Ujumbe wa Mwalimu Mtembeleaji, Agosti 2016
Kutunza Familia Pamoja
Kwa maombi jifunze ujumbe huu na utafute kujua kitu cha kushiriki. Je, kuelewa “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” kutazidisha vipi imani yako katika Mungu na kubariki wale unaowachunga kupitia ualimu wa kutembelea? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.
“Mume na mke wana jukumu takatifu la kupendana na kutunzana na kwa watoto wao.”1 “Nyumbani ndiyo mahabara ya Mungu ya upendo na huduma,” alisema Rais Russell M. Nelson, Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.
Baba yetu wa Mbinguni anataka waume na wake kuwa waaminifu mmoja kwa mwingine na kustahi na kutendea watoto kama uzao kutoka kwa Bwana.”2
Katika Kitabu cha Mormoni, Yakobo alisema kwamba upendo ambao waume waliokuwa nao kwa wake zao, na upendo ambao wake waliokuwa nao kwa waume wao, na upendo ambao wote walikuwa nao kwa watoto ilikuwa ndiyo sababu Walamani wakati mmoja walikuwa wema zaidi kuliko Wanefi (ona Yakobo 3:7).
Mojawapo wa njia bora za kualika upendo na uwiano katika nyumba zetu ni kwa kuongea kwa ukarimu kwa wanafamilia wetu. Kuongea kwa ukarimu huleta Roho Mtakatifu. Dada Linda K. Burton, Rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, anatuomba tufikirie: “Ni mara ngapi kwa kusudi ‘tunasemezana maneno ya ukarimu’?”3
Maandiko ya Ziada
Hadithi Hai
Mzee D. Todd Christofferson wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alishiriki uzoefu wa utotoni ambao ulimsisitizia umuhimu wa kuipenda familia. Wakati yeye na kaka zake walikuwa wavulana, mama yao ulifanyiwa upasuaji mkali kwa sababu ya saratani ambao ulikuwa na maumivu sana kwake kutumia mkono wake wa kulia. Akiwa na familia ya wavulana, kulikuwa na kupiga pasi kwingi, lakini mama alipiga pasi, mara nyingi alisitisha na kwenda kwenye chumba chake cha kulala kulia hadi uchungu ulipotulia.
Wakati babake Mzee Christofferson alipogundua kilichokuwa kinatendeka, kisiri alikaa na njaa wakati wa mchana kwa karibu mwaka mzima ili kuweka akiba hela za kutosha kununua mashine ambayo ilirahisisha kupiga pasi. Kutoka na upendo wake kwa mkewe, aliweka mfano wa kutunza miongoni mwa wavulana wake. Kuhusu jambo hili la upendo, Mzee Christofferson alisema, “Mimi sikujua dhabihu ya baba yangu na kitendo cha upendo kwa ajili ya mama wakati huo, lakini sasa ambapo najua, mimi najisemeza mwenyewe, “Hapo kuna mwanaume kamili.’”4
© 2016 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa Marekani. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/16. Tafsiri iliidhinishwa: 6/16. Tafsiri ya Visiting Teaching Message, August 2016. Swahili. 12868 743