Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Agosti 2016
Tumaini la Upendo wa Familia ya Milele
Katika vipawa vyote Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo anavyotoa kwa watoto Wake, kikuu ni uzima wa milele (ona M&M 14:7). Kipawa hicho ni kuishi katika uwepo wa Mungu Baba na Mwanawe Mpendwa milele na milele. Ni tu katika ufalme wa juu katika falme za Mungu, selestia, ambapo kamba za upendo za maisha ya familia zitaendelea.
Sisi sote tunatumainia furaha ya kuishi katika familia yenye upendo. Kwa baadhi yetu, ni hisia ambayo hatujaipata—hisia tunajua inawezekana lakini bado haitapatikana. Tunaweza kuwa tumeiona katika maisha ya wengine. Kwa baadhi yetu, upendo wa familia umeonekana kuwa halisi zaidi na wenye thamani wakati kifo kinapotutenganisha na mtoto, mama, baba, kaka, dada, ama babu mwenye upendo na mpendwa.
Sisi sote tumeishahisi tumaini kwamba siku moja tunaweza kuhisi tena upendo wa huyo mwanafamilia tuliempenda sana na sasa tunatamani kumkumbatia tena.
Baba wa Mbinguni mwenye upendo anajua mioyo yetu. Kusudi lake ni kutupa furaha (ona 2 Nefi 2:25). Na kwa hivyo alitoa kipawa cha Mwanawe ili kuwezesha furaha ya miungano ya familia inayoendelea milele. Kwa sababu Mwokozi alivunja kamba za kifo, sisi tutafufuliwa. Kwa sababu alifanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, sisi tunaweza, kwa imani na toba, kuwa wastahiki wa ufalme wa selestia, ambapo familia uunganishwa pamoja katika upendo milele.
Mwokozi alimtuma Nabii Eliya kwa Joseph Smith kurejesha funguo za ukuhani (ona M&M 110). Kwa funguo hizo, zikaja nguvu za kufunganisha, zikitoa kipawa kikuu katika vipawa vya Mungu kwa watoto Wake—uzima wa Milele katika familia zilizounganishwa milele.
Ni toleo ambalo kila mtoto wa Mungu ambaye uja ulimwenguni anaweza kudai. Theluthi moja ya watoto Wake wa kiroho ilikataa toleo Lake katika dunia ya kiroho. Kutokana na ukosefu wa imani ya kutosha na kisha uasi wa wazi, walichagua kamwe kutokupata furaha ya kipawa cha Baba wa Mbinguni cha familia za milele.
Kwa wale ambao walipasi mtihani muhimu katika ulimwengu wa kiroho kabla kuzaliwa na kwa hivyo kuhitimu kupokea kipawa cha miili yenye kufa, uchaguzi mkuu wa uzima wa milele bado ni wetu. Kama tumebarikiwa kupata injili ya urejesho, tunaweza kuchagua kufanya na kushika maagano na Mungu ambayo yanatuhitimisha kwa uzima wa Milele. Tunapovumilia uaminifu huo, Roho Mtakatifu atathibitisha matumaini yetu na imani kwamba tuko kwenye njia ya uzima wa milele, kuishi katika familia milele katika ufalme wa selestia.
Kwa wengine, hiyo furaha ya milele inaweza kuonekana ukungu ama hata tumaini linalofifia. Wazazi, watoto, kina kaka, na kina dada wanaweza kuwa walifanya chaguo ambazo zinaonekana kuwazuia kutoka kwa uzima wa milele. Unaweza hata kushangaa kama wewe bado umehitimu kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.
Nabii wa Mungu wakati mmoja ilinipa ushauri ambao hunipa amani. Nilikuwa na wasiwasi kwamba chaguo za wengine zingeweza kuzuia familia yetu kuwa pamoja milele. Alisema, “Una wasiwasi juu ya shida usiyostahili kuzingatia. Wewe ishi kwa ustahili wa ufalme wa selestia, na mipangilio ya familia itakuwa mizuri ajabu kuliko unavyofikiria.”
Kwa wote ambao uzoefu wao wa kibinafsi ama ambao ndoa na watoto—ama ukosefu wake—unatia ukungu katika matumaini yao, mimi natoa ushuhuda wangu: Baba wa Mbinguni anawajua na anawapenda kama watoto Wake wa kiroho. Wakati ukiwa pamoja Naye na Mwanawe Mpendwa kabla ya maisha haya, Wao waliweka ndani ya moyo wako tumaini la kuwa na uzima wa milele. Nguvu za Upatanisho wa Yesu Kristo zikifanya kazi na Roho Mtakatifu akiongoza, unaweza kuhisi sasa na utahisi katika ulimwengu ujao upendo wa familia ambao Baba yako na Mwanawe Mpendwa wanayotaka wewe hupokee.
Mimi nashuhudia kwamba unapoishi kwa ustahili wa ufalme wa selestia, ahadi ya kinabii kwamba “mipangilio ya familia iitakuwa mizuri ajabu kuliko unavyofikiria” itakuwa yako.
© 2016 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imechapishwa Marekani. Kiingereza kiliidhinishwa: 6/16. Tafsiri iliidhinishwa: 6/16. Tafsiri ya First Presidency Message, August 2016. Swahili. 12868 743