2016
Familia Ni za Milele.
Agosti 2016


Watoto

Familia Ni za Milele

Kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo na urejesho wa funguo za ukuhani, tunaweza kuishi na familia zetu milele. Ni nini unachokipenda kuhusu familia yako? Fuatilia maelekezo haya ili kutengeneza mnyororo wa karatasi wa kusherekea familia yako.

  1. Kunja kipande cha karatasi nusu mara mbili ili kiwe mshipi mrefu.

  2. Chora mtu akiwa mikono inanyoshwa kufikia nchi zilizokunjwa.

  3. Kata picha ya mtu huyo. Usikate pale mikono inagusa nchi zilizokunjwa.

  4. Ikunjue. Andika au chora kitu ambacho unapenda kuhusu kila mwanafamilia.

  5. Unga kwa gamu pamoja kama una familia kubwa.

Chapisha