa duniani na mbinguni ni watoto wetu na uzao wetu.”1
Mzee Neal A. Maxwell wa Jamii ya Mitume kumi na Wawili alisema:
“Tunaamini katika familia, na tunaamini katika watoto. …
“‘… Mungu akawabarikia [Adamu na Hawa], Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi’ [Mwanzo 1:28]. …
“Amri hii haijasahaulika ama kuwekwa kando katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.2
Ingawa sio wengi wetu watakuwa wazazi katika maisha haya, tunaweza kulea watoto wa kila umri. Tunafurahia baraka za kuwa sehemu ya familia ya Baba wa Mbinguni, na tunapata furaha na changamoto za kuwa sehemu ya familia ya ulimwenguni. Na kwa wengi, uzazi unawangonja katika milele iliyo mbele.
Maandiko ya Ziada
Hadithi Hai
“Sauti nyingi katika ulimwengu leo zinapuuza umuhimu wa kupata watoto ama kushauri kucheleesha ama kupima idadi ya watoto katika familia,” Mzee Andersen alisema. “Mabinti wangu juzi walinielekeza kwenye blogi iliyoandikwa na mama Mkristo (ambaye si wa imani yetu) mwenye watoto watano. Alisema: ‘[Kukua] katika hii tamaduni, ni vigumu sana kupata mtazamo wa biblia wa umama. … Watoto wanapatiwa umuhimu wa chini zaidi ya chuo. Chini ya safari za ulimwenguni kwa kweli. Chini ya uwezo wa kutembea usiku kwa nafasi yako. Chini ya kufanya mazoezi katika ukumbi wa mazoezi. Chini ya kazi yoyote unayoweza kupata ama kutarajia kupata.’ Kisha akaongezea: ‘Umama si jambo la burudani, ni mwito. Hauwezi kukusanya watoto kwa sababu unawaona kuwa warembo kuliko stempu. Sio kitu cha kufanya wakati una wakati wa ziada, Ni kile Mungu amekupa muda kwa ajili yake.’”3
© 2016 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa Marekani. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/16. Tafsiri iliidhinishwa: 6/16. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, July 2016. Swahili. 12867 743